Asante Rais Magufuli kupambana na mafisadi TANESCO, sasa umeme sio kero tena na haukatiki muda mrefu

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,910
51,904
Tanesco iligeuzwa chombo cha kisiasa ambacho mafisadi waliitumia Tanesco kuifanya serikali ya CCM ichukiwe na wananchi ili upinzani ushinde

2015 karibu na uchaguzi mkuu nilikuwa Arusha mjini umeme ulikuwa unazimwa siku nzima unawashwa saa saba usiku na kuzimwa saa tisa usiku. watu vyakula viliwaozea kila ukipita kila kona CCM ilikuwa ikiporomoshewa matusi ya nguoni kumbe mifisadi ikishirikiana na mifisadi mifanyakazi us Tanesco iliamua kutumia Tanesco kama chombo chao cha kuipiga chini CCM

Na hili lilifanyika sana mikoa ya kaskazini na majiji ya Mbeya, Dar, Arusha na Mwanza na sehemu mbalimbali za miji kama Iringa nk Hali iliyosababisha maeneo hayo kuchukuliwa na upinzani kirahisi tu kwa kutumia kero ya Tanesco tu

Baada ya Raisi Magufuli na kutumbua mafisadi Tanesco na kuibana mifisadi ya umeme sasa hivi hali shwari tuna enjoy umeme wananchi kero imeisha. nyumba hata za vijijini za majani zina umeme wa Rea na haukatiki hovyo

Mtu akibeza mafanikio ya Magufuli muulize tu vipi umeme ukilinganisha na kabla 2015 Magufuli kuingia madarakani hali unaionaje? Raisi Magufuli asante kutuondolea kero ya umeme kuanzia ugumu wa kuupata, kukatika vipindi virefu, nk

Ilikuwa 2015 kurudi Numa kabla Rais Magufuli hajashika urais wafanyakazi wa Tanesco wakionekana mtaani na magari yao watu walikuwa watu mtaani walikuwa wakiwazomea na kuwaombea dua mbaya na wengine kuwarushia mawe kuwa wamekuja mtaani kukata umeme!!!

Watanzania waliehuka umeme kuwaka ilikuwa sherehe kubwa ya kushangilia kuliko ushindi wa simba na yanga umeme uliokatika unaporudi!!! Yaani ukirudi watu wanashangilia kama wehu ngoma za madebe zinapigwa mitaani kwenye mabaa watu wanaruka ruka juu kama ngoma ya masai kufurahia umeme adimu uliorudi!!

Toka mheshimiwa Magufuli ashike madaraka sherehe Hizo zimekufa. Umeme raha mstarehe. Asante Raisi Magufuli kwa kutatua kero hii kubwa iliyokuwa inagusa watu wote wa juu hadi wa chini kabisa nchi nzima.Anayebisha mafanikio ya Raisi Magufuli aangalie kipengele cha umeme pekee nchi nzima na alinganishe na kabla hajaingia madarakani 2015
 
Kwenye suala zima la umeme na ujenzi wa baadhi ya miundombinu, NAMPONGEZA.

Ila kwenye sera ya ajira kwa vijana na hasa wahitimu wa vyuo, kwenye suala la maslahi ya wafanyakazi, uhuru wa habari, kuminya demokrasia, hulka yake ya kupenda kusifiwa kupita kiasi,

kuwacheleweshea wastaafu mafao yao, na pia kutaka kuwadhulumu hao hao wastaafu kupitia KIKOKOTOO, Kujimilikisha Bunge, Ubaguzi kwenye kesi za ufisadi na uhujumu uchumi, nk. HASTAHILI pongezi yangu kwa kweli.
 
Kwa kweli Mh. Raisi anahitaji sifa nyingi sana, kafanya makubwa hili kukomesha mgao na ujambazi ni miongoni mwa mengi aliyoyafanya. Siku hizi hata wakikata umeme mara nyingi hutoa taarifa before, labda iwe ni emergency, ila kuna baadahi ya maeneo kama Wilaya ya Ngara sijui wana tatizo gani mwezi huu karbu kila siku lazima umeme ukatike hasa nyakati za usiku kuanzia saa tano.
 
Tanesco wako fasta,hilo halina mjadala

ila usiwajaze sifa sana

ni kazi na ndio wajibu wao
 
Kwa hili la umeme ki ukweli sina ubishi...nakumbuka nyakati zile umeme unakosekana siku nzima unapita salon, kwa Wachomea mageti unakuta jamaa wamekaa wanapiga tu stori.
 
Sio kwamba anapambana na mafisadi bali anawaondoa mafisadi waliokuwepo mwanzo maana hana mgao hivyo ana create mafisadi wake ambao wanamuweka kwenye payroll so stuka kwahiyo atafanya mambo tofauti ili uone amefanya jambo kubwa kuondoa ufisadi lakini behind anatengeneza mafisadi wapya ambao ni chain yake!! Usiseme sijakwambia maana akili hizi tumefunuliwa wachache sana wenye maono ambayo wengine hawayaoni.
 
Mimi simkubali Magufuli kwa mambo mengi sana, lakini kwa hili la umeme kapatia. Lakini hawezi kupata kura yangu maana hafai kuwa rais, kwani ana mapungufu mengi.
Sasa nani atakuwa Rais? Maalimu Seif wa ACT?
 
Tanesco wako fasta,hilo halina mjadala

ila usiwajaze sifa sana

ni kazi na ndio wajibu wao
Kabla Magufuli Kuingia kwani haukuwa wajibu wao? Magufuli anawasimamia vizuri ndio maana wanawajibika sababu hacheki nao kwenye kazi Ni hapa kazi tu
 
Ni kweli mkuu japo sio mdau wake sana kwa hili la Umeme nampa Gwala aisee.Tulichezewa sana aisee.Siku hizi umeme kwa sisi wa matumizi ya kati sio shida tena.
 
Sio kwamba anapambana na mafisadi bali anawaondoa mafisadi waliokuwepo mwanzo maana hana mgao hivyo ana create mafisadi wake ambao wanamuweka kwenye payroll so stuka kwahiyo atafanya mambo tofauti ili uone amefanya jambo kubwa kuondoa ufisadi lakini behind anatengeneza mafisadi wapya ambao ni chain yake!! Usiseme sijakwambia maana akili hizi tumefunuliwa wachache sana wenye maono ambayo wengine hawayaoni.
Sawa haina shida kaondoa mafisadi ya umeme na haja replace mifisadi mingine ya umeme.!!!

Hoja yako haina mashiko angekuwa na mihasira ya kukosa mgao wa rushwa za mifisadi ya Tanesco angeiondoa mifisadi ya umeme iliyokuwepo aka replace mifisadi yake mipya ya kumpa rushwa na wananchi nchi nzima tungeendelea kuteswa na Tanesco!!! Lakini hamna Hilo!!! Kaipiga chini mifisadi ya Tanesco wananchi nchi nzima twapata raha hakuna fisadi mpya Tanesco wa kutuonea
 
Matusi ya rejareja haya..

Yani chama cha upinzani kitumie shirika la umma kuhujumu utendaji wa serikali iliyopo madarakani!? Na serikali ipo tu inaona hayo yote!?

Hahahah siasa za Bongo bhana.....
 
Matusi ya rejareja haya..

Yani chama cha upinzani kitumie shirika la umma kuhujumu utendaji wa serikali iliyopo madarakani!? Na serikali ipo tu inaona hayo yote!?

Hahahah siasa za Bongo bhana.....
Lowasa alikuwa na mtandao wa kuhujumu kikwete viongozi wengi serikalini aliwaweka yeye akiwa Waziri mkuu walipogeukana na Kikwete akamtoa uwaziri mkuu akamuweka Mizengo pinda akaanza hujuma kikwete aonekane dhaifu utendaji baadaye akajiunga chadema kisirisiri akijua hawaivi na Kikwete Hivyo akipigwa chini aende chadema!!! Alivyoenda chadema mtandao wote alioiweka serikalini na mashirika ya umma wakawa naye wakiwemo wa Tanesco kuhakikisha kila mtu kwenye nafasi yake anahujumu ili Serikali ya,CCM ionekane boya!! Tanesco Ni moja ya mashirika yaliyofanikisha chadema kupata wabunge!! Kwa kuzalisha kero nyingi za umeme kwa wapiga kura zilizofanya watu wachukie CCM Hadi Basi.Hicho ndicho kilifanya Hadi akina God bless lema wakashinda Arusha!!!

Ndio maana Raisi Magufuli aliposhika tu katika maeneo alianza kutumbua ni Tanesco
 
Back
Top Bottom