Rais Magufuli ni Dikteta?

dkn

Senior Member
Oct 7, 2010
139
42
Watanzania tumekuwa na maneno mengi sana kuhusu Awamu ya Tano na mbaya zaidi kuwa Raisi wetu John Pombe Magufuli ni Dikteta na maneno mengi ya kejeli. Ukweli unabaki pale pale JPM ni mzalendo kweli hata kama ana mapungufu yake kama binadamu ila amefanya mengi ambayo yanahitaji nguvu za ziada na kujitoa kwa lolote.

Haya yanayotokea sasa hivi ndani ya CCM yamekuja muda muafaka sana kuwatoa mamluki ndani ya chama. Hata ingekuwa ni chama pinzani kimeshika hatamu, pamoja na maendeleo mazuri haikuwa muda muafaka viongozi wastaafu kupeleka waraka wao kwenye public kwani kuna ngazi za kufuata ndani ya chama.

Tunaona madhara ya watoto wa viongozi walivyoanza kupewa madaraka, walishazoea kuishi maisha ya anasa na kupata upendeleo kila maeneo husika. Tuangalie watoto wa Baba wa Taifa wanaishi vipi, ingawa wengine wamepewa nyadhifa au kugombea ila ni tofauti sana na viongozi vijana wa sasa hivi wanaotoka katika familia zenye au zilizokuwa na viongozi wa Serikali na CCM.

Surveillance inayofanywa ya mawasiliano ya viongozi wa serikali siyo kitu kigeni katika nchi yoyote, hata kama siyo viongozi katika usalama wa nchi inaruhusiwa, maneno mengi kuwa privacy ya mtu imekiukwa hamna kitu kama hicho. Watambue wao ni viongozi wa Kiserikali na jamii kwa ujumla na wanatakiwa kufuata sheria za serikali na chama, iwapo itaonekana kuna dalili za kuleta misiguano au vurugu ndani ya chama au nchi, lazima serikali itumie mbinu zozote kuhakikisha maslahi mapana ya nchi na serikali yanafanikiwa.

Viongozi wengi wa juu wastaafu wa Serikali ndiyo mafisadi wakubwa katika nchi yetu, JPM aliwaambia watulie kama wastaafu na wamuache afanye kazi yake. Sasa hivi wanaanza kuleta chochoko zisizo na maana, angalau wamesema mambo yanayohusu nchi yao ila ni ubinafsi, mara hatujapewa majina ya barabara, mitaa mjue kwamba mliisaidia CCM kama chama ni siyo nchi. Mambo mliyofanya kwa manufaa ya nchi hii ni madogo sana kulinganisha na ufisadi, wizi wa mali za serikali, kujilimbikizia mali bila kuwa na ushahidi mali mlipataje.

Mwisho, JPM anaona mambo yanavyoenda kwa wabunge wa CCM, kumekuwa na unafiki wa kubeza vyama pinzani hata kwa mambo ambayo yako sahihi, ila JPM amelenga zaidi kufuta kero za wananchi ambazo upinzani umekuwa ukiongea kwenye kampeni zake ambayo sisi wananchi tunafurahia. Upinzani ni muhimu sana katika maendeleo ya nchi, na wanaosema JPM anaua upinzani mara Dikteta si kweli anatimiza yale ambayo walikuwa wakisema CCM na Serikali yake inaboronga na hawana la kusema, ila wanapotaka kuleta uvunjifu wa Amani lazima serikali ichukue tahadhari kubwa.

Wabunge wa CCM bungeni lazima wasimamie maslahi ya wananchi na wakubali yale mema ya upinzani, tumeona wabunge wachache wa CCM wakikosoa Serikali bungeni kama Mheshimiwa Bashe katika positive way, unakosoa na kutoa maoni ya jinsi ya kutatua au kufanikisha jambo fulani na siyo kukosoa bila kutoa mbadala wa kutatua tatizo. Ni wabunge wachache sana wa CCM wanaweza kutoa hoja zikiwa supported na takwimu, na vielezo au wapi njia zipi zilitumika katika nchi yetu au nchi jirani kwa kufanya research kama Mheshimiwa Bashe, wengi wao wamekalia kupiga makofi na kukosoa upinzani. Hakuna haja ya maneno ya kwenye khanga bungeni kutoka kwa wabunge wa CCM, karibia kila jimbo maendeleo yanaonekana ni nyie kuwaambiwa wapinzani tumefanya hiki na tunaendelea kama kuna mawazo chanya ya upinzani basi yanachukuliwa na yanafanyiwa kazi.
 
Hapana
Yule mzee ni mzalendo.
Ni mtukufu
Ni mpenda watu
Ni close minded person
Anajua mambo mengi
Atalipeleka taifa letu mahali fulani.

Tujiandae kwa lolote.
 
Back
Top Bottom