Mpunilevel
JF-Expert Member
- Sep 14, 2015
- 3,140
- 1,871
Ndugu Rais Magufuli baada ya kuanza kudhibiti mianya inayoliteketeza taifa, mahasimu wako wa kisiasa walitaka kukuchonganisha na nchi wahisani ili ukwame katika majukumu yako ya kuiletea Tanzania maendeleo.
Utakumbuka ule msaada wa MCC. baada ya kusitshwa jamaa hawa walipiga vigelegele sana wakiamini utakwama. Lakini ulisimama imara na makusanyo ya kodi yaliyotukuka bila kulalamikia msaada huo.
Jambo la pili ninalokumbuka ni uchaguzi wa zanzibar, nao pia walitaka kutumia kama karata ya kukukwamisha lakini ilishindikana.
Pia Kuna jambo lilizuka kwamba huhitaji wawekezaji nchini, ambavyo si kweli bali ulihitaji uwekekezaji wenye tija kwa taifa kwa wawekezaji kulipa kodi stahiki.
Vihunzi vyote hivi vya kuhusiana na nchi wahisani naona kama vile umeanza kuviluka.
Leo Watanzania tumeshuhudia umekutana na barozi mbali mbali kwa ajili ya uwekezaji mkubwa hapa nchini mwetu. Hongera sana Rais.
Mataifa yaliyokua yanapandwa chuki dhidi yako wameanza kukuelewa vizuri nini unahitaji kwa Tanzania yetu, hii ni ishala nzuri kwa mafanikio ya utawala wako.
Mahasimu wako baada ya kuona wazungu wamewapuuza, wamehamehamishia vita hiyo ndani ya nchi kuhakikisha unakwama kuendesha nchi kwa ufanisi.
Propaganda nyingi kwa kutumia baadhi ya vyombo vya habari kuuaminisha umma wa Watanzania kwamba wewe si chochote huku mioyoni mwao wakitambua wewe ni tishio kwao.
Hili nalo naamini watashindwa tu.
Ndugu Rais mamlaka uliyonayo kikatiba ni makubwa sana. Kikundi hichi cha wachache waliozoea vya kunyonga na hakika utakisambaratisha kwa mujibu wa sheria za nchi.
Mungu ibariki Tanzania.