Rais Magufuli: Naomba mradi huu ukamilike kabla sijatoka madarakani maana atakayeingia anaweza akaufuta

Rais Magufuli ameeleza kuwa alifanya juhudi za makusudi kwa kumtumia Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Patrick Mfugale, kukamilisha mchoro wa daraja la juu kwenye ziwa Victoria eneo la Kigongo Busisi lenye urefu KM 3.2.

View attachment 1284588

Akiongea katika hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi leo Desemba 7, 2019, Rais Magufuli amesema, mradi huo ni muhimu na anamshukuru Mfugale kwa kukamilisha mpango mapema pamoja na Bunge kwa kupitisha bajeti ya ujenzi huo.

‘Nimeona nimtumie Mfugale haraka haraka, nikamwambia kamilisha mapema katika kipindi changu cha Urais inawezekana muda wangu ukiisha anaweza akaja Rais mwingine akaufuta huu mradi, na huyu Mfugale amekuwa akifanya vizuri katika miradi yote ya madaraja nchini’, ameeleza.

Aidha Rais Magufuli amewaasa wananchi wa Mwanza hususani wa Wilaya za Sengerema na Misungwi ambapo mradi huo upo kuutumia vizuri kwa kunufaika kiuchumi kwani ni mradi muhimu kwa watanzania wote na nchi jirani.

Awali Mfugale alieleza kuwa mradi huo unagharimu Shilingi Bil. 699, ambazo zote ni fedha za ndani na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 40.

Wana Mwanza na Geita mpewe nini yawezekana mmeteseka kwa siku nyingi lakini sasa neema hiyo imefika
 
Mfugale hata kama ukisifiea kiasi gani kama kwenu hujashawishi uweke kumbukumbu yako ni bure kabisa

Mfugale ni mtanzania hii mitazamo ya "kwao au kwenu au kwetu" ndiyo inatugawa, mtanzania wa kabila lolote anaweza kwenda Mwanza akilitumia hilo daraja na hata mtu wa Mwanza anaweza kwenda Iringa hadi Mbinga au Kyela kwa barabara za lami, daraja la Kigongo lisiwatie watu wivu ni daraja linalojengwa Tanzania kwaajili ya watanzania.
 
Rais Magufuli ameeleza kuwa alifanya juhudi za makusudi kwa kumtumia Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Patrick Mfugale, kukamilisha mchoro wa daraja la juu kwenye ziwa Victoria eneo la Kigongo Busisi lenye urefu KM 3.2.

View attachment 1284588

Akiongea katika hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi leo Desemba 7, 2019, Rais Magufuli amesema, mradi huo ni muhimu na anamshukuru Mfugale kwa kukamilisha mpango mapema pamoja na Bunge kwa kupitisha bajeti ya ujenzi huo.

‘Nimeona nimtumie Mfugale haraka haraka, nikamwambia kamilisha mapema katika kipindi changu cha Urais inawezekana muda wangu ukiisha anaweza akaja Rais mwingine akaufuta huu mradi, na huyu Mfugale amekuwa akifanya vizuri katika miradi yote ya madaraja nchini’, ameeleza.

Aidha Rais Magufuli amewaasa wananchi wa Mwanza hususani wa Wilaya za Sengerema na Misungwi ambapo mradi huo upo kuutumia vizuri kwa kunufaika kiuchumi kwani ni mradi muhimu kwa watanzania wote na nchi jirani.

Awali Mfugale alieleza kuwa mradi huo unagharimu Shilingi Bil. 699, ambazo zote ni fedha za ndani na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 40.
KUKAMILIKA.

Miezi 40, uchaguzi bado miezi 12, anauhakika wa kushinda,

UCHAGUZI WA NINI?,

UCHAGUZI UWE BAADA YA DARAJA KUKAMILIKA.
 
Mfugale ni mtanzania hii mitazamo ya "kwao au kwenu au kwetu" ndiyo inatugawa, mtanzania wa kabila lolote anaweza kwenda Mwanza akilitumia hilo daraja na hata mtu wa Mwanza anaweza kwenda Iringa hadi Mbinga au Kyela kwa barabara za lami, daraja la Kigongo lisiwatie watu wivu ni daraja linalojengwa Tanzania kwaajili ya watanzania.
Iwe mwisho kuwa na rais Msukuma.
 
Kwa mantiki hiyo bado ana mpango wa kugombea ili miradi alihoanzisha ikamilike yote
Mkuu we umefuta mingapi?? Afu miezi 40 kuanzia sasa si itakuwa Uchaguzi tayari au kuna uhakika wa kushinda 2020??
 
Mfugale ni mtanzania hii mitazamo ya "kwao au kwenu au kwetu" ndiyo inatugawa, mtanzania wa kabila lolote anaweza kwenda Mwanza akilitumia hilo daraja na hata mtu wa Mwanza anaweza kwenda Iringa hadi Mbinga au Kyela kwa barabara za lami, daraja la Kigongo lisiwatie watu wivu ni daraja linalojengwa Tanzania kwaajili ya watanzania.

Kwani mzungu hawezi kutumia hiyo miundombinu? Kumbuka matumizi ya hiyo miundombinu ni hela yako na sio utanzania wako.
 
Kama yeye alivyoufuta mradi wa bandari ya bagamoyo
Kwani huo mradi ulikuwepo?
Bunge lilikuwa lishapitisha bajeti ya huo mradi?
Jk aliacha Ameweka Saini?

Nani aliweka jiwe la Msingi la huo Mradi?

Daah Watanzania Tutaendelea kuwa wajinga Hadi lini ukute na wewe ulitumia pesa za ukoo kusomeshwa.
 
Back
Top Bottom