Rais Magufuli mulika Maabara ya Taifa

DidYouKnow

JF-Expert Member
Jul 28, 2019
1,094
1,691
Mheshimiwa Rais kuna uhuni mwingi katika usimamizi wa magonjwa ya mlipuko kama Corona na Ebola.

National lab wamekuwa wanajifanya kuwa wana wataalamu wanane tu wanaoweza kupima Corona kwa kutumia mashine ya PCR. Na kwamba taasisi kama KCRI, Muhimbili, Mbeya Referral na Bugando hawana uwezo huo. Wao wanadai hospitali hizo hazina watu waliosoma Molecular Biology.

Shida kubwa hapo national lab hufanya vipimo hivi kuwa wa dili. Wafanye wenyewe. Wapata allowances. Bahati mbaya sana wanabebana watu waliosoma Molecular Biology SUA, ambao hawa background ya afya ya binadamu.

PCR ni test ya kawaida sana. Na sasa PCR zote ziko automated. Zinafanya kila kitu zenyewe. Hata mtoto wa miaka mitano anaweza fanya hicho kipimo akielekezwa tu. Bahati mbaya wanajifanya wanaweza fanya wao tu.

Wataalamu wengi sana watanzania wanaweza endesha hizo mashine na zipo nyingi tu hapa Tanzania labda shida ni safety level ya maabara husika. Kuna PCR huko mikoa zinafanya vipimo vya HIV maelfu kwa mwaka. Wote hao sio graduate wa SUA tu.

Tuwaulize national lab wana accreditation ipi hadi wajione hata majibu yao ni mazuri zaidi? Wenzao KCRI na Mbeya Referral wana accreditation ya ISO na pia wana wataalam. NIMR Mbeya wana wataalamu na accreditation ya American Pathologists.

Inawezekana ndio maana majibu yao hayaaminiki.
 
Back
Top Bottom