Rais Magufuli: Mh. Heche toa mkono mfukoni unapozungumza na mimi, wewe ni kama mwanangu wa kumzaa

Ni kweli kabisa. Ndani ya ccm nani atamkubali mtu ambaye kabla ya kusema NDIYO lazima ahoji?
Majibu ya Heche Leo hadi akanyang'anywa mic ni kama vile mkulu kapigwa upper cut ndani ya mchezo wa boxing.
CCM hii ya ndio mzee mnaiweza nyie pekee wenye vipaji vya unafiki
Hivi wewe kweli unaweza kumkatalia Mbowe?
 
Mfuko wa Jimbo TZS.58M kwa mwaka, Ina maana Wabunge kibindoni kuna takriban TZS.150M. Tujiulize, walizotuletea Jimboni ni kiasi gani? Tutambue kuwa tunaendelea kujiumiza kwa Kuendekeza Itikadi za Kisiasa kwa Misingi ya Vyama
 
Akiwa kwenye mkutano na Wananchi wa Tarime, baada ya mwanafunzi kumweleza Changamoto za shule alimuuliza mbunge huyo kuhusu fedha za jimbo, mbunge huyo akawa anamjibu, Magufuli akamkatisha akamawambia sitaki maelezo mengi, nimekuuliza swali Rahisi tu, Mbunge akaelezea baada ya kumaliza Magufuli akamkosoa tena kuongea naye huku ameweka mikono mfukoni na kumwambia hiyo ni dharau kwa kuwa yeye ni kama mwanae wa kumzaa



Rais Magufuli alikuwa akichangisha michango baada ya mwanafunzi kumwekezea kero kwenye shule yao

Inawezekana alihofu akahisi kujikojolea kwa hiyo akaweka mkono mfukoni ili kuzuia.
 
hahhaha kumbuka hizi ni kila mwezi...kwa hiyo kama hazitoshi kwa mradi basi azitafune tu..ruhsa sio...?..mbunge wenu amewaaibisha sana..mnaonekana.wote wezi kumbe...kila mtu akipata nafasi anachota..na tabia hii kawafundisha mzee wenu na mwenyekigoda..hatuwalaumu saaana..wacha tumezee kwanza
Usidandie gari kwa mbele! Kama hujui uliza na hutaitwa mjinga! 58M ni kwa mwaka na siyo kwa mwezi kama unavyodai!
 
Hata kama ilikuwa ni kweli, sidhani kama pale ilikuwa mahala pake, na hasa ukizingatia kuwa yeye ni mpinzani, UNAMCHONGEA mteule wake ili amtumbue! Alichokipata, NILIKITEGEMEA!
Sote tulishuhudia mahojiano yalivyokuwa, yalikuwa mahojiano ya wazi kabisa na ukweli ukajulikana
 
Back
Top Bottom