Rais Magufuli: Magazeti yanayoandika kuna njaa yamenunuliwa na wanasiasa na wafanyabiashara

Anaejua kuna njaa nchi hii ni Rais, mimi ndio ninayejua wapi kuna njaa na wapi hakuna. Tanzania hii haina njaa wala watu hawana njaa,anasema Rais JPM kutoka Simiyu

Wanaotangaza kuna njaa ni watu wanaolipwa pesa na wafanyabiashara na wanasiasa ili kusema nchi ina njaa na ukame wa kuuwa watu na mifugo.

Yapo magazeti yanayotumiwa na wafanyabiashara na wanasiasa ili kusema Tanzania kuna njaa. Kuna mfanyabiashara mmoja ana tani 25,000 za mahindi bandarini anataka aingize bila kodi kwa kisingizio cha njaa Tanzania. Rais anasema ameagiza alipe kodi na asipitishe mahindi hayo bure kwa kisingizio cha njaa, Tanzania haina njaa.

Kuna mfugaji mwingine walimlipa hela wanasiasa huko Mvomelo, akaenda mbele ya Tv na kusema ana mifugo inakufa kwa ukame.

"Nimeagiza wamwambie auze hizo ng'ombe ili aepukane na ukame. Huwezi kuwa na ng'ombe karibu elfu na zaidi na wanakufa ng'ombe 16 unaanza kulialia badala ya kuuza upate hela ya kula na ujikimu kimaisha."

Rais anasema hatapeleka chakula Simiyu na Bariadi eti kisa ukame. Wananchi walitakiwa kujua kama mvua ni ndogo basi walime mazao yanayostahimili ukame na si kulazimisha kulima mahindi yanayohitaji mvua nyingi. JPM anasema msema ukweli ni mpenzi wa Mungu na yeye anasema ukweli kuwa hataleta chakula popote kwa sababu ni wanasiasa na wafanyabiashara ndio wananunua magazeti kutangaza njaa.

Rais kamuumbua Dr Kamani, mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu anayemtaka Rais aruhusu kuingiza mifugo kwenye hifadhi, wakati yeye akiwa waziri wa Mifugo wakati wa JK hakufanya hivyo, sasa kama sio unafiki ni nini? JPM anasema yeye sio mnafiki, hataruhusu mifugo kuingia kwenye hifadhi kwa sbb ya sifa za kisiasa huku akiharibu mazingira.

Rais anasema Watanzania walizoea kuambiwa maneno "matamu matamu" na wanasiasa huku muda ukienda bila kuwa na maendeleo. Yeye anataka watanzania wasahau maneno matamumatamu. Ataongea ukweli tu,tena ukweli mchungu hata kama utawaudhi watu, kama ni jiwe atasema jiwe na sio mchanga mgumu uliokusanyika pamoja.

Rais amewaomba Watanzania wazidi kumuombea, wapo "wapinzani" wake wanamsimanga kwa kununua ndege, na wakati kwa miaka mingi Tanzania haikuwa na ndege, na hao wanaomkosoa ndio hao hao wanaokimbilia kuzipanda.

Baadae Rais akamuita mhandisi Maji wa Mkoa wa Simiyu ili aje aelezee mpango wa Maji kutoka Ziwa Victoria kuja mkoa wa Simiyu na Wilaya zake... Mhandisi hakutoa majibu mazuri, akaja RAS ambaye akasema kikwazo ni mlima wa Ngasamo ambao una madini ya Nikel(?) ambao ndio ilipaswa kuwa na tank la kuleta maji.

Rais ameagiza eneo hilo kuwekwa Tank ili wananchi wa Simiyu wapate maji. Amemuagiza Kamishna wa madini aifute leseni endapo mwekezaji wa mgodi husika hatoridhishwa na maamuzi hayo, na kusisitiza ujumbe umfikie Waziri wa Madini.

Na mwisho Rais amesisitiza watu wafanye kazi, hakuna wa kugawiwa chakula bure. Hawezi akawasomeshea watoto bure,ajenge barabara, anunue ndege, ajenge hospitali na kuweka madawa ktk hospital, alete huduma ya maji na bado watu wakae tu na kusubiri eti serikali itawatafutia chakula.Watu wafanye kazi ili wapate chakula na si kusubiri chakula cha serikali.

"SERIKALI YANGU HAITATOA CHAKULA, NINAPOSEMA SILETI CHAKULA SILETI KWELI, WALA SIMUNG'UNYI MANENO NA SITALETA KWELI, MLIZOEA MANENO MATAMU SASA MIMI SINA MANENO MATAMU" alisisitiza Rais Magufuli.

Mwishoni Rais amemalizia kwa kusema: "Naweza kuwa sio mwanasiasa mzuri sana, Lakini ipo siku mtakuja kunikumbuka"
Mimi anaposema hapeleki chakula naona sawa tu. Nikuwa nikiangalia huo msaada wa chakula kaya inapewa kilo 5 au 10 halafu unaona serikali imesaidia kuondoa njaa? Huo si mlo wa siku 10 tu.. Sawa kabisa wacha tufanyekazi. Asiyefanyakazi na asile!

Ila ukweli ni kwamba kuna ukame maeneo mengi ya nchi, hivyo bei ya vyakula itakuwa si rafiki, mifugo itaendelea kufa pia. Bilashaka mgao wa umeme utatunyemela..
 
majibu hyo ypo kwenye mkutano na wanahabari pale ikulu,akijibu swali la pascal mayalla sasa naona mnasumbuka nae bure tu.
 
Nilishauri hapa kuwa kama Rais anataka kujua ugumu wa maisha na kuanza kuheshimu watu wake Sera yakubana matumizi ianzie Ikulu.....


Ushauri: Sera ya kubana matumizi tuanzie Ikulu

Ikulu ijinunulie chakula chake kutoka kwenye mshahara wa Rais kama wanavyofanya Marekani.

Hivi Rais unawezaje kujua kuwa hakuna njaa kuliko mwananchi anayeishi huko Lamadi,Mwabasabi,Nyamikoma,Kahangara,Bundilya,Nyanguge na kisesa....

Au Rais unawezaje kujua kuwa chakula kipo cha kutosha kuliko wananchi wanaishi Tandale,Magomeni,Mtoni kwa azizi Ally,Mbagala kuu ,Mbande na nk.

Hivi Rais uwa anatoka Ikulu kwenda kununua sembe mtaani?

Au analishwa tu na kodi zetu bila kujua hata chakula kunanuliwa sangapi?....

Hivi Rais anaweza kujua mchele umepanda bei lini sangapi?

Kwa kutumia hawa washauri wanaoisha hapo Ostabay? Tena kwa kodi zetu pia kula bule kulala bule.

Au wakuu wa wilaya wanaowaweka ndani waandishi wanaotoa taarifa za njaa huko mtaani?....

Kama tu unawashangilia wanahujumu maendeleo ya wananchi kama wanavyofanya wakina Gambo pale Arusha unawezaje kuwahurumia wananchi wanalia njaa na ukame?......

Mr Rais umepotoka kama si kulewa madaraka kila mtu aliye makini anakushangaa kwa kuyakana yote uliyaahidi kipindi chako cha kampeni ...

Sembe itapanda wewe utaendelea kuwa Ikulu na kula kuku kwa mlija watakaotaabika ni wananchi wa kiwango cha chini.......

Mchele utapanda na wewe utaendelea kukaa Ikulu uku ukitoa matamko ya kuwakashifu wananchi wako ambao ndio walipa kodi iliyokuweka ikulu.....

Ndio maana nikashauri angalau na wewe ungesikia machungu kiasi ungetumia mshahara wako wa Milioni 36 kwa mwezi kununua Sembe na Mchele ili uweze kujitunza mwenyewe...

Washauri wako wanapotosha ukweli, hata kama unasema kuna tani 25,000 bandarini hivi tani hizo zinaweza kuzuia njaa kweli? Chakula cha kugawa kwenye kata moja kikaisha unasema eti kinataka kuingia bure bila kulipa kodi unachekesha sana watu weredi....

Tunakushangaa na tutaendela kukushangaa kwa matamko yako yanayo onyesha ni jinsi gani ulivyo na chuki na wafanya biashara wakati ukipata janga unawaita Ikulu wakuchangie pesa za kujenga barabara zilizo aribika kwa tetemeko kama unavyofanya uko Kagera...


Raisi amesema mwenye jukumu la kutangaza Baa la njaa kwa mujibu wa Katiba ya JMTZ ni Raisi wa JMTZ, hivyo wote wanaotangaza njaa wanavunja Sheria ya nchi!
 
Tuliipenda wenyewe ndindi,tulichagua wenyewe ndindi acha tuisome namba eeee sisiemu mbele kwa mbeleee
 
Back
Top Bottom