Rais Magufuli; Kuongoza kizazi hiki lazima uwe dikteta tu, bila hivyo nchi itakushinda

BM Pesambili

Senior Member
Jul 10, 2016
102
624
Naililia nchi yangu Tanzania , kila nikitafakari machozi yananitoka nakosa majibu nabaki kujiuliza tutafika kweli? Magufuli kazi unayo sana kuongoza kizazi hiki cha vilaza pole sana!

Limekuwa taifa la ajabu ajabu sana, viongozi wake (UKAWA & CCM)wamekuwa wanafiki, wazandiki, waongo hawaaminiki tena katika jamii. Wameruhusu kiburi na jeuri kuwavika kama mkufu shingoni mwao. Wana mawazo na mapenzi machafu mioyoni mwao. Kila kiongozi amekuwa muongo tu, kauli na videndo haviendani, ni wasaliti wa kwanza wa kauli zao wenyewe. Walimtangaza mchafu nchi nzima watanzania wakaamini hivyo gafla wakageuka tena kumtangaza msafi nchi nzima watanzania wakaamini tena hivyo bila kuwaoji kauli zao zile za mwanzo walizozisaliti wenyewe. Nchi imekuwa ya wanafiki sana hii. Tumekuwa jamii ya watu wa ajabu sana, tumebaki kuangalia mambo juu juu tu, na kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu , jamii iliyojaa wapuuzi na wanafiki wengi.

Kila kukicha upendo unapungua baina ya watanzania, visasi, dhuluma, wizi, ubakaji, ufedhuli, majivuno, matabaka, ukada na umasikini unazidi kutumaliza. Ee Mungu wetu tusaidia kizazi hiki cha vilaza. Tumebaki kuabudu watu weupe na vitu vyao na uchafu wao wote. Tumekubali kuporwa utu wetu na kufanywa vivuli vya wazungu kiasi cha kupoteza hata utamaduni wetu.

Tumekuwa na vijana na wasomi wa hovyohovyo, kushinda kwenye mitandao kuanzia asubuh mpaka jioni kuangalia vipicha vya uchi uchi na ngono( ponograph), Kutukanana na kupost vipicha vya kipuuzi kwenye mitandao. Vinguo vyao wanavyovaa vya ajabu visizo hata maadili. Wanapenda vimagazeti na vijarida vya ngono ngono tu. Mada za mapenzi na mambo ya kipuuzi yanapewa kipaumbele kuliko hata mambo ya kitaifa. Kwenda kulima na kufanya kazi hawataki, viwanda vitakuja kwa muujiza gani?

Magufuli Rais wangu pole sana kuongoza jamii ya mashoga na wasagaji, wavuta bange na madawa ya kulevya. Mandanguro kila kona yamejaa madada poa na makaka poa wanashindania wateja na bahati mbaya wateja wao wengi ni viongozi wetu hawahawa wanaopiga marufuku mchana usiku ndio wateja wao. Taifa lawanafiki sana hili.

Makanisa na misikitini kwetu kama kimbilio na msaada kwa matatizo haya lakini huko ndiko kuna balaa. Hii ya makanisa niache nitaleta mada yake baadae maana inahitaji hekima ya Mungu sana kuijadili. Tumekuwa na uelewa finyu hata katika masuala ya msingi yanayohusu taifa letu, uelewa finyu unatufanya turubuniwe kirahisi au tuelekeze nguvu zetu kwenye mambo ambayo yanaonekana katika nyuso zetu kama ndio utatuzi wa matatizo yetu kumbe ni upuuzi.

Tuna wasomi wengi lakini wameshindwa kujiamini na kujisimamia. Wamekuwa ndio chanzo cha matatizo yetu. Wameshindwa kabisa kujitambua, kudadisi, kujituma, kuwa wabunifu, kupenda kazi, kuwa na mwenendo na maadili mema kama mfano kwa jamii. Wakulima , wafugaji na wavuvi wetu wataendelea kuwa maskini kwa sababu vijana wao baada ya kupata elimu yao ya vyeti wanakimbilia mjini, kutafuta kazi ya viyoyozi na kuvaa Suti. Hawataki kusikia tena habari ya kilimo wala ufungaji, kutwa nzima mitaondaoni na handfone masikioni. Bahati mbaya ajira zenyewe zimeota mbawa. Kizazi hiki kimekuwa kizazi cha hovyo sana kuwahi tokea.

Tanzania yangu jamani umerogwa na nani? Ngoja nishie hapo maana kadiri ninavyoandika machozi yananitoka. Magufuli Rais wangu pole sana. Naomba Mungu akujalie hekima uvumilivu na busara.

Boniphace .M. Pesambili.
 
Pamoja na kuandika mambo mengi mazuri ambayo ndio udhaifu wa nchi na wananchi wake, Lakini ningekuona wa maana kumshauri bw. mkubwa akawa na taasisi imara zenye nguvu za kujitegemea e.g. Katiba nzuri, Takukuru huru. Kwa sababu Maghufuli ni mwanaadamu kipindi chake kitaisha na atapita
 
observer1994.jpg

swissme
 
Kweli mkuu leo umeandika ukweli mtupu, waga nakupiga kwa hoja zako lakin hapa nimenyanyua mikono juu nimesalenda. We ni kichwa hatari daa!! Japo simpendi Magufuli na lichama lake lakni kiuhalisia ana kazi kubwa sana kuongoza kizazi hiki.
 
Nadhanani kama wanasiasa hawafai mbona ndo kawajaza huko kwenye vitengo nyeti
 
Limekuwa taifa la ajabu ajabu sana, viongozi wake (UKAWA & CCM)wamekuwa wanafiki, wazandiki, waongo hawaaminiki tena katika jamii. Wameruhusu kiburi na jeuri kuwavika kama mkufu shingoni mwao. Wana mawazo na mapenzi machafu mioyoni mwao. Kila kiongozi amekuwa muongo tu, kauli na videndo haviendani, ni wasaliti wa kwanza wa kauli zao wenyewe. Walimtangaza mchafu nchi nzima watanzania wakaamini hivyo gafla wakageuka tena kumtangaza msafi nchi nzima watanzania wakaamini tena hivyo bila kuwaoji kauli zao zile za mwanzo walizozisaliti wenyewe. Nchi imekuwa ya wanafiki sana hii. Tumekuwa jamii ya watu wa ajabu sana, tumebaki kuangalia mambo juu juu tu, na kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu , jamii iliyojaa wapuuzi na wanafiki wengi.

Hivi teuzi bado zipo?
 
Tatizo NI hiki kizazi cha Viroba
Nakuambia nitatizo,
Kutwa siasa kazi hapana.
Siasa zenyewe hawajui kufuata mkumbo tu.
Tatizo lingine
Kuachia watu Elimu ndogo kuongoza Vyama vilivyo zungukwa na wenye Elimu kubwa pia NI tatizo.

Magu kaonyesha anaingia JF
Tunaomba aongeze kubana zaidi

Bila hivyo mambo yatakuwa mabaya
 
Tatizo la Taifa letu ni kutopenda kujituma, kufanya kazi, kupenda short cut, Haya ndio yanayoleta umasikini, umasikini uleta kukata tamaa, kukata tamaa ndio chanzo cha mabaya yote uliyoandika (chuki, uongo, wivu, usagaji, bange, kukaa tu, kutokutumia muda sawa sawa nk)
 
Limekuwa taifa la viroba, bange, mizinga. Mpaka viongozi walevi wakati wa majukum ya kazi mfano huyo waziri aliyetunbuliwa. Yaan nchi ya vituko hii. Mungu tusaidie tu
 
Magufuli tunakuunga mkono baba, watu walizoea vya bwerere. Fe fikiria mtu hajasoma lakini ana wadhifa serikalini, waliosoma walionekana wajinga. Wajanja wanabangaiza tu na kujipatia mishahara serikalini huku wakichekewa na kuambiwa fursa kwa kila Mkwere/Mtanzania, for what wakati haujasoma kihivyo? Pale Ikulu ilikuwa ni sehemu ya dili, watu wanahonga pesa wapatiwe kuongoza almashauri ili waiibie serikali na yule jamaa mtalii alijuwa lakini alikuwa anacheka tu. Kwa sasa vihiyo wanatumbuliwa eti wanalia na kumkejeli rais kuwa ni dikteta, really? Yaani hujasoma na hauna ujuzi wowote ule unataka ulipwe tu na serikali? To hell.
 
Tatizo NI hiki kizazi cha Viroba
Nakuambia nitatizo,
Kutwa siasa kazi hapana.
Siasa zenyewe hawajui kufuata mkumbo tu.
Tatizo lingine
Kuachia watu Elimu ndogo kuongoza Vyama vilivyo zungukwa na wenye Elimu kubwa pia NI tatizo.

Magu kaonyesha anaingia JF
Tunaomba aongeze kubana zaidi

Bila hivyo mambo yatakuwa mabaya

'Kikazi cha viroba'. Hapo sasa unatafuta ugomvi na Wachaga.
 
Mtoa mada nakupongeza kwa dhati kabisa, kwani kwa asilimia kubwa upo sahihi kabisa. Nchi hii watu wengi wanataka mambo makubwa na ya kifahari huku wakiwa wamekaa tu bila hata kujishughulisha kwa namna yoyote ile. Ni watu wenye kuilalamikia serikali kwa kila jambo bila aibu. Ni kizazi kilichokosa uvumilivu na kisichojituma. Ili kubadili hali na mtazamo wa watu wa nchi hii ili wawe wachapakazi ilikuwa ni kumweka madarakani RAIS ambaye ni KOMANDOO, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na viongozi wote wa ngazi mbalimbali wawe ni wanajeshi na nchi iongozwe kijeshi japo kwa miaka michache tu. Kwa kufanya hivyo bila shaka nchi ingeweza kupiga hatua za maendeleo siku hadi siku. MHESHIMIWA RAIS MAGUFULI, MUNGU AKUONGOZE, AKULINDE, AKUTIE NGUVU, AKUPE HEKIMA, BUSARA NA UJASIRI ili uweze kuliokoa taifa hili katika janga la umaskini, uvivu, ufisadi, wizi, uzembe, ubinafsi nk.
 
Kuongoza nchi ni kazi rahisi sana,kiongozi anatakiwa kutengeneza mfumo utakaongoza nchi. Kuwe na mahakama huru,bunge huru,polisi huru. Yoyote atakaevunja sheria atahukumiwa kutokana kosa lake. Sasa kiongozi akijipapambanua kuwa yeye ndio kila kitu na siku akitoka kwenye uongozi tutarudi kulekule tulikotoka.
Ningempa pongezi kama angetengeneza mfumo usiomzunguka yeye bali uzunguke katiba na sheria.
 
Naililia nchi yangu Tanzania , kila nikitafakari machozi yananitoka nakosa majibu nabaki kujiuliza tutafika kweli? Magufuli kazi unayo sana kuongoza kizazi hiki cha ****** pole sana!

Limekuwa taifa la ajabu ajabu sana, viongozi wake (UKAWA & CCM)wamekuwa wanafiki, wazandiki, waongo hawaaminiki tena katika jamii. Wameruhusu kiburi na jeuri kuwavika kama mkufu shingoni mwao. Wana mawazo na mapenzi machafu mioyoni mwao. Kila kiongozi amekuwa muongo tu, kauli na videndo haviendani, ni wasaliti wa kwanza wa kauli zao wenyewe. Walimtangaza mchafu nchi nzima watanzania wakaamini hivyo gafla wakageuka tena kumtangaza msafi nchi nzima watanzania wakaamini tena hivyo bila kuwaoji kauli zao zile za mwanzo walizozisaliti wenyewe. Nchi imekuwa ya wanafiki sana hii. Tumekuwa jamii ya watu wa ajabu sana, tumebaki kuangalia mambo juu juu tu, na kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu , jamii iliyojaa wapuuzi na wanafiki wengi.

Kila kukicha upendo unapungua baina ya watanzania, visasi, dhuluma, wizi, ubakaji, ufedhuli, majivuno, matabaka, ukada na umasikini unazidi kutumaliza. Ee Mungu wetu tusaidia kizazi hiki cha ******. Tumebaki kuabudu watu weupe na vitu vyao na uchafu wao wote. Tumekubali kuporwa utu wetu na kufanywa vivuli vya wazungu kiasi cha kupoteza hata utamaduni wetu.

Tumekuwa na vijana na wasomi wa hovyohovyo, kushinda kwenye mitandao kuanzia asubuh mpaka jioni kuangalia vipicha vya uchi uchi na ngono( ponograph), Kutukanana na kupost vipicha vya kipuuzi kwenye mitandao. Vinguo vyao wanavyovaa vya ajabu visizo hata maadili. Wanapenda vimagazeti na vijarida vya ngono ngono tu. Mada za mapenzi na mambo ya kipuuzi yanapewa kipaumbele kuliko hata mambo ya kitaifa. Kwenda kulima na kufanya kazi hawataki, viwanda vitakuja kwa muujiza gani?

Magufuli Rais wangu pole sana kuongoza jamii ya mashoga na wasagaji, wavuta bange na madawa ya kulevya. Mandanguro kila kona yamejaa madada poa na makaka poa wanashindania wateja na bahati mbaya wateja wao wengi ni viongozi wetu hawahawa wanaopiga marufuku mchana usiku ndio wateja wao. Taifa lawanafiki sana hili.

Makanisa na misikitini kwetu kama kimbilio na msaada kwa matatizo haya lakini huko ndiko kuna balaa. Hii ya makanisa niache nitaleta mada yake baadae maana inahitaji hekima ya Mungu sana kuijadili. Tumekuwa na uelewa finyu hata katika masuala ya msingi yanayohusu taifa letu, uelewa finyu unatufanya turubuniwe kirahisi au tuelekeze nguvu zetu kwenye mambo ambayo yanaonekana katika nyuso zetu kama ndio utatuzi wa matatizo yetu kumbe ni upuuzi.

Tuna wasomi wengi lakini wameshindwa kujiamini na kujisimamia. Wamekuwa ndio chanzo cha matatizo yetu. Wameshindwa kabisa kujitambua, kudadisi, kujituma, kuwa wabunifu, kupenda kazi, kuwa na mwenendo na maadili mema kama mfano kwa jamii. Wakulima , wafugaji na wavuvi wetu wataendelea kuwa maskini kwa sababu vijana wao baada ya kupata elimu yao ya vyeti wanakimbilia mjini, kutafuta kazi ya viyoyozi na kuvaa Suti. Hawataki kusikia tena habari ya kilimo wala ufungaji, kutwa nzima mitaondaoni na handfone masikioni. Bahati mbaya ajira zenyewe zimeota mbawa. Kizazi hiki kimekuwa kizazi cha hovyo sana kuwahi tokea.

Tanzania yangu jamani umerogwa na nani? Ngoja nishie hapo maana kadiri ninavyoandika machozi yananitoka. Magufuli Rais wangu pole sana. Naomba Mungu akujalie hekima uvumilivu na busara.

Boniphace .M. Pesambili.
Leo umekuja vizuri, aksante!
 
KWA KUWA BIASHARA NI KUUZIANA NA KUNUNULIANA NA UKITAKA KULA LAZIMA UKUBALI KULIWA BASI SASA CHA KUFANYA KUANZIA SASA UKIENDA DUKANI DAI RISITI ASIPOKUPA RISITI UJUWE HIYO SIYO BIDHAA KWA MATUMIZI SALAMA YA BINADAMU
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom