Uchaguzi 2020 Rais Magufuli hutaki 'matusi' yapi katika kampeni?

mtz one

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
4,272
1,210
Si mara moja au mbili namsikia rais Magufuli akikazia kuwa hataki matusi wakati wa kampeni. Nilimsikia wakati anavunja bunge nimemsikia tena leo pale Somanga akiwa njiani kurudi Dar. Magufuli amekazia sana eneo hilo kuwa hataki matusi watu wanadi sera zao.

Ni matusi gani Magufuli anayaogopa? Yale ya akina Lusinde na Msukuma au yapi? 2015 ulikua ni mwaka ambao hakuna tusi tusilolisikia kutoka kwa wanadi sera wa CCM na hatukuwahi kumsikia Magufuli akiyakataza zaidi ya kuchekelea na kufurahi.

Sasa kupitia safu hii ningependa kujua Matusi yapi ambayo hataki kuyasikia na anayaogopa? Tafsiri zipi tutumie ili tusijejikuta mikononi mwa dola kama ulivyosema? Matusi yapi hasa hayataki mwanasiasa wetu Magufuli? Matusi gani unayaogopa na hasa yakutoka kwa nani mheshimiwa sana?
 
Huyu ashaona kwamba hana ujanja wa kuzuia kusemwa kama wakati ule anaringa na dola mikononi mwake sasa anaona anakwenda kushindana na watu ambao ili washinde lazima wamseme na yeye kwa madhaifu yake hakuna jingine.
 
Haya kwake ndo matusi?
 
hivi hii tume ya Magufuli au Msajili wa vyama kwa nini hawamuonyi wakati mngombea mmoja wapo anataka watu wakatangze sera zao anazotaka yeye huyu vipi mbona anajisahau sana
 
Mfano wa matuc ni kama haya: CHADEMA wakiiona CCM mavi yanagonga chuppi.. Badala yake unaweza tumia lugha ya staha.. CCM ni tishio kwa CHADEMA kwa kuwa imeyatekeleza hata yale waliyokuwa wanapigia kelele!
 
Wapinzani wana hamu sana ya kumtusi Rais mtaipata tamko ni sheria

Ahaaaa ahaaaa, tafsiri ya matusi anayo mgombea wa chama tawala, na hataki matusi kutoka kwa wengine. Kibaya zaidi, matusi kwake ni kuambiwa ukweli unaomuuma.
 
Si mara moja au mbili namsikia rais Magufuli akikazia kuwa hataki matusi wakati wa kampeni. Nilimsikia wakati anavunja bunge nimemsikia tena leo pale Somanga akiwa njiani kurudi Dar. Magufuli amekazia sana eneo hilo kuwa hataki matusi watu wanadi sera zao.

Ni matusi gani Magufuli anayaogopa? Yale ya akina Lusinde na Msukuma au yapi? 2015 ulikua ni mwaka ambao hakuna tusi tusilolisikia kutoka kwa wanadi sera wa CCM na hatukuwahi kumsikia Magufuli akiyakataza zaidi ya kuchekelea na kufurahi.

Sasa kupitia safu hii ningependa kujua Matusi yapi ambayo hataki kuyasikia na anayaogopa? Tafsiri zipi tutumie ili tusijejikuta mikononi mwa dola kama ulivyosema? Matusi yapi hasa hayataki mwanasiasa wetu Magufuli? Matusi gani unayaogopa na hasa yakutoka kwa nani mheshimiwa sana?
Ni ile suti.
 
Ukipanda jukwaani ukasema lissu kajinyea stendi au mgombea yeyote asiye wa ccm hilo sio tusi tuliambiwa na andunje ndugali hiyo inaitwa kuchomekea, ila ukipanda jukwaani ukasema CAG aligundua ufisadi wa tilioni 1.5 hilo ni tusi kubwa adhabu yake unastahili kutekwa na ikiwezekana kuuwawa kabisa!
 
Back
Top Bottom