Rais Magufuli serikali iwakopeshe wafanyabishara waanzishe viwanda ambavyo malighafi tunazo kwa wingi.

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Makampuni kama Sumsung, hyundai na LG yapo hapo kwasababu ya usaidizi mkubwa wa seriakali ya South Korea. Ilicheki Makampuni ya watu binafsi yanayofanya vizuro kisha ikayapa pesa sawa na bure ili kuyabust. Leo makampuni hayo hayakamatiki.

Nashauri serikali yako ingecheki wafanyabiashara wenye nia na mtaji kiasi na kuwaongezea ili wafungue viwanda. Hapa nazungumzia viwanda kama vya ngozi, kahawa, chai na korosho, kusindika nafaka nk. Serikali iseseme tu watu wasiexport nafaka isiyosindikwa bali wawawezeshe watu kusindika. Tuweke lengo kama Taifa kuwa ikifika mwaka fulani basi Tanzania isiwe unauza mazao yake nje bila kuyasindika.

Tena hii ishu iwe kama emergency hivi na si kupitia TIB ambayo mpaka sasa haijaonyesha matunda yaliyokusudiwa zaidi ya kukopesha wakubwa wasio na nia ya kuwekeza. Kama vipi tuanzishe mfuko wa kusaidia viwanda vya kuongezea mazao thamani.
 
Back
Top Bottom