lingamba lidodi
JF-Expert Member
- Nov 15, 2018
- 964
- 1,137
Habari zenu wana jamvi! Mheshimiwa Rais, nchi hii toka Uhuru haikujengwa na Nyerere,Mwinyi,Mkapa na Kikwete peke yao. Ilijengwa na wananchi wote wakiongozwa na hao niliowataja hapo juu na Jwtz,jkt,Polisi,usalama wa taifa. Wahandisi,wakulima na wana habari,nk.
Hawa wana habari walitoa mchango mkubwa kuhabarisha uma juu ya mambo yanayoendelea ktk nchi yao. Walifanya uchunguzi na kufichua maovu mengi kwenye sekta binafsi hata serikalini.
Wakati mwingine wana habari waliwarahisishia polisi kujua uovu uko mahali gani,takukuru,hata usalama wa taifa pia.
Marais hawa pia walitumia vyambo hivi vya habari na wakaviamini. Wakati wako huu baada ya kuvifunika VYOMBO hivi, kuna uovu mwingi unatendeka lakini wewe hujui kwa kuwa umetegemea Polisi tu.
Watu wanaonewa na hao uliowateua na WENYE fedha bila wewe kujua, hata hao Polisi huonea watu na kubambikia kesi bila wewe kujua. Vyombo vya habari vilifichua mengi bila uwoga na serikali ilichukua hatua na haki ikatendeka au uovu kuondolewa.
Leo hii nchi inatafunwa kimya kimya,wanyonge wanaonewa hawana chombo cha kuwapalizia sauti. Baba!Polisi hawawezi peke yao,usalama nao hawawezi peke yao,nk Mwananchi ilikuwa akiona jambo mahali haliko sawa,akimueleza mwandishi wa habari akalifuatili na kuthibitisha,story ile kesho ikiwekwa gazetini, tayari uovu umefichuka serikali kupitia vyombo vyake inachukua hatua.
Nakushauri badirisha tena Sheria ya vyombo vya habari ili vikusaidie kufichua maovu kama kweli Nia yako ni kukomesha maovu ktk nchi yetu. NCHI HAIJENGWI NA MTU MMOJA BABA!!!!