Rais Magufuli hakikisha, anayekuja hatorudi Dar!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,612
2,000
Waswahili tunapenda sana mteremko na kazi ngumu hatutaki, tunapenda vilivyojengwa na wengine, ndo maana wanataka kung'ang'ania Dar ambayo tayari ilishajengwa kwa sehemu kubwa na Muzungu, Waarabu na Wahindi, sasa Waswahili tunajenga Mji wetu wenyewe Dodoma, wavivu wameshaanza kuchonga midomo!

Hivyo Raisi wangu Magufuli nafikiri tayari umeshatufahamu, hivyo kama ulivyofanya kwenye fao la kujitoa hakikisha pia hapa kwenye kuhamia Dodoma mpaka inapofika 2025 umeshafika mbali kiasi kwamba mvivu atakayekuja 2025 ambaye najua atataka arudi Dar ashindwe pa kuanzia, hiyo ndo dawa ya Mswahili mvivu!
Kwenye fao la kujitoa bila ya wewe hakuna ambaye angeweza kufanya uamuzi mgumu na muhimu kama ule, na mpaka 2025 hata akija mvivu hawezi kurudisha fao la kujitoa kwani itakuwa chaos na haitawezekana tena, hivyo na Dodoma fanya hivyo hivyo vinginevyo huyo Mji hakuna mvivu atayehamia, bila ya wewe kuwa ngangari, najua unaweza raisi wangu!

Mimi Askari wako!
 
Mwanamalundi

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,124

Kuhamia dodoma ni kwa mujibu wa sheria iliyopitishwa na bunge. Sasa kama kuna "mswahili mvivu" mmoja atataka kurudi dar es salaam huko siku za usoni, basi "mswahili mvivu" huyo hana budi kurudi bungeni tena ili kubadilisha sheria.
 
popoma

JF-Expert Member
May 5, 2017
2,380
2,000
Uchumi unaporomoka endeleeni na propaganda zenu kwa kuwa ndiyo kazi inayowaweka mjini
 
maringeni

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
3,205
2,000
We jamaa mbona umekaa kiutatanishi? Mtu harudi vipi? Afie Dodoma? Akiwa likizo je? Weekend na sikukuu?
Elewa kuwa dodoma bado pori kwa waliozoea dar. Maji ya bahari lazima mkuu !!

Punguza jazba na kujipendekeza. Haya ni maisha tuu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom