Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,706
- 149,945
Sitaki kuamini kama swala la kushusha mishahara ya vigogo serikali linawezekana kwani naona litakabiliwa na changamoto nyingi tu kama vile sheria za utumishi wa umma na pia wengi wao watakuwa wamechukua mikopo katika mabenki na Taasisi zingine za kifedha ambazo mtumishi huyu hulipa kulingana na mshahara wake kwa kuzingati kigezo cha 1/3 ya basi salary.
Anachoweza kufanya Magufuli na serikali yake kwa sasa ni labda kuandaa mikataba mipya ya ajira ambayo haitaruhusu mishahara ya aina hii kwa wale watakaokuja kuchukua nafasi za vigogo hawa wa sasa baada ya wao kustaafu,kuacha kazi,kufukuzwa kazi,n.k pamoja na kutowapa fursa ya wao kuongezewa mishahara kitu ambacho kitawafanya wengi wao waache kazi na kutafuta ajira kwenye mashirika makubwa ya kimataifa au NGO's.
Sasa tuachene na hilo swala la kupunguza mishahara na tuzungumzie hili swala la perdiem.Hili swala la posho za perdiem ndio la hovyo kupindukia serikalini na ninaweza kusema ni la kibaguzi kabisa.
Hivi kuna ulazima gani wa kuweka viwango vikubwa vya tofauti vya posho ya safari baina ya Waziri, Katibu wa Wizara,Mkurugenzi wa Shirika, Manager katika shirika hilo,n.k wakati wote wanakwenda nchi moja au mkoa mmoja?Hotel anayolala manager(tena nzuri ti) inakuwaje katibu Mkuu wa Wizara ashindwe kulala?Isitoshe, wengine hata mahotelini hawalali bali wanalala kwa ndugu zao au kwenye majumba yao.
Raisi kama ni kutafuta usawa,basi anza ni hili la kulipana per diem kwa kuangali vyeo/sclale za mishahara ili hali wote mnaenda safari moja. Lipeni flat rate kuanzia Waziri, Mbunge, Mkurugenzi,Manager,n.k.Anaetaka makuu ajigharamie mwenyewe kwa kuongeza hela kutoka mfukoni mwake.
Napendekeza hili liende sambamba na kupiga marufuku watumishi wa umma kusafiri na ndege katika daraja la "business class" na badala yake watumie "economy class",asietaka aachie ngazi.
Starehe kama hizi fanya kwa pesa yako na si kwa kodi za wananchi masikini wa nchi hii.