Rais Magufuli: Hongera Kafulila kwa uzalendo dhidi ya IPTL. Waliokuita tumbili wao ndio matumbili

Huu ni unafiki mwingine wa dikteta uchwara. Kama wakati ule Wabunge wa wapinzani wasingekuwa na uhuru ndani ya Bunge kama ilivyo leo hii kwa uhuru wao kuminywa spika na naibu wake kwa kunyimwa muda wa kuzungumza kuambiwa wabadili kile wanachotaka kuzungumza basi hili la wizi wa pesa za Escrow lisingejulikana na hivyo kala singa na Ruge leo hii wangekuwa ni watu huru.

Wabunge wa upinzani wapewe nafasi yao inayostahili kule Bungeni ili wafichue maovu mbali mbali ambayo bado yapo tele kwenye hii Serikali dhalimu. Bunge liheshimiwe, katiba iheshimiwe na sheria za nchi pia ziheshimiwe.


Mh Rais Magufuli akiwa ziarani Kigoma, Uvinza amezidi kusisitiza kuwa hii vita dhidi ya mafisadi na wale wote wanaotumia madaraka yao kujinufaisha wenyewe haitamuacha mtu.

Akimpongeza Kafulila kwa kuwa mzalendo wa kweli kwa kuwapigania watanzania kuhusu IPTL hadi akaitwa tumbili,akifunguliwa na kesi n.k. Amesema waliomuita tumbili wao ndiyo matumbili.

Amesisitiza pia kuachana na siasa za uvyama badala yake tuhimize maendeleo.

My take:
Kwa ujumbe huu wa leo, ni kiashiria kibaya kwa waliodhani Rais anazuga tu.
 
Mi nilichojifunza, mchochezi wa leo ni mzalendo wa kesho kwa matokeo yaleyale ya kipimo cha mkojo. Wakati wa awamu ya 4 Tumbili alipimwa mkojo akadhihirika kabisa kuwa ni mchochezi. Akafunguliwa na kesi kabisa. Leo hii, kwa matokeo yaleyale ya kipimo cha mkojo, mchochezi yule anamwagiwa sifa ya ajabu ya uzalendo, Wakati wale wasimamizi wa sheria za uchochezi wa wakati ule sasa wamegeuka kuwaTumbili! Yaani hii ni ngumu kumeza.
 
I have been greatly touched by the President's speech. I am more convinced than ever before that the man is good. Very good! May God bless him.

Hizo tozo alizotangaza zimefutwa ni muhimu sana pia. Viko vimangi-meza vingi ambavyo vimekuwa vikinyonya na kukandamiza wakulima kwa hizi tozo.

Hapa kazi tu! Go Magu, go! We are with you. We are proud to have you as our President.
 
Mbona hakusimama bungeni kutoa pongezi zake kwa Kafululila? aliogopa nini? Unafiki uliokithiri.
 
sizonje hana lolote , anachofanya ni kuangalia upepo wa kisiasa unapovuma na yeye anajielekeza huko huko (kick kwa pikipiki).

Unafiki unakiua Chama Cha Makinikia. time will tell.
 
Unajiaje kama hakusimama?. Kafulila hivi karibuni amesema kwamba kwenye suala la escrow aliungwa na mkono na mawaziri watano akiwemo Magufuli.

Hakusimama hadharani. Mbona Kafulila yeye aliongea hadharani? Hsyo ya chini chini ndio huwa tunaita ni majungu. Kama aliona ukweli wa jambo husika aliogopa nini kutoka hadharani? Kwa hili asitafute point za mezani, akiri hakutimiza wajibu wake ipasavyo ili kulinda tumbo lake.
 
"Tuachane na siasa za vyama " .....mara "mlikosea kuwachagua upinzani ,maendeleo huletwa na CCM".

Tushike lipi tuache lipi?
 
Hakusimama hadharani. Mbona Kafulila yeye aliongea hadharani? Hsyo ya chini chini ndio huwa tunaita ni majungu. Kama aliona ukweli wa jambo husika aliogopa nini kutoka hadharani? Kwa hili asitafute point za mezani, akiri hakutimiza wajibu wake ipasavyo ili kulinda tumbo lake.
Kafulila alisema walikuwa ni mawaziri watano, mbona huongelei hao mawaziri wengine wanne?.

Acheni kuongelea kila jambo katika mtazamo wa kimtaanimtaani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom