Rais Magufuli: Serikali kupitisha Fedha zote Benki ya NMB

Dumbuya

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
596
878
Salam wapendwa.

Leo nimeweza kupokea kipande cha video toka katika moja ya hotuba zake Mh.Rais akiwa kwenye ziara yake kikazi huko Mtwara.
Mh. amenukuliwa akimuagiza waziri kutoa maelekezo kwa wizara yake kuwa fedha zote za serikali zipitie benki ya Nmb kwani hiyo ndo yenye tija zaidi haswa kwa kuwa serikali ina hisa zake na huwa inapokea gawio pale faida inapopatikana (mwaka uliopita serikali imepokea bil.34).Hapa Mh anasisitiza kuwa kutakuwa na 'special treatment' kwa Nmb kwani inatoa dividend 'gawio' kwa serikali.

My take: Kandarasi na wanufaika wa fedha zote za serikali wakipeleka akaunti zao Nmb,benki nyingine 55 zitapata wapi biashara ?? Hasa ukizingatia kuwa serikali ndiyo main bussiness man na mtawanyiko uliokuwapo unatengeneza mazingira bora ya ushindani wa taasisi hizi za fedha..

Namba awamu hii inasomeka vizurii...Shikamoo JPM !

Link ya Video hiyo hii hapa, unaweza jionea.

 
Back
Top Bottom