Rais Magufuli ebu iokoe CCM kwa kuwapatia wana Bukoba meli mpya

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
122,490
96,054
Wanajamvi,

Kama itakumbukwa kuwa wakaazi wa mkoa wa Kagera wanategemea sana usafiri wa njia ya meli ktk kusafirisha mizigo kwenda na kutoka ktk mkoa wa Mwanza,mara tu baada ya meli yao ya MV Bukoba kupata ajali ya kuzama walibakiwa na MV Victoria na MV Serengeti na meli ambazo pia kwa sasa zipo hoi bin taaban hivyo kuufanya mkoa wa Kagera kubakia bila ya usafiri wa meli.

Tunakumbuka ahadi za JK mwaka 2005 kuwa angewanunulia wana Kagera meli kubwa na mpya mwaka huo hadi 2010 hakuna kilichotekelezeka.

Akaja Magufuli na Kinana mwaka 2010 wakatoa ahadi ya kuwapatia meli mpya lkn hadi hivi sasa wana Kagera wanaendelea kuzisoma ahadi hizo kwenye magazeti.

Tunakuomba Rais Magufuli iokoe CCM kwa kuwapatia meli watu wa Kagera na mikoa ya jirani vinginevyo 2020 CCM mtashikana uchawi.
 
We mtu tangu nchi inapata Uhuru hadi Leo bado anakosa maji safi na salama lakini bado anaendelea kuichagua ccm sembuse hao hawana meli tu..wataichagua tu hata wasipopelekewa hiyo meli..watanzania sijui walilishwa nini??
 
Mkuu kwa wahaya hasa hawa wa dot com ccm mwaka 2020 wataisoma namba kama hawatatekelezewa hiyo ahadi ngumu
1464666173356.jpg
 
Achaneni na mambo ya kuomba meli kubwa ambazo zinatumia masaa 9-12 kwa safari ya masaa 2-3. Kwa nini msiwaombe akina AZAM walete boti za speed kubwa? Hii ni karne ya 21.
 
Achaneni na mambo ya kuomba meli kubwa ambazo zinatumia masaa 9-12 kwa safari ya masaa 2-3. Kwa nini msiwaombe akina AZAM walete boti za speed kubwa? Hii ni karne ya 21.
Mkuu naona wewe upo sudan ya kusini kusiko na Mawasiliano ya kutosha,hizo meli zilishapelekwa na zikafeli
 
Yule alosema watanzania ni maiti zinazitembea kwan alikosea?
Alitukana kutumia Watanzania. Lakini angesema wanachadema angekuwa amepatia. Vipo viashiria vya kuthibitisha hilo. Mojawapo ya uthibitisho huo ni kwamba wanachadema hawatumii ubongo wao kufikiri bali hutumia uti wa mgongo kutenda yale yaliyofikiriwa na wengine. Ndio maana kila siku utasikia wakigeuka geuka mara tubane matumizi, ukibana matumizi, hela hakuna. Rais anasafiri sana nje. Akiacha kusafi rais anajifungia. Haya machache yatoshe kukuthibitishia kuwa wanachama wa Chadema ni maiti wanaotembea na si Watanzania.
 
Yaani kwa akili yako unafikiri Tanzania tunashindww kununua meli mpya?
Ok kama mnaweza kununua meli mpya mnashindwa nini kutekeleza ahadi zenu kwa hao wana kagera na huu ni mwaka wa 10 mnaingia kwa gia za kuwanunulia hiyo meli?
 
Alitukana kutumia Watanzania. Lakini angesema wanachadema angekuwa amepatia. Vipo viashiria vya kuthibitisha hilo. Mojawapo ya uthibitisho huo ni kwamba wanachadema hawatumii ubongo wao kufikiri bali hutumia uti wa mgongo kutenda yale yaliyofikiriwa na wengine. Ndio maana kila siku utasikia wakigeuka geuka mara tubane matumizi, ukibana matumizi, hela hakuna. Rais anasafiri sana nje. Akiacha kusafi rais anajifungia. Haya machache yatoshe kukuthibitishia kuwa wanachama wa Chadema ni maiti wanaotembea na si Watanzania.
Maiti anaye tembea ni wewe na hao maiti wenzako msiyo jifahamu na cdm itabakia kuwa kiboko ya maccm
 
Back
Top Bottom