Rais Magufuli, makomandoo kupamba Sherehe za miaka 53 ya Muungano Dodoma

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945

Maonesho ya ukakamavu na mbinu za medani katika kupambana na adui hasa kulinda amani ya nchi yetu kutoka Kikosi Maalum cha Makomandoo wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), itakuwa ni sehemu ya shamrasha zitakazopamba maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yatakayofanyika kwa mara ya kwanza mjini Dodoma Aprili 26 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama maadhimisho hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, pia yatapambwa na burudani nyingine kutoka vikundi mbalimbali.

Taarifa ya Waziri Mhagama ametaja shughuli nyingine zinazotarajiwa kufanyika siku ya Muungano kuwa ni gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama (JWTZ,JKT, Polisi na Magereza) na onesho la mbwa na farasi waliofunzwa.

Aidha, Waziri Mhagama aliongeza kuwa mambo mengine yatakayofanyika ni gwaride la uzalendo la wanafunzi wa shule za sekondari za Dodoma, burudani za vikundi vya ngoma za asili kutoka Dodoma na Zanzibar, Yamoto Band, vikundi vya muziki wa kizazi kipya kutoka kwa wasanii Mchungaji Zayumba, Jacob Beats, Mwenge Jazz Band na Mgosi Matarumbeta.

“Kauli mbiu ya sherehe za kutimiza miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni Miaka 53 ya Muungano; Tuulinde na Kuumarisha, Tupige Vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii,”alifafanua Waziri Jenista Mhagama.

Ametoa wito kwa wananchi wote nchini kusherehekea siku hiyo muhimu kwa kudumisha amani, upendo, umoja na mshikamano kwa maendeleo ya nchi.

“Ninaomba kuchukua nafasi ya pekee kuwaomba wananchi wote waliopo Dodoma kujitokeza kwa wingi uwanja wa Jamhuri siku hiyo ya Jumatano tarehe 26 Aprili 2017 kuanzia saa 12:00 asubuhi ili kusherehekea kwa pamoja maadhimisho hayo muhimu kwa nchi yetu,”alisema Jenista Mhagama.

Maadhimisho ya Muungano yanafanyika kwa mara ya kwanza Dodoma ikiwa ni siku kadhaa tangu Serikali ya Awamu ya tano ianze kutumiza azma ya kuhamia katika makao makuu hayo mapya

HABARI MAELEZO
 
hiyo ratiba(matukio) tunaifahamu mbona hata hakukuwa na haja ya kuisema lbd kutukumbusha hiyo tarehe ahsente.
Hivi ule mchanganyo wa sehemu ya ardhi kutoka Tanganyika na Zanzibar ulifanyika wapi vile?

Je, katika mchanganyo huo ; udongo kutoka Zanzibar ulihusisha mchanyato wa udongo kutoka visiwa vya Unguja na Pemba? Au udongo huo ulitoka kisiwa kimoja?
Kuuliza si ujinga bali ni sehemu ya kutaka kujifunza...
 
Wabadilishe style banaa walete wale wa miamvuli na wakimbize ndege mbili 3 walete vifaru inatosha!!! Wale wakomavu wapasua tofali tumekinai banaa!! Hawana jipya wale ni wanyanyua vyuma tu wanamaliza ration za jeshini hakuna kitu banaaa!!
 
kuna majitu siku jpm alivyokataa maadhimisho ya siku ya uhuru december 9 ,2015 walishangilia sana kuwa hakuna umuhimu wa kuangalia makomando wakivunja tofali kwa ugoko,cha ajabu mwaka jana tarehe na mwezi kama huo yakawa kwenye Tv yanashabikia hao hao makomando,stupid tanzanian
 
Yani adui asubiri umtishe kwa kuvunja tofali anakuangalia tu. Wamekuwa kama bongo movies, scene zile zile tangu Uhuru,tumewachoka bwana aahh!!!
 
Mafunzo yao yako karibu sawa na ya USA NAVY SEAL au? Mi nauliza tu, kwa sababu tunataka kuona tekinolojia zaidi ikitumika, hata japo itumike inayoendana na uwezo wetu, hii ya kutumia maguvu kuvuta gari kwa mikono na kupiga mateke matofali mi naona kama ya kizamani vile!!!
 
Hivi ule mchanganyo wa sehemu ya ardhi kutoka Tanganyika na Zanzibar ulifanyika wapi vile?

Je, katika mchanganyo huo ; udongo kutoka Zanzibar ulihusisha mchanyato wa udongo kutoka visiwa vya Unguja na Pemba? Au udongo huo ulitoka kisiwa kimoja?
Kuuliza si ujinga bali ni sehemu ya kutaka kujifunza...
Uchochezi
 
Mafunzo yao yako karibu sawa na ya USA NAVY SEAL au? Mi nauliza tu, kwa sababu tunataka kuona tekinolojia zaidi ikitumika, hata japo itumike inayoendana na uwezo wetu, hii ya kutumia maguvu kuvuta gari kwa mikono na kupiga mateke matofali mi naona kama ya kizamani vile!!!
acha hizo USa navy seal ni sea,air and land je comando wetu wana uwezo huo
 
Back
Top Bottom