WHITE HOUSE
Member
- May 8, 2016
- 22
- 20
Katika viongozi ninaowakubali duniani kwa Sasa sitosita kulitaja jina la Dr John Pombe Magufuli, ni kili katika uchaguzi Mkuu uliopita Magufuli hakubahatika kupata kura yangu huku nikijua asingeweza kubadili taswira ya viongozi kujilimbikizia mali, viongozi kutumia mamlaka yao kuwadharau wananchi na mengine mengi.
Sasa hivi nimeamini Rais Dr.Magufuli anaishi anachokisema, anatenda anachokiamini katika kuibadilisha Tanzania ya maendeleo.
Narudi katika point.
Tangu mwaka jana Rais Dr.Magufuli alipoingia tuu madarakani waziri wa habari alitoa taarifa kuanza kutoonyeshwa bunge live, sababu kubwa ilikua ni kubana matumizi, na baadae asasi huru ziliamua kutoa pesa zake ili kufadhili urushwaji wa bunge live kwa vyombo vitakavyokua tayari kulipiwa gharama hizo.
Lakini bado bunge na waziri mhusika likakataa kutoruhusu urushwaji wa bunge live huku wakija na sababu tofauti na ile iliyotolewa mwanzo na waziri wa habari, Muda huu wakaja na sababu ya eti ni kuwafanya Watanzania wafanye kazi hiyo mida ya bunge badala ya kuangalia bunge ili waendane na Falsafa ya Rais wetu na ikapita. Watu tukajiuliza kwanini wamebadilisha sababu baada ya hii asasi kuamua kugharamikia gharama ya matangazo ya bunge kama waziri alivyodai??
Hapa Kuna mchezo mchafu umendaliwa dhidi ya utawala wa Dr Magufuli pindi alipochaguliwa ambapo yeye hajaufahamu, huu mchezo umendaliwa na viongozi ndani ya chama ambao wanaamini kupitia Rais Dr. Magufuli basi biashara haramu ya kifisadi, madawa ya kulevya na kuingiza mizigo bila kulipa kodi hawataifanya, Sasa wanafanya hivi ili kumyumbisha ili aonekane hafai,
Sote tunajua moja ya kazi kubwa ya baraza la mawaziri ni kumshauri Rais Ila sio kila waziri ana nia njema ya kumshauri Rais. Naamini hili Wazo la kutorushwa Live bunge siyo la Dr Magufuli Ila kashauriwa, na huyu aliyemshauri basi Rais Hakujua nia kuu ilikua nini japo aliingia na gia ya kubana matumizi lakini yeye alijua dhahiri matokeo yake na mikakati yao ya kukuhujumu Rais itakamilika.
Kuhariri bunge ni lengo lililoandaliwa na wabaya wa Rais kupitia wabunge na mawaziri wapiga dili na ndio maana imekaliliwa mara kadhaa mawaziri wawili wamekua wakifanya vikao vya siri na wafanyabiashara wakubwa kwenye hotel Dodoma na hizi taarifa alizipata Rais.
Kuna video nyingi sana zitahaririwa na kufanyiwa edit ili Rais azione kumbe zinatengenezwa ili kumchanganya Rais na azifanyie kazi kumbe ni edit.
Siunge mkono waziri kunywa pombe na anastahiri kuwajibishwa Ila Kuna hujuma kubwa inafanywa dhidi ya Rais kwa kupitia bunge kuhaririwa.
Rais naikubali sana kazi yako na uko ndani ya mioyo ya Watanzania Ila kuwa makini na hili suara la bunge kuhaririwa, kuwa makini na huyu waziri aliyekushauri bunge lihaririwe nyuma ya pazia anajua anachokifanya, nyuma ya Huyu waziri aliyekushauri kuna movie inatengenezwa huku wewe ukiwa hauijui na baadae movie inaisha maadui wako wanashinda vita.