Rais Magufuli, Nani amempa kibali mkurugenzi huyu wa Nokia - Vodacom? Nani yupo nyuma yake?

Mhandisi Mzalendo

JF-Expert Member
Aug 23, 2010
6,562
11,083
Mheshimiwa Rais, pole na majukumu ya ujenzi wa Taifa letu na kazi kubwa, ngumu na nzuri ambayo umekuwa ukiifanya hasa hii ya utumbuzi wa majipu ambayo kwakweli unaifanya kwa ustadi mkubwa na sisi kama wananchi wako tunajivunia sana kuwa katika nchi ambayo serikali yake inakemea maovu na kutetea maslahi ya wananchi wake. Mwenyezi Mungu akupe afya njema na aendelee kukujalia Hekima na busara katika majukumu yako nasi tufaidi rasilimali za nchi yetu nzuri aliyotujalia Mwenyezi Mungu.

Mheshimiwa Rais, tunaomba tukusaidie kukuonesha jipu moja ambalo limekuwa likitusumbua sana wananchi wako sisi tunaofanya kazi katika kampuni ya NOKIA inayoshughulika na uendeshaji wa mitambo ya kampuni ya VODACOM TANZANIA LTD.

Mheshimiwa Rais, kuna Operations Director wa kampuni ya NOKIA anaitwa JAN , huyu bwana kibali chake cha kuishi nchini kilishaisha tangu mwisho wa mwezi wa Tatu(3) Mwaka huu 2016. Na kwa taarifa za kuaminika huyu mtu alishakataliwa kuhuisha kibali chake cha kuendelea kuishi nchini na hata alipokata rufaa ili aongezewe miezi mitatu(3) watoto wake wamalizie shule ifikapo June 2016 alikataliwa. Kwa maana alijua kibali kinaisha na hakupaswa kuandikisha watoto shule kwa kipindi kinachozidi ruhusa yake ya kuendelea kuwepo hapa nchini.

Mheshimiwa Rais, baada ya kukataliwa, aliamua kuondoka nchini na hata alishaaga na kuagwa na kampuni ya NOKIA kwa kula keki na usiku hafla ndongo na wafanyakazi wote tarehe 31.3.2016 na sisi sote tulishaambiwa tutoe anuani yake ya barua pepe katika kumbukumbu zetu na tusimnakili katika barua pepe zote zinazohusiana na shughuli za kiutendaji za NOKIA. Lakini kama waswahili wasemavyo ukishangaa ya Musa utayaona ya Firauni, hazijapita wiki mbili mtu huyu yupo nchini na amerejea ofisini (NOKIA) na sisi hatujui wala hatujafahamishwa amerejea kama nani? Hatujaambiwa amerudi kuendelea na nafasi yake ama vipi? Na kinachotukera tangu amerudi amekuwa ni mtu wa kutusumbua, kutunyanyasa na kuhakikisha haki za wafanyakazi wazawa zinabanwa ikiwa ni pamoja na kutupokonya baadhi yetu vitendea kazi mfano magari tuliyokuwa tunayatumia katika shughuli za kampuni.

Mheshimiwa Rais, katika uchunguzi wetu tumebaini kuwa kuna kampuni inayoshirikiana naye kwa karibu sana na ndiyo anayoitumia kuwarubuni wafanyakazi wasio waadilifu wa idara mbalimbali za serikali ikiwemo Uhamiaji walio Wizara ya mambo ya ndani na ile Wizara inayoshughulikia mambo ya Ajira. Kampuni inayojishulisha kushirikiana na Operations Director Jan huyu kufanikisha vibali halali kwa njia zisizo halali inaitwa MAUVE CORPERATE SYSTEMS. Na katika kampuni hii ya MAVE CORPERATE SYSTEMS tunaomba mtu anayetumia namba 0657 227 1** Iliyosajiliwa kwa jina la Joc achunguzwe maana ndiyo mtu anayemsaidia huyu bwana kuwasiliana na watu wa Uhamiaji na Wizarani na ndiye mtu ambaye anahongwa na kupewa hongo za kuwapelekea wafanyakazi hao wa idara za serikali wasio waaminifu. Lakini pia katika uchunguzi huo asikosekane mtu mwenye namba 0754 811 *** iliyosajiliwa kwa jina la SARA huyu ana wadhifa mkubwa katika kampuni hii ya MAVE CORPORATE SYSTEMS na ambaye pia anahusika katika harakati hizi za raia huyu wa POLAND ambaye amekuwa kama Mungu mtu hapa ofisini kwetu.

Mheshimiwa Rais,tunaamini kupitia hii kampuni mambo mengi yatabainikia maana inasadikika hawa ndo watu wanaotumika na maafisa wa uhamiaji kusaka wateja wa kuwapa vibali kwa njia ya panya huku wao wakijipatia ulaji. Na kwa wakati huu haitakuwa vibaya pia kupata uhalali wa Operations Director huyu kuendelea kuwepo nchini maana inasemekana amepata kibali cha miezi mitatu na huku tayari ameanza mchakato wa kusaka kibali cha miaka miwili (2) kupitia kampuni hiyo ya MAVE CORPARATE SYSTEMS na maafisa wa uhamiaji.

Mheshimiwa Raisi, huyu mtu tulishamshtaki wizarani na vielelezo vyote vipo kule na tulishaahidiwa kuwa atashughulikiwa kwa namna ambavyo amekuwa akitunyanyasa na kutubagua sisi wazawa kwa kutunyima haki zetu pamoja na kuwalipa wageni mishahara mikubwa na kuwapangishia mahotel ilihali sisi wazawa tukifanya kazi katika mazingira magumu tena tukiwa tunafanya kazi zilezile wanazofanya wageni na zingine sisi tukiwa ndo tunawaelekeza. Hadi sasa hatuna mikataba ya kazi baada ya kukataa kusaini mikataba ya kinyonyaji na kupeleka suala letu kwenye wizara inayohusika na mambo ya ajira. Mikataba ilishaisha tangu Februari 29, 2016. Huyu mtu ndiye kikwazo kikubwa katika madai yetu. Na ameshaapa kuwa yupo tayari wote tuache kazi ila si yeye kutulipa madai ambayo hata wizara iliona ni ya msingi na ambayo yanalindwa na sheria inayosimamia mambo ya ajira.

Mheshimiwa Rais, mikataba tuliyoikataa haina stahiki nyingi ikiwemo hata malipo ya kazi ya masaa ya ziada maana kazi yetu mara nyingine ni ya masaa 24 na haina mapumziko ya mwisho wa wiki wala sikukuu. Haya yote wizara inayajua na hata sasa tunapoandika wizara ilishaamuru walipe malipo ya ziada yaani Overtime Allowance kulingana na sheria za kazi zinavyosema lakini huyu bwana pamoja na NOKIA wamekataa kufanya hivyo wala kutoa mikataba inayoeleweka.
Lakini pia tunaomba NOKIA kwa upande wa VODACOM wachunguzwe maana tunaamini wawekezaji wote wanapaswa kufuata sheria za nchi katika uendeshaji wa shughuli zao hapa nchini ikiwemo namna wanavyoshughulikia wafanyakazi. Hatuamini kuwa katika awamu hii, wawekezaji ambao wanajidai wapo juu ya sheria bado wana nafasi ya kuendelea kukanyaga haki za wazawa na kunufaika wao wenyewe huku wakiwaacha watanzania na umasikini wao.

Mheshimiwa Rais, tunaamini ujumbe huu utaupata wewe mwenyewe ama hata wasaidizi wako na tunaomba suala hili liangaliwe kwa namna ya kipekee maana raia wako tunaendelea kupata shida kinyume na kiu yako ya kila siku ya kuona sheria za nchi zinafuatwa na Raia wako wanafanya kazi na kuletea manuafaa kwa taifa letu na kila mtu kuonja matunda mazuri ya awamu hii ya HAPA KAZI TU.

Mheshimiwa Rais,
tangu mtu huyu amerudi kinyemela na katika mazingira ya kutatanisha tumekosa hata imani na wizara iliyokuwa inashughulikia mambo yetu na ndiyo maana tumeamua kukuandikia wewe mwenyewe ili haki itendeke na wazawa wafanye kazi kwa kutimiza dhamira chanya ya serikali yenye uaminifu na inaysimamia haki uchukue nafasi yake. Ni matumaini yetu kuwa hili litakufikia.

Asante kwa kutusikilizana tunaamini majipu haya ya idara muhimu ya uhamiaji sasa yatashughulikiwa kikamilifu kwa ufundi na ustadi wa hali ya juu.
 
Namuomba waziri husika apate kusoma hapa na kuanza kazi upya! Apite kwenye makampuni yote makubwa kuangalia vibali na pia zile nafasi za wazalendo ambazo hawa wageni wanazikalia kuacha wazawa wakinyanyaswa wakati kazi zoote zinafanywa na wazawa kw weledi mkubwa sana! Wapite Tigo kuna mambo kama hayo mengi tu; wapite Vodacom pia yapo....waende Airtel pia wamejazana pale wahindi na wazungu ambao hawastahili kabisa kuwepo pale, wanahonga uhamiaji na kuendelea kukaa nchini na wana biashara za siri nasikia hasa kwenye mbuga zetu huko! Waende makampuni ya TBL,SBL.....ule waraka wa wizara ya kazi waufuatilie kuona wazawa sasa wanapewa haki yao! Imetosha sasa!
 
Hii ni aibu kwa taifa letu wenyewe kunyanyaswa watakavyo,badae watucheke. I hope serikali itaifanyia kazi hili, hao wachache wala hongo watawajibishwa
 
Mavunde umelala usingizi wa pono nilitegemea wewe kama kijana ungesaidia vijana wanaonyanyasika kwenye haya makampuni ya simu.
 
Magufuli kazi anayo.ila naamini atalishughulikia hili la hongo idara ya uhamiaji.
 
Namuomba waziri husika apate kusoma hapa na kuanza kazi upya! Apite kwenye makampuni yote makubwa kuangalia vibali na pia zile nafasi za wazalendo ambazo hawa wageni wanazikalia kuacha wazawa wakinyanyaswa wakati kazi zoote zinafanywa na wazawa kw weledi mkubwa sana! Wapite Tigo kuna mambo kama hayo mengi tu; wapite Vodacom pia yapo....waende Airtel pia wamejazana pale wahindi na wazungu ambao hawastahili kabisa kuwepo pale, wanahonga uhamiaji na kuendelea kukaa nchini na wana biashara za siri nasikia hasa kwenye mbuga zetu huko! Waende makampuni ya TBL,SBL.....ule waraka wa wizara ya kazi waufuatilie kuona wazawa sasa wanapewa haki yao! Imetosha sasa!

Hahahahahah mkuu hakuna kitu kinachoendelea mawaziri hawajui wanajua kila kitu kuhusu awa wageni wanaoishi kiujanjaujanja.

Mawaziri bado wanaishi kwa mazoea wengi tu ilimradi Magu kitu ajakitolea macho wao wanalala tu.
 
Mavunde umelala usingizi wa pono nilitegemea wewe kama kijana ungesaidia vijana wanaonyanyasika kwenye haya makampuni ya simu.
Mavunde hamna kitu pale mzigo tu ule. Yupo insta kule anarusha picha za kuzindua makongamano yani watu wanamwandikia taarifa kibao yupo kimya tu.
 
Isije ikawa ndiyo kampuni za uwekezaji na wawekezaji mikwara tulio letewa na TIC enzi za mkurugenzi mchapakazi Julie
 
Mwenye email za wahusika mawaziri ampe jamaa amtumie....niliwah pata kesi km hii ...nikatumiwa na email ya waziri wa ajira enzi hizo...nikamtumia kilio changu...bahat nzuri akajibu.....akamtuma mtu wa ajira mkoani nilipokuwa ...yule jamaa wakaja watatu wakafika wakazungukia maeneo ya kazi na kupendekeza maboresho ya miundo mbinu...lastly wakaenda kuagwa ofisin...kila mtu alipewa million moja.....kuku majogoo 5 kila mmoja ...kesi ikaishia hapo..kwa hiyo niliwasaidia kuongeza kipato siku ile.....acheni vitu vingine vinatia hasira za kwenye ubongo na misuli
 
Duh...Tanzania ina mambo...poleee mkuu
 
Back
Top Bottom