Rais Magufuli na Kuuzwa kwa Polisi Oysterbay!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,815
Je raisi Magufuli kukubali utawala wake kushuhudia uuzwaji kwa waarabu wa eneo lote la Polisi Oysterbay kuanzia Namanga mpka Moroko ulioanzia utawala uliopita ili kupisha ujenzi wa shopping Mall?
Yaani Polisi Oysterbay inakwenda kuhamishwa na nyumba zao zote za kuishi ili kupisha ujenzi wa Shopping Mall ya Mwarabu!
 
Usilalamike hakuna baya lisilowezekana ktk utawala wowote wa ccm, wewe umeliona hilo tu? umesahau viwanda 460 vyote viliuzwa? na sasa ni magodauni tu? umesahau na Loliondo ilienda? iko ikulu itageuzwa kuwa Hotel ya wawekezaji.
Chezea ccm wewe?
 
Je raisi Magufuli kukubali utawala wake kushuhudia uuzwaji kwa waarabu wa eneo lote la Polisi Oysterbay kuanzia Namanga mpka Moroko ulioanzia utawala uliopita ili kupisha ujenzi wa shopping Mall?
Yaani Polisi Oysterbay inakwenda kuhamishwa na nyumba zao zote za kuishi ili kupisha ujenzi wa Shopping Mall ya Mwarabu!

Nilichangia bila kuangalia ID ya mleta mada, kumbe ni wewe kuwadi la ccm? sasa Unashangaa nini? Tuache sisi wapinzani tushangae, ondoa unafiki wako hapa.
 
Je raisi Magufuli kukubali utawala wake kushuhudia uuzwaji kwa waarabu wa eneo lote la Polisi Oysterbay kuanzia Namanga mpka Moroko ulioanzia utawala uliopita ili kupisha ujenzi wa shopping Mall?
Yaani Polisi Oysterbay inakwenda kuhamishwa na nyumba zao zote za kuishi ili kupisha ujenzi wa Shopping Mall ya Mwarabu!

Unashangaa kwan hujui utawala wa ccm
Wenye akili zetu tushajua maigizo ya magufuli
Ye ana deal na watumish kasahau wanasiasa
 
Eneo lile Rais amesema ni "prime" hivyo police wangetafuta hati na kukopa bank ili wajenge magorofa wakae!
Wazo hilo ni zuri lakini kitendo hicho kinaligeuza kutoka prime kuwa kama ma flat ya kilwa road tu.. Sio prime tena na hayana thamani kiuchumi.
Pia polisi kukopa maana ni serikali ikope na kutuongezea tena madeni kwa kujenga nyumba za polisi .Deal hatuijui lakini inahusu kujengwa kituo kipya cha kisasa zaidi cha police ..na kujengwa nyumba za kukaa polisi. Benefit nyengine hazijulikani lakini hakijauzwa ni JV agreement.
Eneo lile linakua Prime kutokana na kuweza kuendelezwa likazalisha na kuongeza ajira na kodi.
Eneo lile programm yake ni kujenga commercial property kubwa zaidi EA. Na itaajiri zaidi ya watanzania 5000 likimaliza. Kodi a,bayo tanzania itapata itatusaidia..kuendesha mambo yetu . Pia eneo hilo litasaidia kupendezesha jiji letu kwa mandhari nzuri.
Kama mwarabu shida kumpa kufanya uendelezaji basi tutafute hata mnyamwezi tumpe lakini ni bora mars million kuliendeleza kuliko kujengwa nyumba za polisi na kuchagua mazingira.
 
Taarifa za awali kuhusu mradi huo mkubwa wa kitega uchumi katika eneo hilo la sasa la Kituo cha Polisi Oysterbay, zinasema eneo hilo linakusudiwa kujengwa majengo ya kisasa, yatakayokuwa na maduka makubwa ya kisasa pia, maarufu kama ‘Shopping Malls,’ hoteli kubwa ya kitalii yenye kumbi za kisasa za mikutano, hospitali ya kisasa, ofisi za kukodisha, makazi ya kukodisha, maeneo ya maegeshi na maeneo ya kila aina ya starehe na huduma nyingine muhimu katika maisha ya kisasa.

Aidha, taarifa hizo za awali zinaeleza kwamba uamuzi huo wa Serikali, wa kuhamisha kituo hicho cha polisi kutoka hapo kilipo na mahali hapo kupewa mwekezaji, ulisukumwa na mahitaji makubwa ya nyumba za maofisa wa jeshi hilo na askari wake wa kawaida.
Kwa mujibu wa taarifa hizo za awali, Serikali inahitaji kujenga nyumba mpya 34,710 kwa ajili askari polisi na hivyo kuhitaji eneo kubwa na mpya kuliko eneo hilo la Oysterbay linaloelezwa kuwa na ukubwa wa ekari 24 tu, ambalo haliwezi kutosheleza kuwa na majengo ya kituo pamoja na nyumba hizo za askari polisi. Haikuweza kufahamika eneo hilo la Mikocheni A, ambalo kituo hicho kitahamia, lina ukubwa gani.

Uchunguzi wa FikraPevu umebaini kwamba Mshauri Mwelekezi wa Serikali kwa ajili ya Mradi huo wa Oysterbay, ili kuona kama mradi huo utakuwa na faida ni Kampuni ya Bureau for Industrial Cooperation (BICO) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Uteuzi wa kampuni ya BICO kama Mshauri Mwelekezi wa Serikali, unaelezwa kuzingatia uzoefu wa kampuni hiyo katika masuala ya uwekezaji vitega uchumi, ikiwa pia ndiyo iliyohusika katika ushauri wa wa Mradi wa Kitega Uchumi cha Mlimani City, uliko kando ya barabara ya Sam Nujoma, ambao Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ni mmoja wa wabia wa mradi huo.

Taarifa kutoka serikalini, ambazo zimethibitishwa na baadhi ya maofisa wa Polisi wa kituo hicho cha Oysterbay, zimebainisha kwamba gharama za jumla za uwekezaji katika mradi huo mkubwa wa kitega uchumi katika eneo hilo, zinakadiriwa kufikia Sh bilioni 426.6 hadi kukamilika.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Sh bilioni 395 kati ya hizo zitatumika kwa ajili ya uwekezaji wa majengo ya mradi huo, wakati Sh bilioni 31.6 zitatumika kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa kituo kipya hicho pamoja na nyumba za maofisa wake na askari wa kawaida.

Aidha, taarifa hizo zinaeleza pia baada ya kukamilika kwa mradi mzima huo, Jeshi la Polisi nchini, ambalo ndilo litakuwa mbia wa mradi huo, litakuwa linajiingizia kiasi cha Sh bilioni 4.36 kila mwaka kama tozo ya kawio, fedha itakayolisaidia jeshi hilo kutatua kero zake nyingine zinalolikabili, ikiwemo kero ya uhaba wa nyumba za kuishi askari wake.
 
Eneo lile Rais amesema ni "prime" hivyo police wangetafuta hati na kukopa bank ili wajenge magorofa wakae!
Wazo hilo ni zuri lakini kitendo hicho kinaligeuza kutoka prime kuwa kama ma flat ya kilwa road tu.. Sio prime tena na hayana thamani kiuchumi.
Pia polisi kukopa maana ni serikali ikope na kutuongezea tena madeni kwa kujenga nyumba za polisi .Deal hatuijui lakini inahusu kujengwa kituo kipya cha kisasa zaidi cha police ..na kujengwa nyumba za kukaa polisi. Benefit nyengine hazijulikani lakini hakijauzwa ni JV agreement.
Eneo lile linakua Prime kutokana na kuweza kuendelezwa likazalisha na kuongeza ajira na kodi.
Eneo lile programm yake ni kujenga commercial property kubwa zaidi EA. Na itaajiri zaidi ya watanzania 5000 likimaliza. Kodi a,bayo tanzania itapata itatusaidia..kuendesha mambo yetu . Pia eneo hilo litasaidia kupendezesha jiji letu kwa mandhari nzuri.
Kama mwarabu shida kumpa kufanya uendelezaji basi tutafute hata mnyamwezi tumpe lakini ni bora mars million kuliendeleza kuliko kujengwa nyumba za polisi na kuchagua mazingira.
umeongea vizuri na umeainisha tatizo moja kubwa hapa nchini. Tunafanya jitihada za kutosha za kuvutia wawekezaji lakini inapotokea huyo mwekezaji ni mwarabu, hapo neno mwekezaji linatoweka na badala yake agenda inakuwa "mwarabu"! This is the highest level of insanity! Waarabu wamewekeza miradi mikubwa kila pembe ya dunia sasa why Tanzanians are so pessimistic about arabs?

Anyway, Wacha tuwasubiri "wakinga" wawe mabilione waje wawekeze!
 
Back
Top Bottom