Rais Magufuli, kama kweli si Dikteta, wakemee Polisi wasikuchonganishe na Wananchi

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,863
3,851
Kuna uwezekano mkubwa sana wa Serikali ya Magufuli kuchukiwa na wananchi, hasa kwa vitendo vya Polisi kuwa na viwango viwili (double standards) katika kulinda Usalama wa Raia na Mali zao.

Polisi wanadhibiti Vyama Vya Upinzani kufanya shughuli zao ili hali wakati huohuo wanaachia Chama Cha Majipu (CCM) kikiendelea na Shughuli zake kwa mtindo ule ule unakatazwa na Polisi.

Mifano:
Polisi walizuia Ukawa wasikusanyike huku wakimuacha Mwigulu Nchemba akiikusanya wana CCM kule Singida.

Polisi walizuia Maandamano ya Ukawa wakati huohuo wakiachia maandamano ya CCM kule Mwanza.

Polisi wamesambaratisha Mahafali ya Chaso (Wanafunzi Chadema Vyuo Vikuu) wakati huo huo wakiachia wale wa CCM wakiendelea na mahafali ya aina ile ile yaendelee kule Iringa.

Hii sio sawa. Na kama kweli Magufuli kama Amri Jeshi Mkuu, sio Dikteta basi akemee hali hii.
 
Back
Top Bottom