Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 71,232
- 127,306
Watanzania tuanze kujiuliza. Kwaanini Unaenda Shule wakati unajua Hakuna Ajira.
Nani aliyewaroga?.
Kuna vijana wanaona yaliowakuta Kaka na Dada zao waliosoma sana. Na wao wanafuata mkumbo huohuo. Kisa Prestige!!.
Elimu unasoma ikusaidie nini kama haitoi Ajira ?.
Unasoma ya nini kama haikuwezeshi kujiajiri?.
Na Kama haikupi descent life?
Tena unakopa Mkopo mrefu wa chuo kikuu unadaiwa na Riba, ukijumlisha na miaka ya kulipa. Unadaiwa Pesa ya kununua Rav 4 ya mtumba.
Graduate, Ukijitazama hata vocha unagongea kwa maparenti ambao hawajabukua kama wewe.
Kusoma sana ni Dalili ya Uoga wa Maisha.
Hakuna Kipya kule ni Muda unapoteza.
Na unarudi kitaa unakuja kuuza vocha kwenye maduka ya Tigo na Voda.
Au kulima kijijini kabisa.
Unakutana na vijana waliachia Form Two wengine La Saba. wanaenda China na Bondeni kwa Madiba kuchukua Mzigo hawajui kubonga kingereza kama chako lakini Mifuko yao imejaa Pesa.
Umebakia tu. You knowww, you knowww..
By ze way.. Niende moja kwa moja kwenye swali lako.
Mheshimiwa Raisi ameruhusu Vijana kupiga biashara popote.
Ametoa na Vitambulisho ili wasisumbuliwe popote. Tena vitambulisho ametoa yeye mwenyewe. Tunaanzaje kuuliza Ajira.
..Tupambane na hali zetu tuweze kujikwamua....
Sawa, kama kujiajiri ni rahisi hivyo. Rais asiibe kura ili kubaki madarakani na yeye aje ajiajiri ili tuende kuiga mafanikio yake, sio yeye ashauri watu kujiajiri wakati yeye mwenyewe anaiba kura ili abaki kwenye ajira.