VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,904
Tumekuchagua kiserikali na kichama. Tumekuchagua kuwa Rais wetu wa Tanzania na pia kuwa Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa. Tulikuchagua utuongoze. Kama watanzania,tuna mawazo,fikra,ubunifu na malengo ya kuleta tija kitaifa. Tukahitaji kiongozi mkuu na tukakupata.
Tulipokuchagua,hatukukuchagua ututishe kwa maneno au vitendo. Umekuwa ukitutisha kimaneno na kivitendo kiserikali na kichama. Umekuwa ukitumia mwamvuli wa 'kusema ukweli'. Ukweli si vitisho. Ukweli ni mkusanyiko wa hoja za haja zinazojadiliwa na kukubaliwa.
Sina tatizo na lengo lako la kuinyoosha nchi. Lakini,nchi haiwezi kunyooshwa kwa mikwara,kejeli na 'mkono wa chuma' wa kiongozi mmoja. Haitawekwa sawa kwa kukataza kila jambo; kupiga mkwara kila mtumishi au kada na kutaka mawazo yako tu yatawale. Dawa ni kuimarisha idara na vyombo vya utendaji na kuviacha vitende
Dawa ni kuiacha demokrasia imee,itendeke na isaidie katika kuikosoa Serikali kwa mambo ya kitaifa. Muda mwingine,kuyazuia maji yateremkayo si suluhisho la mwisho. Kuzuia kunaweza kuzua kizaazaa. Watumishi na makada wanahitaji faraja,hoja na tija. Tafadhali tuongoze,usitutawale!
Mwafaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha kumchagua Lissu kuwa Rais wa TLS)