mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,774
- 12,084
“Wapo watu wamejaa wivu mioyoni mwao, wengine atasimama mbona hela hazipo, wale walizoea hela za rushwa, walizoea hela za utapeli, kwa sasa wanafikiri fedha hizo zitapatikana kama zamani, kwa sasa hela za utapeli za kudhulumu wananchi hazitapatikana , na nataka niwaambie na nitangaze kwa dhati kabisa, serikali yangu haigawi hela”, alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli aliendelea kwa kuwasisitiza wananchi kufanya kazi kihalali, na wale wataoendelea kufanya ufisadi watakiona cha mtemakuni.
“Usipofanya kazi hata hizo ulizonazo zitapotea, kwa hiyo mafisadi wakae wakijua hilo, zile fedha walizokuwa wamezoea kuzipata kwa kufisadi wananchi masikini hawatazipata tena, na wakifanya ufisadi kwa sasa hivi wajiandae kutumbuliwa na kwenda gerezani, wakaone shida ya kule, kwa sababu hatuwezi tukaruhusu Watanzania kuishi maisha ya shida, wakati wapo watu wengine walikuwa wanaishi kwa jasho la masikini”, alisema Rais Magufuli.
NOTE:
Ukipambana na ufisadi, utaagusa mfumo wa sheria, na ikibidi kubadili au kurekebisha katiba.
Sheria zitakapokuwa imara, na mifumo ya kitaasisi itakapokuwa imara, kisha vyombo husika vikapewa nguvu ya kushughurikia ufisadi, tunaweza kupunguza ufisadi au angalau kupunguza madhara yake.
Lakini ukipambana mafisadi, kwa sheria zinazompa mtu mmoja maamuzi ya mwisho, mtu huyo (rais) ataishia kuwadhibiti anaoona anawamudu na/au anaowachukia, na kuwaacha asiowamudu na/au anaowapenda.
Kwakuwa hatuna sheria, bali tuna mtu, kwa hiyo tuendelee kuchekelea fisadi huyu akishughurikiwa wakati fisadi yule aliyemtuma/aliyeshirikiana naye akiendelea kupeta.
Kuna tofauti kati ya kupambana na ufisadi na kupambana na mafisadi.
Sent using Jamii Forums mobile app