Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,780
- 10,710
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana thread mbalimbali zinazoanzishwa hapa jamvini, hasa baada ya rais kuchukua hatua fulani. Wengi wetu, inawezekana kutokana na mfumo tuliolelewa nao hatuoni nia njema ya hatua hizo. Tumegeuka madebe shinda, kutwa kucha kutika!
Leo nitagusia hatua moja tu ambayo inamtofautisha mh rais na watangulizi wake, isipokuwa mwl Nyerere. Akiwa Shinyanga rais amesisitiza kuwa hakuna chakula cha msaada!! Wengi humu macho yamewatoka pima! Wachina wana msemo usemao mtoto wa jirani mpe samaki, mtoto wako mpe ndoana! Watanzania tumekuwa wavivu sana katika kila jambo. Sasa mh rais anafanya hayo ili turudi kwenye msitari. Wakati hata njaa bado haijafika, tayari watu wameanza mipango ya kupata msaada. Maana yake ni kuwa hatufikiri nje ya misaada na hatufanyi kazi tena tukisubiri njaa ilitupate misaada.
Hili la rais linaonekana baya sana leo, lakini baada ya miaka michache litakuwa na manufaa makubwa sana kwani kila kaya itajenga utamaduni wa kujiwekea akiba ya chakula. Na hii itasababisha maisha yenye mpangilio (long term plan).
Watanzania tuachane na utamaduni wa kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa. Kauli za kupumbazana za wanasiasa kwa manufaa yao binafsi ndizo zilizotufikisha hapa. Mtu anaye kujengea uwezo ndiye rafiki wa kweli, sio yule anaye kujengea utegemezi. Rais Magufuli anatupatia ndoana, hivyo ni jukumu letu kutafuta kitoweo. Ni pale tu tutakapotambua hili ndipo tutakapopata maendeleo katika ngazi ya chini kabisa. Tuache uvivu tufanye kazi. Baada ya kufurahia kutumbuliwa kwa watumishi wa umma, wacha na sisi tutumbuliwe!