Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Huu ushuzi apeleke kwao chato hajui anapita tuu, wanaotaka kusoma wasome no matter what aache upuuzi wake
 
Yuko sawa kabisa kama mwanaume miaka 30 kwann mwanamke yy aendelee na shule uonevu uo kwa wanaume

Hahahahaha. Mmoja anafungwa miaka thelathini, mwingine anapewa adhabu inayolingana na hiyo ya kwenda kulea mtoto milele kwao, hakuna kurudi shuleni. Wote ni wakosefu..
 
Nyie watu mna matatizo in common. Angetangaza kuwa wenye mimba / waliojifungua wataendelea kusoma , mngemsimanga zaidi kuwa amewapa watoto ruksa ya ngono. Ila tatizo nyie ni watu wa kupinga tu kila kitu.

Hongera Magufuli. Mimba siyo ajali inaepukika.

Spirit uliyonayo hapa kutetea wfnz wabebe mimba ungeitumia kuhimiza waepuke mimba na mazingira yake
 
Kwenye huu mjadala tuangalie lugha inayotumika.

Anasema, kwa msisitizo kwamba sitasomesha. Sawa tunajua yeye ni Rais wa nchi. Lakini anasomesha yeye kama Pombe kwa hela yake au ni serikali anayoingoza?

Kusema hatasomesha au serikali yake haitasomesha kuna tofauti kubwa kwenye mentality ya kiongozi.

Inaleta picha ya jinsi anavyoyachukulia madaraka aliyopewa.

Je anajiona ni mtumishi wa watu au wananchi6ndiyo wanaomtumikia?
 
Mitazamo ya watu lazima itofautiane, usimlaumu mtu kuwa anapinga kila kitu kwa sababu hata kukubali kila kitu pia ni kosa. Lazima tujadili kama debate afu baadae tunaweza kupata muafaka na msimamo wa pamoja.
 
Kwenye huu mjadala tuangalie lugha inayotumika.

Anasema, kwa msisitizo kwamba sitasomesha. Sawa tunajua yeye ni Rais wa nchi. Lakini anasomesha yeye kama Pombe kwa hela yake au ni serikali anayoingoza?

Kusema hatasomesha au serikali yake haitasomesha kuna tofauti kubwa kwenye mentality ya kiongozi.

Inaleta picha ya jinsi anavyoyachukulia madaraka aliyopewa.

Je anajiona ni mtumishi wa watu au wananchi6ndiyo wanaomtumikia?
Kauli zake nyingi ni za ubinafsi...kauli kama serikali yangu,utawala wangu,sitatoa fedha kusomesha wazazi,mara anasema alichukua form mwenyewe hakusaidiwa na mtu....kuna umimi fulani kwenye kauli zake..kauli zinatokana na mawazo na mawazo ndio tabia ya mtu..mtu hawezi kuwa tofauti na mawazo yake..mawazo ya watu wa namna hii hupelekea tabia ya kutaka kunyenyekewa na kuabudiwa,hawataki kupingwa wala kumskiliza mtu mwingine,atajiaminisha hii nchi ni yake na hamna nwingine kama yeye..na hapo ndio itakuja mwanzo wa uraisi wa milele..
 
Mabadiliko katika jamii yoyote ni lazima na Uongozi wowote utakuwa na malengo binafsi, namuunga mkono Rais ila jamani si kwake tu, na kwa mwengine yyt haya maneno machafu yaacheni, nachukizwa tu na baadhi ya vitendo vya wanasiasa Afrika kwanza kuwa uchaguzi umeisha halafu bado wanazozana au kuzungumzana, pili kuwa masuala ya msingi na hakki za Raia kuzinadi kuwa maendeleo, kweli neno maendeleo ni kutoka sehemu, mahala flani kwenda mahala flani lkn yanazingatio, maana Hatua kubwa ni hisia za Raia kwenye kutafuta aman ya Roho, hv anapokuja mtu kusema Maendeleo ni barabara kutoka mahala flani mpaka mahala flani ndio maendeleo? umekamilisha hisia za Raia? au kumrahisishia na kumpa tu hakki yake ya msingi, kurahisisha usafiri maana wapo wengi watatumia barabara ile na maisha bado yapo chini sina maana kuwa zisejengwe bali Rais gani duniani towa Afrika kanadi kuwa maendeleo ni barabara au maji wakati ni hakki zao.

Kwa kumaliza tu ni kwamba Juhudi za kuinua Tanzania ya Viwanda ihusike vyema kwenye akili zetu ni dhana njema kustawisha Uchumi wa Taifa hongera Rais lkn Usiisahau Zanzibar maana ni Nusu ya Tanzania.

Ahsanteni wadau.
 
Tulicheza na kupoteza Rasilimali muhim sana Tanzania basi hata bikra na Heshima za hawa watoto binafsi mm si muumini mwema wa Mambo ya Wamagharibi lkn sisi wenyewe tayar tumekuwa tukipendezwa na hayo sasa hata kuchukizwa tuanze sisi na anapokuja mwenzetu tuamke maana usipoamka kwa mdomo utamwagiwa maji, hivi wewe kama mwanafunzi mzazi na Jamii inakukataza kuzini au kuwa na mahusiano ya kimapenzi machafu tena ukikiri hilo iwe dhambi kuzuwiwa kwenda Kusoma kwnn wewe mwenyewe umeshindwa kuheshim hisia za kuamshwa kwa wema na kutaka nguvu zitumike kisha uchukie kujitambua shida.
 
Mimi naungana nafasi ya kuwajibika kabla ya kuwajibishwa yy anawajibika si jeuri lkn inaonekana wazi kuna vikwazo na mashaka mengi yanayomkosesha Raha kwa kufikiria kuinuwa Taifa la Tanzania kwanini tuiuungane nae tukawa na nguvu ya pamoja. Ijapokuwa kama Mtu mmoja ananguvu wingi wa watu huwa hauna maana tena maana itakuwa ni Mkusanyiko wa Arusi ya Nzi.

Hongera Magufuli,mimi si muumini wa Chama chochote Tanzania ijapokuwa ni Raia maana tokea nielewe kuhusu ubaya na dhambi za Uongozi na uchafu wa jamii zetu nimekuwa nakiepuka kila chenye ishara ya kunitia matatizoni maana unaweza kuwa na njia ya utatuzi lkn ukabezwa kwa mfano wapo wenye Elimu ajira hawana na wamezaliwa na Vipaji.
 
Kauli zake nyingi ni za ubinafsi...kauli kama serikali yangu,utawala wangu,sitatoa fedha kusomesha wazazi,mara anasema alichukua form mwenyewe hakusaidiwa na mtu....kuna umimi fulani kwenye kauli zake..kauli zinatokana na mawazo na mawazo ndio tabia ya mtu..mtu hawezi kuwa tofauti na mawazo yake..mawazo ya watu wa namna hii hupelekea tabia ya kutaka kunyenyekewa na kuabudiwa,hawataki kupingwa wala kumskiliza mtu mwingine,atajiaminisha hii nchi ni yake na hamna nwingine kama yeye..na hapo ndio itakuja mwanzo wa uraisi wa milele..
Kuna kila dalili za ungwazi wa muyaya kama tunamkumbuka Kamuzu Baada.
Lazima tupinge hilo kwa nguvu zote
 
Nimeangalia video clip iliyoambatishwa:
Binti akipata mimba marufuku kwenye shule ya sekondari za serikali - kwenye elimu bure
NGO na Private sector hazijazuiwa kuwasomesha mabinti waliopata mimba kwenye shule zao
Wanaowapa mimba adhabu ipo - miaka 30 jela, haijalishi ni mwalimu, mwanafunzi mwenzake nk.
Walio kwenye vyuo vya elimu ya juu ruksa kuzaa
Tusiige kila tunacholetewa toka nje maana wametuletea madawa ya kulevya, ushoga ( ambao hata ng'ombe hawafanyi)

Changamoto mbalimbali zipo za kuwapoteza watoto ambao wangeweza kwenda mbele na kufanikiwa zaidi lakini madhara yake kwa jamii (kama itaruhusiwa kuzaa na kurudi shuleni) yakoje?
Huyu mtoto anayezaliwa malezi yake yakoje - mama yuko shuleni, mtoto anabaki na nani?
Je baada ya kujifungua mzazi aruhusiwe kurudi shuleni baada ya muda gani?
Je aruhusiwe kuzaa mara ngapi na kurudi shule! mara moja, mbili, hata tatu?
Kama watasoma na watoto wao wanao karibu, tunahitaji miundo mbinu ya ziada ya kuhifadhi hivyo vichanga wakati mama zao wako darasani?
Je wasome kwenye darasa moja na wasio na watoto?
Kuwafukuza shule mabinti waliopata mimba inaonekana ni adhabu kubwa, lakini je nini kifanyike tukitilia maanani changamoto nilizotaja hapo juu!
 
watu wataogopana
vijana/wanaume watawaogopa wasichana especially wa shule na hao wasichana wa shule watawaogopa
maana wpte watakua alert kuwa nikichezea nakula miaka 30 , na msichana nae anajua ndio mwisho wa ndoto zake
 
mi huyu baba simuelewi make ni mzee wa kuanza kumalizia saa daaaaaaaah mzee wapi noah zetu jamaa hawajaleta mpunga au ndo changa la macho
 
Kuna kila dalili za ungwazi wa muyaya kama tunamkumbuka Kamuzu Baada.
Lazima tupinge hilo kwa nguvu zote

Hilo mkuu lisikupe shida. Hii agenda inaanza kushupaliwa mdogomdogo lakini madhara yake ni kuwa chama chake kinawekwa rehani. Mgfl kuendelea madarakani forever haina maana CCM kuendelea madarakani forever. Mwenye macho anaweza kuliona hilo. Kwa kifupi hii ni mikanganyiko ya ndani ya chama chao na hoja hizi zilianzia kwenye mkutano mkuu wa Dodoma. Walikataa kabisa kuwa walijadili hili lakini sasa muda tayari unasema. Watajikorogakoroga hadi wabaki uchi.
 
Back
Top Bottom