Rais Magufuli sikia kumekucha

mkuu wa kijiji

JF-Expert Member
Apr 7, 2017
966
1,053
Habari yenu,

Si kila jambo nitakaloambiwa naliamini wala si kuyapuuza kila kisemwacho.

Kwa sababu Kila aletae neno litakuwa na maana iwe njema au mbaya lakini litakuwa na maana.

Rais naamini kazungukwa na wataalam lukuki na wenye weledi kwenye mambo ya Kisiasa na kiuchumi.

Mambo hayako sawasawa kiuchumi mkuu hali ni mbaya ambayo watanzania hawajahi kukutana nayo miaka ya hivi karibuni.

Kwa hali ilivyo unapaswa Sasa ujitathimini Kwa maslahi ya Taifa letu.

RaisbKwa hali inavyoendelea watajitokeza watu wenye kutaka kiti kikuu si Kwa kujaribu kama 2015 bali kuchukua kiti.Naamini wewe mwenyewe utakuwa umekaribisha haya.

Rais Kwa Sasa uhusiano kati ya wananchi wa kawaida na serikali si wenye afya nzuri kabisa.

Hata sisi makada wako tuliokuwa na imani na wewe tuna mashaka makuu Kwa Sasa.

Suala la Korosho lipate majibu wasikudanganye,Kilimo chenye kubeba ajira ya watanzania asilimia 75%hakijapewa uzito.

Nina Mengi ya kusema lakini nimalizie Kwa kusema wewe ndie Raisi na mkuu wa Nchi ni vema ukawa na muda Kila mwisho wa mwezi ukaongea na Taifa kupitia vyombo vya habari na kutumia lugha nzuri na ya matumaini kwa wananchi wako.

Mwisho wewe unapaswa ujenge umoja wa Kitaifa Nchi imekuwa ya ukanda.

Nina imani hata mpambe wako atasoma itakufikia
 
Katika maisha yangu sikuwahi kuona umuhimu wa kupiga kura ila upepo wa 2015 ulinipitia nikampgia kura jiwe....kwa Sasa Naomba malaika watubadilishie wamrudishe mengi wamchukue jiwe
Najuta na nimetubu..... Wakati natoka kumpigia kura jiwe gari ilipinduka njiani niliuguza mguu mwezi..... Leo hii jiwe anatufanya tuishi kama mashetani...... Kwa kweli bora turudishiwe mengi
 
Back
Top Bottom