Rais Magufuli: Msigeuze vyuo maeneo ya siasa

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
RAIS John Pombe Magufuli amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu kutovigeuza vyuo hivyo maeneo ya kufanyia siasa, badala yake wavitumie kama maeneo ya kusoma na kufanya utafiti.

Dkt. Magufuli alisema kwamba, wanafunzi hao wanapaswa kujikita katika masomo wafanye vizuri na kwamba siasa watazikuta na kuzikimbia.

Aliyasema hayo jana Jumatatu, Mei 7, 2018 wakati alipozungumza na wanajumuiya ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mjini Morogoro akiendelea na ziara yake mkoani humo.

"Msivigeuze vyuo maeneo ya kufanya siasa, vitumieni kama maeneo ya kusoma na kufanya tafiti, hizi siasa mtazikuta tu na mtazikimbia wenyewe, pigeni shule," alisema.

Aidha, aliwaasa wanafunzi wasifuate mkumbo na kufanya fujo na kusababisha migomo vyuoni, kwani hatasita kuwafukuza na kuvifunga vyuo hivyo.

"Tafadhalini msifuate mkumbo, kila mmoja ana wazazi wake na amekuja hapa kwa njia anazozijua mwenyewe, kila mmoja ana maisha yake, hivyo ninawaomba someni.

"Kama kitatokea chuo chochote kinafanya fujo mimi huyu, eeeh, mimi sitasika kufukuza, na nikiwafukuza sijui nitawarudisha lini, hili lazima niwaeleze ukweli," alisema.

Akijibu hoja mbalimbali za Wanafunzi, Rais Magufuli alisema anatambua kwamba zipo changamoto nyingi, lakini baadhi zinaweza kutatuliwa na uongozi wa chuo pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Aliagiza fedha kiasi cha Shs. bilioni 2 kilichotengwa kwa ajili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kipelekwe SUA ili kujenga hosteli na kutatua changamoto ya malazi kwa wanachuo hao.

"Waziri (Profesa Joyce Ndalichako) amesema kuwa ametenga bilioni 2 kwa ajili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, naagiza hizo bilioni mbili zije hapa (Chuo Kikuu Sokoine) kwa ajili ya ujenzi wa hosteli.

"Lakini ninachotaka mimi ni ufuatiliaji na mimi najua "value for money" (thamani ya fedha)," alisema Rais Magufuli.

Alisisitiza pia kwamba, serikali yake haiwezi kutoa mikopo ya masomo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu nchini.

Alisema serikali yake imekuwa ikiongeza fedha za mikopo na kuwakopesha wanafunzi wengi zaidi lakini akasisitiza kuwa sasa haitaweza kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu.

"Nataka niwahakikishie Serikali ya Awamu ya Tano inawapenda wanafunzi wa vyuo vikuu, lakini lazima niwaambie ukweli Serikali haiwezi kutoa mikopo kwa wanafunzi wote," alisema.

Alidokeza kwamba watakaopewa kipaumbele ni wale wanaosomea udaktari, ualimu na uhandisi.

Mwishoni mwa mwaka 2017, serikali iliidhinisha Shs. 427 bilioni za mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/18.

Hata hivyo, Rais Magufuli alisema pia kwamba, kumekuwepo na udanganyifu kwa baadhi ya watu katika suala la mikopo, ambapo kwa mwaka 2017 wanafunzi 3,500 wasiostahili walipewa mikopo.

Rais Magufuli aliwaahidi wanafunzi na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine kwamba serikali yake inakichukulia kwa umuhimu mkubwa chuo hicho kama mboni ya jicho, kwani ndicho pekee kinachoweza kuleta mabadiliko ya kweli katika mapinduzi ya kilimo na hivyo kusaidia kutekeleza kauli mbiu ya Tanzania ya Viwanda.

"Tunakichukulia chuo hiki kwa umuhimu wa kipekee kabisa na tumeandaa mipango kamambe kufanya complete reform as far as agriculture is concerned(mabadiliko makubwa kwa kadiri kilimo kinavyohitaji)," alisema.

Awali, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, alisema SUA ndiyo chuo kilichopewa fedha nyingi za maendeleo kuliko vyuo vingine hapa nchini, ambapo kimepewa jumla ya Shs. bilioni 8.

Lakini Rais Magufuli alisifu na kukipongeza chuo hicho kutokana na mchango mkubwa wa maendeleo ambao kimeutoa tangu kuanzishwa kwake, hususan katika tafiti mbalimbali.

"Moja ya tafiti kubwa iliyowahi kufanywa na ikakitambulisha chuo na nchi kimtaifa ni ile tafiti ya kuwafundisha panya kugundua mabomu na kugundua ugonjwa wa Kifua Kikuu, nawapongezeni sana," alisema.

Alisema kwamba, wakati akiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, na alipokuwa waziri takriban miaka 20 ndiyo alipogundua kuwa sekta ya kilimo ina mchango mkubwa kwenye kukuza uchumi wa nchi na kwa maendeleo ya taifa.

"Tumeamua kuwa na viwanda na tumeamua kuwa viwanda vyetu hivyo vitumie malighafi za hapa hapa Tanzania, kwa maana hakuna viwanda kama kuna malighafi mbovu na malighafi nzuri zitapatikana kutokana na chuo hiki (SUA)," alisema.

Akaongeza: "Wasomi wa SUA na wasomi wa Tanzania kwa ujumla tujiulize, ni kwa nini tuna ng'ombe wengi na ni wa pili kwa Afrika lakini tunazidiwa na nchi nyingine kuwa na viwanda vya maziwa ambazo hazina hata ng'ombe wengi? Tuna ng'ombe wengi lakini hatuna viwanda vya nyama?”

"Nianaamini katika hatua zote mlizozichukua, Chuo Kikuu hiki (SUA) kitakuwa ni chanzo cha kubadilisha maisha ya Watanzania wengine, mimi ninaamini hivyo, endeleeni hivyo.

"Nataka dhamira ya Baba wa Taifa (Mwalimu Julius Nyerere) aliyeamua kuanzisha chuo hiki, kupitia serikali ya awamu ya tano tunataka tuifufue dhamira hiyo na tukienda vizuri hapa naamini Tanzania ya viwanda itafanikiwa.

"Hata watu wanaosema elimu imeshuka, sijui kama wamefika hapa, hapa ambapo wanawafundisha panya kugundua mabomu na kifua kikuu," alisema Rais Magufuli.

Ili kukijengea uwezo zaidi chuo hicho, Rais Magufuli aliahidi kukipatia matrekta 10 kwa ajili ya kuendeleza miradi ya kilimo, huku akisema uzalishaji huo utasaidia kukifanya chuo kijiendeshe na kutatua baadhi ya changamoto.

Mwisho.
 
Hongera sana Mh,

Usiishie hapo tu pia tunakuomba ufute matawi ya vyama vya siasa hasa hasa CCM na CHADEMA, ujenzi wa chuo kikuu cha CCM kitakachokuwa kinafundisha siasa, futa course mbali mbali kama vile political science n.k,

Walimu wa hayo masomo nao wote warudi makwao wakalime. Nakupongeza mh maana siasa vyuoni ni adui wa maendeleo.
 
Naamini alimaanisha usitumie muda wa masomo katika Siasa maana hukufuata Siasa chuoni.
 
Hongera sana Mh,

Usiishie hapo tu pia tunakuomba ufute matawi ya vyama vya siasa hasa hasa CCM na CHADEMA, ujenzi wa chuo kikuu cha CCM kitakachokuwa kinafundisha siasa, futa course mbali mbali kama vile political science n.k,

Walimu wa hayo masomo nao wote warudi makwao wakalime. Nakupongeza mh maana siasa vyuoni ni adui wa maendeleo.
Machafuko punguza munkari
 
Ile clip ya kampeni Tabora kuhusu mikopo ya elimu ya juu nani anayo? Tujikumbishe kidogo!
 
RAIS John Pombe Magufuli amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu kutovigeuza vyuo hivyo maeneo ya kufanyia siasa, badala yake wavitumie kama maeneo ya kusoma na kufanya utafiti.

Dkt. Magufuli alisema kwamba, wanafunzi hao wanapaswa kujikita katika masomo wafanye vizuri na kwamba siasa watazikuta na kuzikimbia.

Aliyasema hayo jana Jumatatu, Mei 7, 2018 wakati alipozungumza na wanajumuiya ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mjini Morogoro akiendelea na ziara yake mkoani humo.

"Msivigeuze vyuo maeneo ya kufanya siasa, vitumieni kama maeneo ya kusoma na kufanya tafiti, hizi siasa mtazikuta tu na mtazikimbia wenyewe, pigeni shule," alisema.

Aidha, aliwaasa wanafunzi wasifuate mkumbo na kufanya fujo na kusababisha migomo vyuoni, kwani hatasita kuwafukuza na kuvifunga vyuo hivyo.

"Tafadhalini msifuate mkumbo, kila mmoja ana wazazi wake na amekuja hapa kwa njia anazozijua mwenyewe, kila mmoja ana maisha yake, hivyo ninawaomba someni.

"Kama kitatokea chuo chochote kinafanya fujo mimi huyu, eeeh, mimi sitasika kufukuza, na nikiwafukuza sijui nitawarudisha lini, hili lazima niwaeleze ukweli," alisema.

Akijibu hoja mbalimbali za Wanafunzi, Rais Magufuli alisema anatambua kwamba zipo changamoto nyingi, lakini baadhi zinaweza kutatuliwa na uongozi wa chuo pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Aliagiza fedha kiasi cha Shs. bilioni 2 kilichotengwa kwa ajili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kipelekwe SUA ili kujenga hosteli na kutatua changamoto ya malazi kwa wanachuo hao.

"Waziri (Profesa Joyce Ndalichako) amesema kuwa ametenga bilioni 2 kwa ajili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, naagiza hizo bilioni mbili zije hapa (Chuo Kikuu Sokoine) kwa ajili ya ujenzi wa hosteli.

"Lakini ninachotaka mimi ni ufuatiliaji na mimi najua "value for money" (thamani ya fedha)," alisema Rais Magufuli.

Alisisitiza pia kwamba, serikali yake haiwezi kutoa mikopo ya masomo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu nchini.

Alisema serikali yake imekuwa ikiongeza fedha za mikopo na kuwakopesha wanafunzi wengi zaidi lakini akasisitiza kuwa sasa haitaweza kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu.

"Nataka niwahakikishie Serikali ya Awamu ya Tano inawapenda wanafunzi wa vyuo vikuu, lakini lazima niwaambie ukweli Serikali haiwezi kutoa mikopo kwa wanafunzi wote," alisema.

Alidokeza kwamba watakaopewa kipaumbele ni wale wanaosomea udaktari, ualimu na uhandisi.

Mwishoni mwa mwaka 2017, serikali iliidhinisha Shs. 427 bilioni za mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/18.

Hata hivyo, Rais Magufuli alisema pia kwamba, kumekuwepo na udanganyifu kwa baadhi ya watu katika suala la mikopo, ambapo kwa mwaka 2017 wanafunzi 3,500 wasiostahili walipewa mikopo.

Rais Magufuli aliwaahidi wanafunzi na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine kwamba serikali yake inakichukulia kwa umuhimu mkubwa chuo hicho kama mboni ya jicho, kwani ndicho pekee kinachoweza kuleta mabadiliko ya kweli katika mapinduzi ya kilimo na hivyo kusaidia kutekeleza kauli mbiu ya Tanzania ya Viwanda.

"Tunakichukulia chuo hiki kwa umuhimu wa kipekee kabisa na tumeandaa mipango kamambe kufanya complete reform as far as agriculture is concerned(mabadiliko makubwa kwa kadiri kilimo kinavyohitaji)," alisema.

Awali, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, alisema SUA ndiyo chuo kilichopewa fedha nyingi za maendeleo kuliko vyuo vingine hapa nchini, ambapo kimepewa jumla ya Shs. bilioni 8.

Lakini Rais Magufuli alisifu na kukipongeza chuo hicho kutokana na mchango mkubwa wa maendeleo ambao kimeutoa tangu kuanzishwa kwake, hususan katika tafiti mbalimbali.

"Moja ya tafiti kubwa iliyowahi kufanywa na ikakitambulisha chuo na nchi kimtaifa ni ile tafiti ya kuwafundisha panya kugundua mabomu na kugundua ugonjwa wa Kifua Kikuu, nawapongezeni sana," alisema.

Alisema kwamba, wakati akiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, na alipokuwa waziri takriban miaka 20 ndiyo alipogundua kuwa sekta ya kilimo ina mchango mkubwa kwenye kukuza uchumi wa nchi na kwa maendeleo ya taifa.

"Tumeamua kuwa na viwanda na tumeamua kuwa viwanda vyetu hivyo vitumie malighafi za hapa hapa Tanzania, kwa maana hakuna viwanda kama kuna malighafi mbovu na malighafi nzuri zitapatikana kutokana na chuo hiki (SUA)," alisema.

Akaongeza: "Wasomi wa SUA na wasomi wa Tanzania kwa ujumla tujiulize, ni kwa nini tuna ng'ombe wengi na ni wa pili kwa Afrika lakini tunazidiwa na nchi nyingine kuwa na viwanda vya maziwa ambazo hazina hata ng'ombe wengi? Tuna ng'ombe wengi lakini hatuna viwanda vya nyama?”

"Nianaamini katika hatua zote mlizozichukua, Chuo Kikuu hiki (SUA) kitakuwa ni chanzo cha kubadilisha maisha ya Watanzania wengine, mimi ninaamini hivyo, endeleeni hivyo.

"Nataka dhamira ya Baba wa Taifa (Mwalimu Julius Nyerere) aliyeamua kuanzisha chuo hiki, kupitia serikali ya awamu ya tano tunataka tuifufue dhamira hiyo na tukienda vizuri hapa naamini Tanzania ya viwanda itafanikiwa.

"Hata watu wanaosema elimu imeshuka, sijui kama wamefika hapa, hapa ambapo wanawafundisha panya kugundua mabomu na kifua kikuu," alisema Rais Magufuli.

Ili kukijengea uwezo zaidi chuo hicho, Rais Magufuli aliahidi kukipatia matrekta 10 kwa ajili ya kuendeleza miradi ya kilimo, huku akisema uzalishaji huo utasaidia kukifanya chuo kijiendeshe na kutatua baadhi ya changamoto.

Mwisho.
Tunapenda thread za namna hii,hujaogeza wala kupunguza neno,safi sana ,wale wenzetu wanatafuta kaneno ka kuingilia jukwaani ili watukane,wanafikiri Magufuli is a perfect person
 
Back
Top Bottom