Rais Magufuli: I wish I could be IGP; Ni kuhusu wale wanakwaya pale central

Emc2

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,808
16,834
Sikiliza agizo hapa kwa wale walioenda kuimba central

image.jpeg

Inaonyesha kila kinachoendelea huwa kinamfikia Rais Magufuli ambapo leo kwenye hotuba yake IKULU Dar es salaam ameongea kuhusu wale Mashabiki wa Yanga walioonekana kulifutafuta vumbi gari la Mfanyabiashara Yusuph Manji baada ya kuingia kuhojiwa Polisi kwenye sakata la dawa za kulevya.
image.jpeg

Pamoja na hilo, rais pia ameongelea ishu ya Wanakwaya wa Askofu Gwajima kwenda na kusimama nje ya kituo cha kati cha Polisi baada ya Askofu huyo kuingia kuhojiwa na Polisi kwenye sakata la dawa za kulevya.


Hotuba kamili hii hapa chini

 
Huyu ndiye Amiri Jeshi Mkuu...watu wako serious unaitwa unakwenda na dharau kisa eti kwakuwa umeitwa na kijana Makonda...

Huyo kijana ni Mamlaka (Regional Commissioner). Unaitwa na wewe unaita vyombo vya habari unatoa tamko...dharau hizi.
 
Yaani anavyowapa kichwa subiri uone kinachofuata, watapiga watu ovyo ovyo, nani hajui polisi wanapeleka form four failures ambao hata sheria hawaijui. Ni wazi kabisa mkubwa anatangaza vita. Hakuna uhuru tena Tanzania, nilitegemea atachukua hatua kwa kukurupuka kwa kondakta, ila naona anatoa full support. We can't expect anything better, ndiyo nature yake ilivyo, ubabe ubabe. Uraia wa US ukipita aisee bongo kwa heri, sio rahisi kudeal na mambo haya. Wanachekacheka ila jamaa hacheki, yupo serious kabisa.

Ambaye anafurahia haya asubiri siku zamu yake ikifika, ndio tatizo la mambo kama haya mara nyingi badala ya kugusa wenye hatia yanagusa watu innocent. Endeleeni kucheka, zamu yenu bado. Mtu kusafisha gari awekwe ndani kwa sheria ipi? Nyerere angekua anayaona haya angetoa machozi kabisa.

Tanzania aliyebaki na busara sasa hivi ni Waziri Mkuu tu, ametulia ila anafanya kazi kwa akili sana, hataki kiki na wala hana presha za kuvunja sheria.
 
Jamaa ni muoga sana huyu. Anaonekana anawaogopa sana 'wakubwa', maana kila hotuba yake haishi kuwataja wakubwa.
Hata nguvu inayotumika kuwadhibiti na kuwashughulikia watu ni zile nguvu za mtu mwoga baada ya kukimbia na kufanikiwa kufika kwenye kifusi cha mawe/kokoto (majeshi), anaona ni muda wa kujilinda na kujibu mashambulizi. Hivyo ndivyo nimuonavyo mkuu wangu.
 
Back
Top Bottom