Kwa kweli tunayo kila sababu ya kujisifu uwepo wa mkuu wetu JMP. TBA ni kati ya idara ya serikali iliyoaminika kuwa haiwezi chochote na wababaishaji. Ilifika mahala tukaona TBA ni mzigo hadi tukaamua kuuza baadhi ya nyumba za serikali kwa maana ya kutua mzigo.
Kumbe hili shirika si tu lina wataalamu bali lina wazalendo na wachapa kazi, sote tumeona kazi zao nzuri pale UDSM wamejenga majengo safi na kwa muda mwafaka, kazi hizi tulizoea kuzisikia kwa benjamini Netanyahu anapojenga makazi ya wayahudi. kumbe na sisi tunaweza. kwa kweli JPM nitamwita African Bibi.
TBA wamekamilisha ujenzi wa mabweni, wanaelekea kukamilisha ujenzi wa shule ya Ihungo na sasa wameanza ujenzi wa makazi bora na ya kisasa ya Magomeni, hongereni sana.
Sasa hebu tufufue na mashirika mengine, miaka ya themanini kulikuwa na shirika la umma la MECCO lililo jishughulisha na ujenzi wa barabara, huku kwetu hadi leo kuna mtaa unaitwa mecco eneo hilo lilikuwa kambi ya kampuni hiyo, pia lilikuwepo shirika la PEHCOL hili lilikuwa linakodisha mitambo ya ujenzi wa barabara na ilikuwepo idara ya serikali iliyoitwa common works hii idara ilijishughulisha na repair ndogondogo za barabara. Tukifufua mashirika haya naimani kabisa gharama za ujenzi wa barabara zitapungua sana. tuachane na wachina sasa.
Napendekeza Prof. Mbarawa akae na JPM wateue bodi ya wakurugenzi na wateue CEO walifufue shirika hili la umma, tujenge barabara wenyewe, tuwatumie vijana wetu wa sumajkt katika ujenzi wa barabara na miundo mbinu mbalimbali. Tunaweza anza kulitumia shirika letu la mecco katika ujenzi wa reli mpya sambamba na kampuni hii ya kireno.