Rais Magufuli: Mwijage unanikwaza kwa kushindwa kufuta viwanda visivyoendelezwa

Katika hali isiyo ya kawaida katika ufunguzi wa kiwanda cha saruji mkoani Tanga, rais mbele ya hadhara amemtamkia waziri wa viwanda anamkwaza, anasema anaogopa nini kufuta viwanda ambavyo havijaendelezwa mbona mwenzake Lukuvi anafuta mashamba.

anasema amekua akimpa maelekezo ofsini na hata kwenye baraza la mawaziri lakini hafanyi hivyo.

mwijage kaa chonjo.
Sikio la kufa halisikii dawa.
 
Huyo Mwijage anapaswa kujiuzulu kwa hicho alichoambiwa hadharani kwani inaonekana ameshaambiwa sana lakini hatekelezi. Ni kwanini hatekelezi? Huenda kuna matatizo ya kisheria, au sababu anazopewa na wamiliki wa hivyo viwanda ni za msingi na boss wake hakubaliani nayo.

Kwahiyo njia pekee kwa Mwijage ni kujiuzulu kitu ambacho kinamuwia vigumu kwani huenda anaona aibu atachekwa kwa kishindwa kazi, ama hawezi kuachia mshahara mzuri anaopata kupitia uwaziri. Je mnakumbuka yale maneno yake ya msiniharibie kitumbua changu kwani nina watoto wadogo wa kulea? Si utamaduni wa viongozi wa kiafrika kujiuzulu, na hilo linajidhihirisha kwa Mwijage.
 
Katika hali isiyo ya kawaida katika ufunguzi wa kiwanda cha saruji mkoani Tanga, rais mbele ya hadhara amemtamkia waziri wa viwanda anamkwaza, anasema anaogopa nini kufuta viwanda ambavyo havijaendelezwa mbona mwenzake Lukuvi anafuta mashamba.

anasema amekua akimpa maelekezo ofsini na hata kwenye baraza la mawaziri lakini hafanyi hivyo.
mwijage kaa chonjo.
hatamfukuza, amempa muda arekebishe, afanye anavyotaka.
 
Mwijage week ijayo hana kazi,

Hapa ndo napata picha ya ile kauli yake kwamba ana watoto anasomesha kwa hiyo wasimponze ile kazi anaipenda,

Kwaheri mwijage.
Alitushauri tujiajiri ni zamu yake sasa kujiajiri na yeye
Maskini weekend itakuwa ndefu kwake, kama hajashinda kanisani basi anazunguka kwa waganga asitumbuliwe
 
Sio kila kitu ni cha kuongea in public.

Sometimes ni ushamba sijui? Bado sijajua nini tatizo la kila kitu kutaka watu wakisikie........

Kama alielezwa privately hakuelewa, inabidi aelezwe kwenye kadamnasi ili siku atakapokuja kuwajibishwa msirudi tena kudai kaonewa.Bosi hapangiwi, anapanga.
 
Heheee! Mwijage hapo atajinyea .. Nakumbuka ile clip flan aliyokuwa analilia ajira kwamba wasije wakamponza ana watoto wanamtegemea
Kauli kama ile inaonyesha anawaonea aibu hao watu, acha atumbuliwe tu, sijawahi mkubali, ana porojo nyingi kuliko vitendo!
 
Kwani kuna viwanda kweli vinastahili kufutwa? au vilishajifia miaka kadhaa iliyopita? Labda kama anaongelea viwanda vidogo (cherehani 4) mbele ya ofisi za ccm.
Ndo hivo inabidi kufutwa sababu vimekufa, waliobinafsishiwa wameshindwa kuendeleza. Uwe unajiongeza kabla ya kudandia mada usizozijua
 
Tanzania bila ubabe hakuna maendeleo, namkubali sana JPM, tulizoea kubembelezana na kuoneana haya, enzi hizo kwishinei

Ndio maana sikuwahi kumkubali JK tangu 2005 hadi sasa.

Naona Tanzania mpya ikija kwa kasi, ni wenye akili timamu tu ndio tunaliona hiloo
 
Back
Top Bottom