Rais Magufuli ndani ya Igunga, mwenyekiti wa CHADEMA aomba amsalimie

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,982
Katika mwendelezo wa ziara yake ya siku nne katika Mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita, Rais Magufuli amefanya mkutano Igunga.

Katika kuonyesha jinsi ambavyo wananchi wengi wanakubaliana na mtazamo na mwelekeo wake katika hatma ya Taifa, Mwenyekiti wa CHADEMA amewaomba sana walinzi wa Rais ili asalimie Rais kwa sababu anachokifanya Rais kinamgusa katika hali chanya kimaisha na kitaifa.

Rais baada ya kuona tukio hilo aliwaomba walinzi wake kama kuna uwezekano wamruhusu.

Rais Magufuli amezungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika vijiji vya Nanga na Ziba na amefanya mikutano ya hadhara Igunga na Nzega ambako amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake itahakikisha inatekeleza ahadi zilizopo katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2015.

Katika mkutano wa hadhara uliofanyika Igunga, Rais Magufuli amepokea malalamiko ya wananchi kuhusu kutoanza kutumika kwa kituo cha mabasi na soko na amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Tabora kuhakikisha kituo cha mabasi cha Igunga na soko la Igunga vinaanza kutumika kuanzia Jumatatu ijayo ya tarehe 01 Agosti, 2016.

Kuhusu kero ya maji, Dkt. Magufuli amesema Tanzania imepata mkopo wa dola za kimarekani Milioni 268.35 kutoka nchini India ambazo zitatumika kutekeleza mradi wa kusambaza maji ya ziwa Viktoria katika Miji ya Tabora, Igunga, Nzega, Sikonge

VIDEO:

58.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nanga Wilaya ya Igunga Ndugu Masesa Kishiwa Makala kutoka Chadema wakati akiwa safarini kuelekea Nzega Mkoani Tabora.
75.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Ziba Wilayani Igunga mkoani Tabora.
1cnbcbn.jpg

29.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia ya wakazi wa Igunga mkoani Tabora katika ziara yake ya kikazi katika Mkoa huo wa Tabora
106.jpg

Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wananchi.
410.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Igunga mkoani Tabora mara baada ya kuwahutubia Wilayani hapo.
 
Uchaguzi umeisha, kumsalimia hakubadilishi matokeo. Walikuwa wanafanya utani wa jadi kwamba yeye aliwagalagaza ccm kijijini.
 
Walivyowapanga Wenyeviti taifa wa TLP.na UDP akina Mrema na Cheyo akapuuzwa sasa anatafuta Kiki kwa Mwenyekiti wa Kijiji wa CHADEMA?

Tukisema Rais Magufuli ana stress kisiasa tutakua tumekosea?

Yaani anatafuta kiki kwa nguvu kiasi hiki kwa mwenyekiti wa Kijiji wa CHADEMA? Je kama angekua Diwani wa CHADEMA je?
 
Unaweza kupitia kwenye hii thread na kusoma alichokisema Mbowe ili tujuue nani alikuwa anatafuta kiki.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbowe ampongeza Rais Magufuli kwa juhudi zake anazozifanya

Mwenyekiti wa CHADEMA alisema hivi;
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amesema wanampongeza Rais Magufuli, kwa harakati zake za kutekeleza ilani ya Chadema na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya Wananchi UKAWA.

Amesema madudu ya ufisadi na uozo unaotumbuliwa hivi sasa baada ya kufanywa na baadhi ya watendaji serikalini ni matokeo ya sauti walizozipaza wapinzani, wakati CCM walikuwa wanaona ni kelele.

chanzo.East Africa Television (EATV)
 
Walivyowapanga Wenyeviti taifa wa TLP.na UDP akina Mrema na Cheyo akapuuzwa sasa anatafuta Kiki kwa Mwenyekiti wa Kijiji wa CHADEMA?

Tukisema Rais Magufuli ana stress kisiasa tutakua tumekosea?

Yaani anatafuta kiki kwa nguvu kiasi hiki kwa mwenyekiti wa Kijiji wa CHADEMA? Je kama angekua Diwani wa CHADEMA je?
tuambie basi na msigwa naye alikuwa anatafuta kiki ndugu...........
 
Tunaposema CHADEMA ni Mpango wa Mungu na ni Gumzo kubwa ugambani walio na mikia na wasio na Mikia wanakuja kutoa Povu
Ona uzi Mzima ni Namna Mwenyekiti wa CCM taifa kuushika Mkono wa Mwenyekiti wa CHADEMA wa kijiji tu.

I cant imagine siku akishika Mkono wa Mbowe
 
Walivyowapanga Wenyeviti taifa wa TLP.na UDP akina Mrema na Cheyo akapuuzwa sasa anatafuta Kiki kwa Mwenyekiti wa Kijiji wa CHADEMA?

Tukisema Rais Magufuli ana stress kisiasa tutakua tumekosea?

Yaani anatafuta kiki kwa nguvu kiasi hiki kwa mwenyekiti wa Kijiji wa CHADEMA? Je kama angekua Diwani wa CHADEMA je?
Kuna kiongoz yuko karibu na wananchi zaidi ya mwenyekiti wa kijiji?
 
Walivyowapanga Wenyeviti taifa wa TLP.na UDP akina Mrema na Cheyo akapuuzwa sasa anatafuta Kiki kwa Mwenyekiti wa Kijiji wa CHADEMA?

Tukisema Rais Magufuli ana stress kisiasa tutakua tumekosea?

Yaani anatafuta kiki kwa nguvu kiasi hiki kwa mwenyekiti wa Kijiji wa CHADEMA? Je kama angekua Diwani wa CHADEMA je?
Kwa Magufuli kila goti litapigwa.

Kama Mzee Mtei amesalimu amri na kusema Magufuli ni kama Nyerere. Nani wa kupinga??

Washika UKUTA wengine wa ufipa ni bora wakabaki kupangusa viatu Vya Mzee Lowasa tu
 
Jamaa nampenda sana nafurahi namuona Hayati Sokoine ktk ubora wake.
Hebu twambie kinachokufanya umlinganishe na sokoine ni kipi,hadi sasa kaifanyia nini nchi hii wakati hata mwaka haujatimiza,bora tungeendelea kutawaliwa na mjerumani hata miaka 50 watu kama hawa wangeelimika
 
Back
Top Bottom