Rais Magufuli: Kamata weka ndani

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,411
RAIS John Magufuli amewawataka Wakuu wa Mikoa nchini kukamata watendaji wa kata wanaowavuruga wananchi na kuwaweka ndani ili kuwatia adabu.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akiwaapisha viongozi hao Ikulu jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku mbili baada ya kuwateua.


“Nyinyi mna mamlaka ya kuwaweka ndani hata masaa 48, wawekeni ndani ili wajue mnatakiwa kuheshimiwa,”amesema Rais Magufuli.


Hata hivyo, ameonesha kukerwa na tabia ya vijana kutofanya kazi na badala yake kuwa mitaani wakicheza na kwamba, wakuu hao wa mikoa wasimamie hilo.


“Kwa kweli ni aibu kuona kijana saa mbili au tatu asubuhi anacheza PoolTable halafu wazee wanalima, kamata peleka kambini walime kwa nguvu,” amesema.


Pia Rais Magufuli amewataka kuwaondoa wafanyakazi hewa kwenye halmashauri zote nchini.


“Mmekula kiapo rasmi nawapa siku 15 kuanzia sasa kuhakikisha wafanyakazi hewa wanaondolewa serikalini mara moja.”

Chanzo: MwanaHalisi
 
Hakuna Good Governance kwenye huu Utawala

sharia ya kikoloni hii

“Nyinyi mna mamlaka ya kuwaweka ndani hata masaa 48, wawekeni ndani ili wajue mnatakiwa kuheshimiwa,”amesema Rais Magufuli.
 
Duuu haya ngoja tuendelee kuona tu kama tatizo ni kukamata tu nakuweka ndani
 
Hii sio kauli ya rais, maana hawa wanaofanya haya ni kutokana na kukosa ajira, anaposema wafanye kazi ziko wapi kazi za kufanya? Rais wakati anatafuta kuingia Ikulu aliahidi ajira kwa vijana hajaqapa ajira ila anaagiza wafanye kazi.... Ipi sasa??
Halafu kamata weka ndani 48hrs baada ya hapo nini kinaendelea?
Mh rais vile viapo ulivyo kuwa umakula majukwani viheshimu.
 
Sidhani kama mheshimiwa rais huwa anafikiria kabla ya kuongea.....nashindwa kusema kuwa anaropoka kwa kuwa nahisi nitamvunjia heshima raisi wangu.....lakini anaendana na sifa za mtu anayeongea bila ya kupima matokeo ya kauli zake.....na hii ni mbaya kwa nchi inayojiita kuwa ni ya kidemokrasia.......
 
Rais aliamuru wakamatwe Watendaji wanaowadharau wananchi ili wajue wananchi ni watu wa kuheshimiwa. Kama Viwanda vya uongo vinalipa basi muda huu mngekuwa Ikulu.
wewe ndio mwongo ...angalia video ya rais wakati anaongea
 
Hakuna Good Governance kwenye huu Utawala

sharia ya kikoloni hii

“Nyinyi mna mamlaka ya kuwaweka ndani hata masaa 48, wawekeni ndani ili wajue mnatakiwa kuheshimiwa,”amesema Rais Magufuli.
Twisting statements to fit your political whims will not work. Start afresh or you will marktime on the same sport till you become past tense.
 
Tatizo sio nani waheshimiwe Bali ni sheria inasemaje ??
Na ukiendekeza dhana
ya kuwaweka watu ndani kinyume cha Sheria 24 ?

Kisa ,
umewaambia wakafanye Kazi ambayo hawana wakakukatalia ni nini kitatokea ?? Sheria inakutaka MTU apelekwe kituoni kwa kosa linaloeleweka siyo haya yakutengeneza ,
Na ndani ya 24 apewe dhamana (kama anastahili)Na kupelekwa mahakamani (ndani ya SAA 24,)
Anaona ugumu gani kusema atapeleka bungeni mwswada wa kufanya mabadiliko ya

sheria ili kuruhusu watu kuwekwa "kizuizini"ndani kwa SAA 24

Hapa mbwembwe tu
 
Nathani UKAWA ujamuelewa rais, lakini sio mbaya kwani wengi wenu mnauwezo mdogo wa kutafsi maneno aliyotoa Rais. Amesema wakamatwe watu wanaofanya makosa, wakamatwe watu wanasiotaka kufanya kazi badala yake wanakwenda kucheza pool table asubuhi. Msisahau kumshukuru rais pale mambo yatakapokuwa manzuri. Kwani mpaka sasa hivi fukuza fukuza imeongeza ufanisi kwenye vitego vingi vya serikali.
 
Iweke hapa kama unayo watu washuhudie muongo ni nani! Rais aliwataka Ma RC kuwaweka ndani watendaji wanaonyanyasa Wananchi.

pia alisema vijana wasio na kazi wanaocheza pool table asubuhi wakamatwe wakalazimishwe kufanya kazi makambini.....hapo makambini alimaanisha jeshini au?
 
Back
Top Bottom