nzalendo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 11,726
- 12,003
Kadiri siku zinavyokwenda pamoja na kuunga mkono baadhi ya hatua anazochukua Ndugu Rais Magufuli kwa lengo la kujenga taifa mpya.
Nasikitika kumtabiria anguko kubwa ambalo hatutakaa tulisahau. Kwanza ieleweke vema kwamba naunga mkono jitihada zake ila kwa mtazamo wangu, Ndugu Magufuli hana haiba ya Uongozi wenye kuwatwisha wananchi jukumu la maendeleo yao.
Rais kwa mtazamo wangu, anahisi kwa kuwa yeye ni AmiriJeshi basi kila mtu yuko chini yake. Kikatiba inawezekana ila katika ulimwengu wa leo cheo cha Rais hakina thamani endapo kitashindwa kushawishi Wafuasi wakabeba maono yake kama kiongozi.
Watu watalazimika kufanya kazi kwa maigizo japo ndani yao hawamuungi mkono Rais kwasababu ameamua kutumia madaraka visivyo (Kutishia) badala ya kutumia madaraka Kushawishi.
Nyerere alikuwa dikteta ila watu walimuunga mkono kwakuwa aliamini katika ushirikiano na nguvu ya wananchi katika kuleta maendeleo. Ninaungana na Rais kwamba lazima awepo mtu wakuongoza katika vita ila sidhani kama hivi ni vita vya mtu mmoja, naamini ni vya wananchi wote.
Baada ya miaka kadhaa ijayo, nchi ingekuwa ya Matunda na Asali endapo;
1. Rais angekuwa jasiri na kurejesha Katiba ya Warioba bungeni na kwa kutumia ushawishi wake ahakikishe inapitishwa.
2. Rais angejikita katika kujenga taasisi huru na zenye nguvu ili tusimtegemee mtu binafsi katika vita hivi maana atapomaliza muda wake vipi akiingia wale jamaa wa dili wataendeleza dili au uadilifu?
3. Rais angetambua nguvu iliopo ndani ya wananchi, angetumia muda mwingi kuwafanya wananchi waone thamani, wajibu na madhara ya kila kitu wanachofanya (Sense of Responsibility) katika kila ngazi.
Ninatamani kuendelea ila naomba niishie hapa kwa sasa.