Ciprofloxacin.
JF-Expert Member
- Apr 15, 2015
- 1,583
- 2,697
Sina uwezo wa kukuona ana Kwa ana mh rais, ujambazi sasa umekuwa zaidi ya jipu tangu umeingia madarakani, ni kama vile kuna kundi kubwa la watu wazito na wenye uwezo mkubwa ambao wamepanga kuihujumu serikali yako ionekane si lolote si chochote.
Maana haiwezekani kila kukicha story ni majambazi yameua na kupora, hii ni dharau kubwa Sana Kwa serikali yako, wanafanya uhalifu utadhani taifa halina serikali au lina serikali legelege.
Nakuomba ufanye haya na ujambazi utakuwa historia Tanzania.
Waite ofisini kwako ikulu, Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya usalama wa taifa TISS, IGP, na DCI, kisha uwape amri ya kwamba, ndani ya siku 30 usingependa kusikia ujambazi sehemu yoyote Tanzania na endapo itatokea basi wao ndo watawajibika.
Mh rais, nakuhakikishia kabisa kuwa hakuna jambazi atakayetamba, maana hawa wana mbinu zote za Ki intelijensia za kupambana na uhalifu na Badala yake wanapambana na uhalifu sugu kimazoea Sana ndo maana ujambazi hauishi. bila hivyo majambazi yatatumaliza si mchezo.
Hata Kama hutasoma wewe mh rais hii habari nina imani utaambiwa na wasaidizi wako na ndo mwisho wa ujambazi utakuwa umefika.
Nawasilisha.