Rais Magufuli na Libya

Nambie saiv wana ubora gani unafuu gan wameupata baada ya kifo cha gadafi?? Unapaswa kuelewa Magufuli anacho maanisha
 
Pamoja na mapungufu yake, maisha yalikuwa nafuu sana kipindi cha Gadafi kulilo ilivyo sasa, hilo wala si jambo la kujadiliana. Hata hao waliovamia wanapata wakati mgumu maana hawakujua hali ingekuwa kama ilivyo sasa. Better the devil you know...
Hivi wewe ukichukuliwa ukawekwa jela na ukalishwa kila aina ya chakula unachotaka je utafurahia ayo maisha ya kifungoni ( bila uhuru)

 
Kuna watu wanakakariri na kutumia mifano ambayo haiendani na mazingira yetu hapa afrika. Ndio maana hawaishi kuropoka, demokrasia demokrasia... .

Mfano wa model iliyofanikiwa hapa afrika ni wa libya. Lakini ni ukweli kuwa sisi magufuli hakufanya mapinduzi na wala si mwanajeshi na sisi tuna mfumo wa vyama vingi
 
Kinachotuponza watanzania ni kukosoa jambo bila kuchunguza uhalisia wake. Uhuru mnaoutaka nyinyi haupo dunia kote. Kila nchi ina sheria na taratibu zake ambazo huwezi kuziepuka.

Kuhusu Libya ni suala ambalo linatakiwa kufundishwa hata mashuleni ili wanaokuwa waelewe kile kilichotokea Libya kabla historia haijaanza kupotoshwa. Jamaa kweli alikuwa dikteka, dikteka ambaye aliandaliwa na Uingereza kuja kuitawala Libya kwa kufanya mapinduzi lakini ni kiongozi aliyependa watu wake. Na waliompinga aliwapoteza. Aliuwa mapandikizi kama 2000, lakini baada ya kutoka madarakani ni watu wangapi wamekufa huko Libya?

Dunia leo inashuhudia idadi ya wakimbizi wengi kuwahi kutokea tangu dunia ianze Huko Syria! Hivi vitu huwezi kuvielewa kama hujaamua kuvielewa...
Gaddafi alitoa skolashipu bure kwa wanafunzi kutoka afrika, na alisaidia afrika katika tozo ya satelaiti tunayotumia leo kwenye mitandao. Pia hiyo Libya ya Gaddafi ilikuwa na maisha bora kwa kila raia kuliko nchi zote za mashariki ya kati.

Sasa shida ya Gaddafi iko wapi hapo? Aliowaua ni kawaida kwa wahaini katika nchi yoyote ile, hata Tanzania Nyerere alikuwa anawapoteza watu waliokuwa wanahatarisha usalama wa serikali yake.
Uhuru mnaotaka nyinyi haupo dunia kote! Serikali lazima isimamie sema ni kwa namna tofauti. Kuna nchi zingine hata uchaguzi hautakiwi kuwepo, sababu za kiusalama na kuepusha vurugu. Ni nafuu kiongozi yule yule aendelee kutawala ili kuepusha machafuko, hii inatokea sana nchi za uarabuni.
 
Basi kama mtukufu anamuona Gaddafi alikuwa poa sana ni vizuri nae akitupeleka kuwa kama nchi ya Libya tupewe kila kitu yeye awe mtawala wa milele kama Gaddafi na baadae tuje kuwa kama Libya.

Ni mpenda fujo siyo mpenda amani,utulivu na upendo
 
Kifupi ni kwamba Mheshimiwa huwachukulia Muammar Ghadaffi na Saddam Hussein kama 'role models' wake. Anawasifia na kuwarejea kila anapoongelea suala la amani. Kwake amani huletwa kwa 'fimbo ya chuma'. Na kwake uhuru na amani ya nafsi si mambo ya msingi sana kama mtu anapata 'huduma muhimu'. Kifupi ni kwamba kwa mtazamo wake mtumwa ambaye 'bwana' wake anamhudumia kwa mavazi, malazi na chakula ni bora kuliko mtu huru anayehangaika kupata mkate wake wa kila siku kadiri anavyojaaliwa.
 
Ngoja niongee kilugha kama baba Jesca aongeapo na watanzania, "Ndamko Ndalo Biswalo..... Ndendya Atukuzwe".
 
Mleta uzi unataka Rais magufuli atolee mfano nchi gani zaidi ya Libya hapa afrika? Libya ni mfano mzuri wa nchi ya kiafrika iliyo tumia rasilimali zake bila misaada kunyanyua maisha ya wananchi wake

Kuna mfano bora kama huo hapa afrika? Mi siuoni
Mzee Karume Zanzibar,alitujengea hadi jengo la Club ya Yanga
 
Hivi wewe ukichukuliwa ukawekwa jela na ukalishwa kila aina ya chakula unachotaka je utafurahia ayo maisha ya kifungoni ( bila uhuru)

View attachment 392762
Hizi kauli zako haziwezi kufanya kazi hata hapo Rwanda. Sio kila kitu kwa lugha ya kiingereza kinafaa katika kuwakilisha hoja yako, bali mifano ya mazingira halisi ndo inasaidia
 
kwa hiyo wewe utakula udikteta?
So far 'hayo mabadiliko' yamembadilishia nini mwananchi?
Elimu bora iko wapi? na hizo dawa hospitalini ziko wapi mbona hata ukienda na watoto wadogo wanaotakiwa kutibiwa bure dawa zinazopatikana hospitalini ni zile za bei rahisi tu, na zile ghali wanasema hawana inabidi ukanunue nje?
Sikia, uwe na akili timamu. Hatuongelei uhuru wa bendera hapa. kama ni hivyo, wewe unadhani nchi za Afrika zilipata uhuru huo mapema kuliko za Ulaya na Amerika? Au unataka kusema kwamba Tanzania, Kenya, Uganda, Zambia, Ghana, etc "zilipata uhuru" kabla ya Marekani, Uingereza, Ujerumani, Norway, Uholanzi, Canada, etc?
 
hapakuwa na mtu wa kumuuliza kama kabadili kauli yake kuwa Gaddaffi alikuwa rais wa Kuwait au Libya? maana sijasikia kama alirekebisha kauli yake
 
Gadafi alikuwa ni dikteta wa kutisha.Watu kuuwawa katika mazingira ya kutatanisha ilikuwa ni kawaida mnoo wakati wa Gadaffi.Ukiwa mpinzani wa Gadaffi ata ukiwa nje ya Libya alikuwa anakutumia majasusi wakumalize.Rejea "Lockerbie bombing" ya mwaka 1988 ambapo Gadaffi alitumia majasusi wake kulipua ndege iliyouwa watu takribani 270 na wengine 10 waliongukiwa na ndege hiyo pale Lockerbie, Scotaland.

Gadafi alikuwa ana bahati Libya ina utajiri mkubwa wa mafuta.Ndio maana aliweza kutoa huduma nyingi za kijamii bure.

Libya ingekuwa na utawala wa kidemokrasia tangu enzi za Gadaffi ingekuwa ni nchi tajiri kuzidi Morocco na Algeria.

Siku zote unapomg'oa dikteta unaacha ombwe la uongozi kwa maana uongozi wote unakuwa umeteuliwa na mtu mmoja na sio na wananchi.Ombwe la uongozi lilitokea pia Uganga baada ya kung'olewa Iddi Amini mpaka alipokuja kupatikana Museveni.Pia Iraq imekumbwa na ombwe la uongozi baada ya kung'olewa Dikteta Sadam Hussein.
 
Kwani hadi Gaddafi anakufa, hizo moroko na Algeria zilikuwa ni tajiri kuliko Libya? Acheni hayo maneno kabisa, maana hata moroko ilikuwa ni nchi ya kifalme na Algeria iliongozwa na rais boutfikra kwa kipindi kirefu...someni historia muelewe
 
Lakini imevurugwa kwa kiwango gani.. Unaweza kutoa takwimu za hivi karibuni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…