VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Kulingana na sera-kauli yako ya 'Tanzania ya Viwanda', kuna Mawaziri wawili ndiyo hasa watakaokubeba au kukuangusha. Hawa ni Waziri wa Viwanda na Biashara na Waziri wa Nishati na Madini. Pamoja na kuthamini na kuamini mchango wa Wizara nyinginezo, Wizara hizo mbili ndizo hasa moyo wa Serikali ya awamu ya tano.
Waziri wa Viwanda ni Charles Mwijage. Waziri wa Nishati na Madini ni Prof. Sospeter Muhongo. Mawaziri hawa wanapaswa kuwa wabunifu, wachapa kazi wa kupigiwa mfano na hata wathubutu. Pia, wanapaswa kuwa washawishi (kuhusu uwekezaji katia viwanda na nishati) na kadhalika. Mawaziri hawa wanapaswa kufanya kazi usiku na mchana.
Awamu ya tano iko migongoni mwao. Mafanikio au kushindwa kwa Rais Magufuli kuko migongoni mwao. Uhalisia wa sera-kauli 'Tanzania ya Viwanda' uko kwao. Wao ndiyo hasa wanaopaswa kuwa murua na bila mawaa. Je, Waziri Mwijage 'anatosha vya kutosha na kutisha kwenye Wizara ya Viwanda na Biashara? Je, Prof. Muhongo anatosha Nishati na Madini?
Bastola ya nini tena jamani!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)