Rais Magufuli, tafadhali angalia madudu yaliyopo TPA, na bodi nzima ya TPA kuna mengi yakutisha pato la taifa linapotea

mahingah

Senior Member
Oct 4, 2016
199
275
Bandari ni moja ya chanzo kikubwa cha uchumi wetu, kuna baadhi ya mambo yanatokea TPA kwanzia bandari ya Dar es salaam na Bandari za maziwa mfano Mwanza, Kigoma na Nyasa.

Kuna upigaji wa hali ya juu katika hizi bandari wakubwa wanapiga kesi zinapelekwa kwa wafanyazi ili kulinda cheo, tunakuomba fanya uchunguzi kuanzia kwa Director General (DG) na wafuasi wake; pesa za nchi zinapigwa na kesi wanapewa wengine, tunakuomba fanya uchunguzi kwa hili swala.
 
Magu ameshindwa sana kuondoa wizi, ubadhirifu na ufisadi kwa miaka yote 5 tunalishwa uongo mtupu mambo mengi yamekuwa mabaya zaidi ya hapo kabla.
 
Moja ya kauli ya DG siku moja ambayo sikuitarajia alikuwa anamwambia Director mmoja wa kitengo.

" Nyie mmekula sana mema ya bandari kwa mda mrefu, sasa pumzikeni ni zamu yetu wapya kusafiri " Hii ilikuwa ni safari ya kikazi ambayo huyo Director alitakiwa awemo, nilimshangaa sana japo sikuweza kuelewa nini ana maanisha hasa.

Naungana na wewe pale kuna upigaji mwingi sana, lakini lazima ujue namba one anampenda sana DG na sidhani kama yuko tayari kumtoa pale kipindi hiki akiwa anajiandaa kwenda kugombania ubunge.
 
Umeongea lakini hujatupa viashiria, kuna mdau mmoja hapa alitoa tuhuma za MSD humu jamii forum, akatoa na vishiria vyake vya kueleweka, baadae kidogo watu wakatumbuliwa.

Hizi tuhuma naziona kama zina-hang.
 
Wajanja wanapiga pesa si mchezo, ila awamu hii wamebanwa kiasi. Awamu iliyopita ilikuwa hapana chezea!
 
Umeongea lakini hujatupa viashiria, kuna mdau mmoja hapa alitoa tuhuma za MSD humu jamii forum,akatoa na vishiria vyake vya kueleweka,baadae kidogo watu wakatumbuliwa.

Hizi tuhuma naziona kama zina-hang......
Mbona nimesema, kuna wizi wa pesa na watuwengine wanabambikiwa kesi
 
Mkuu weka specific cases namna hii hatupati ujumbe, be serious kwa hili weka ishu bayana tuingie kazini
Nashindwa kuongea coz kesi bado ipo, kinachoniuma watu wanapiga pesa kesi wanapewa wengine,fatilia sasa yanaendelea kwenye maziwa makuu
 
Mbona nimesema, kuna wizi wa pesa na watuwengine wanabambikiwa kesi

Wanaiba vipi hizo pesa wakati malipo ni kwa njia ya mtandao? au ndio ile kuhujumu mtandao na kusema system iko down ili wapitishe mambo?

Fafanua kidogo au kwenye waiver ya storage wana-uplift kiujanja ujanja? Ila navyojua TPA the whole operations ni computerized sasa upigaji unatokea wapi?
 
Back
Top Bottom