Pearce
JF-Expert Member
- Dec 15, 2018
- 732
- 1,746
Kweli ana madhaifu mengi tu tutakubaliana wote kutokana na asili ya kisukuma
Wazee wakisukuma na wanyamwezi wanamsemo fulani "Mkubwa hakosei" na mazingira hayo pengine yana changizo fulani katika tabia zake...
Ukweli hatujasikia tena ujangili wa tembo kiasi mataifa ya ulaya yameacha kabisa kujadili hilo. Hivi mnakumbuka Maafisa wa China walituhumiwa kubeba pembe za ndovu katika ziara ya rais wa China Afrika. Kuna jirani yetu mmoja ambaye alikuwa tajiri sana alijenga nyumba yake usiku na mchana mafundi wanapokezana kiasi ikainuka ndani ya mwezi, tena ni nyumba ya chini chini lakini aliweekea msingi wa ghorofa hatukujua huyu mtu hela zote hamepatia wapi, mpaka magufuli alipoingia madarakani akawekwa ndani ndipo tukajua ni mzee wa pembe za ndovu.
Nchi za ulaya ziliituhumu Tanzania kama geti la kuingizia madawa ya kulevya ulaya na wakati huo tumepoteza ndugu wengi tu huko China wakisafirisha madawa ya kulevya hawajawahi kurudi tena Tanzania mpaka leo.
Huku mtaani kuliibuka kundi la vijana walioenda kujiripua na madawa na walikuwa wakirudi mtaani kusema kweli ilifika kipindi tuliona kusoma ni kama kupoteza muda sababu short cut hipo na tunawaona walivyokuwa na pesa nyingi hadi kununua magari hata manne kwa wakati mmoja.
Yapo mengi tu kwa kweli hatutasahau hata tembo wangekuwa na lugha ya kutamka wangekushukuru Mzee wetu
Ila mzee baba tumeona mengi tu mema yako na hatuwezi sahau tatizo ninaloliona umeunganisha maadui wa taifa (Majangili, Mafisadi, wauza madawa ya kulevya) na waliokupenda kwa juhudi zako awali (Wapenda haki katika jamii) kuwa kundi moja wanaokupinga kila leo
Sababu nilizoziona hasa
Haina siri maelfu ya vijana hawana ajira huwezi fahamu ili mpaka ushiriki ajira zinazotangazwa na ajira portal sababu nimeshiriki sana kule unakuta ajira nafasi moja inagombewa na watu si chini ya 200 hadi watu 400 (aina ya nafasi nilizoomba nikashiriki).
Na wapo vijana wengi wamekata tamaa kabisa ukiacha ya kijana Musa wa Rock city mall alieamua kujiua Siku hizi imekuwa kawaida kuwakuta graduates wakiendesha boda boda wakiuza mitumba hadi makondakta na wauza nyanya (sisemi sababu nadharau hizi kazi hapana). basi nini maana ya kupoteza miaka yote katika elimu sababu nafasi za kazi hizi haziitaji tu hata kufika kidato cha 4 5 au 6.
Kauli zako Mzee baba wakati mwingine zinaumiza sana tupo watanzania wengi sana na wengine vyama vyetu ni justice na right tunaumia tunapoona lipo kundi la watu fulani wanaumizwa tu sababu ya itikadi zao na vyama vyao hii haipo sawa.
Mzee wetu Rais wetu na baba wa taifa hili katika kipindi hiki si haki kwa mwenendo wa hali ya taifa letu kutuunganisha kundi moja na maadui wa taifa hili(wauza madawa ya kulevya, LGBT, majangili, mafisadi na wahujumu uchumi) na vijana wasomi ambao wapo kitaa hawana kazi.
Sababu kundi Ovu litachukulia fursa ya ukosefu wa ajira kama kigezo cha kuwaaminisha vijana tusahau mema yako uliyoyatenda tayari kwa taifa.