Ndg wadau wa JF, Jana wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano akikabidhiwa ripoti ya vyeti feki pale Dodoma, alitoa amri ya wale wote waliopatikana na vyeti hivyo wafukuzwe mara moja na mishahara yao kusimamishwa.
Lakini ningependa kumkumbusha Rais kuwa mtumishi wa umma hafukuzwi hivyo, kuna hatua mbalimbali za kisheria zinazopaswa kufuatwa kabla kabla ya suala hilo kutimizwa ( kumfukuza kazi )
Lazima wote waliopatikana ktk makosa hayo wapewe haki ya kusikilizwa kwani sio kila ilichofanya NECTA ni sahihi kunaweza kuwa na makosa makubwa yamefanyika kwa baadhi ya watumishi hivyo haki yao ya kusikilizwa ni suala la msingi sana.
Serikali lazima imuandikie mtumishi huyu mashitaka na apewe muda wa kuyajibu na atakaposhindwa ndipo hatua za kumfuta kazi zinapofanya kazi. Haki ya kusikilizwa ya mtu ni jambo ambalo huwezi kulipinga wala kuliondoa ktk nchi yoyote inayofwata sheria.
Serikali haiwezi yenyewe kuwa mkamataji, mshitaki na hakimu, tukifika hapo sio sheria tena Bali ni udikiteta.
Kwa maoni yangu Rais badala ya kutoa amri alipaswa kutoa muda ili kuwapa nafasi wale wote wenye pingamizi wafanye hivyo na pia kuzipa muda mamlaka husika kufwata hatua zote za kumuondoa mtumishi husika.
Nje ya hapo tutaludi pale pale pa utumbuaji wa majipu ambako baadae serikali imejikuta inawarudisha wengine kwa aibu baada ya kuonekana si kwamba hawana hatia Bali kanuni na sheria hazikuzingatiwa ktk suala mzima la kumuondoa mtumishi huyo.