Rais Magufuli ongeza siku za kukaa Arusha ili tuendelee kupata umeme

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,488
Najua kuna wafuatiliaji humu wanaoweza kumfikishia hii kero ya kukatika katika kwa umeme mkoa huu wa Arusha. Mara ya mwisho umeme kuwepo mfululizo ni kipindi cha uchaguzi baada ya pale umeme hauwezi ukapatikana zaidi ya saa 8 au 9 kwa siku tena usiku wa manane.

Leo ni siku ya tatu umeme haujakatika na ni tangu raisi Magufuli awepo hapa Arusha. Mheshimiwa raisi kabla hujaondoka Arusha naomba utumbue jipu hili la kukata umeme ovyo hapa Arusha maana najua ukishageuza mgongo wataendelea kukata. Kama taifa hili lina usawa endelea kukaa ikulu ya Arusha hata mwezi nasi tufurahie.
 
Magufuli tunaomba wakati ukirudi ikulu ndogo pitia pale tanesko katumbue jipu limeiva kabisa
 
Back
Top Bottom