Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,706
- 149,945
Nimesoma gazeti la Mwanahalisi la Jumatatu, April 25-Mei 1,2016 na kukutana na taarifa ya kusikitisha kuhusu sakata zima la Escrow na pia mwandishi amegusia juu ya maazimio ya Bunge kuhusiana na kashifa hii ya mabilioni ya shilingi.
Baadhi ya mambo ambayo Bunge lilitaka serikali kuyafanyia kazi ni pamoja na haya.
Bunge liliigiza serikali kufikisha mahakamani watuhumiwa wote wa Escrow,ikiwa ni pamoja na kufilisi mtambo wa IPTL na kuitangaza benki ya Stanbic kuwa taasisi ya kutakatisha fedha.
Bunge liliagiza pia kuchunguza na kuwajibisha majaji waliotajwa kunufaika na mgao wa fedha kupitia benki ya Mkombozi na kumfukuza nchini,anaejiita mmilki wa IPTL,Harbinder Sigh Seth.
Maoni ya Lissu kuhusu sakata hili alipohojiwa na mwandishi wa gazeti hili yamenukuliwa kama ifuatavyo:
"....hili liserikali lote limeoza.Kuanzia Ikulu,mfumo wa mahakama hadi viongozi wa madhehebu ya kidini;kote kumejaa rushwa."
Lissu ameongeza, "Tulisema ndani ya Bunge,kwamba majaji wamehongwa na hivyo tukataka wachunguzwe,lakini serikali ya CCM imegoma kwa kuwa walioiba waliwajua na walishirikiana nao."
Mwanasiasa huyo wa upinzani anasema,"utapeli huu ulifanywa na serikali ya Raisi Kikwete, BOT, Benki ya Stanbic na PAP."
Amesema,"......sasa kama kweli wanataka kusafisha nchi,basi waanzie hapo.Siyo kukimbizana na vidagaa.Waanze na maofisa wao wa Ikulu waliokuwa wameigeuza ofisi ya umma kuwa ofisi binafsi."