Rais Magufuli, Dhihaka dhidi ya mbunge wa Serengeti, Marwa Ryoba hazikubaliki

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Inawezekana ni kweli kwamba ukiwa Rais, kwa taswira ya haraka kwa watanzania wengi, unapaswa kupewa taswira ya 'ufalme' na kamwe usikosolewe au kupingwa hadharani kwa baadhi ya mambo. Ni marufuku kukosolewa.

Tunaishi katika taifa ambalo watu wake wanadhani ni sahihi kwa kiongozi mkuu wa nchi kudhihaki viongozi wengine ambao wamechaguliwa na wananchi kww kupigiwa kura nyingi katika maeneo yao.

Tunaishi katika zama ambazo wananchi wanadhani kauli ya Rais ni 'final say' na hakuna ambaye anaweza kujadili katika nchi yenye Mfumo wa vyama vingi vya siasa, nchi ya kidemokrasia.

Lakini katiba ya Tanzania ibara ya Haki ya Uhuru wa Mawazo Uhuru wa Maoni Sheria ya 1984 Na.15 ib.6
18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

Hata hivyo kwa kuongeza tu, sheria yetu ya vyombo vya habari ya mwaka 2016, ime-retain vifungu vya iliyokuwa sheria ya Magazeti ya 1976, inaeleza wazi kwamba; halitakuwa kosa la uchochezi kwa mtu yoyote kutoa au kuchapisha maneno kwa lengo la kupinga na kukosoa serikali au sera zake au mipango yake.

Leo, najitokeza mbele yenu, kama Mtanzania ambaye naipenda nchi yangu, naheshimi tawala zake, naishi katika misingi ya sheria na pia napenda kuona watawala wakiwapa heshima wananchi na maamuzi yao, waheshimu matakwa ya wananchi.

Mheshimiwa Rais, John Pombe Magufuli, katiba na sheria za nchi yetu zimetoa ruhusa kwa kiongozi yoyote, wa cheo chochote kukosolewa na kupingwa hadharani.

Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limegawanyika katika maeneo mawili. Governing Party na Official opposition. Ukiondoa upande wa serikali ambao unawakilishwa na mawaziri.

Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani yake kuna kambi rasmi ya upinzani bungeni ambayo inaongozwa na KUB—Kiongozi wa upinzani bungeni, ambaye kwa 'hadhi' yake ni sawa kabisa na 'waziri mkuu' ndani ya bunge.

Kambi rasmi ya upinzani bungeni imepewa mamlaka na Kanuni za kudumu za bunge kuunda wizara mbadala kwa kila wizara. Kuteua mawaziri mbadala kwa kila wizara. Ndio maana baada ya Rais kutangaza baraza lake, KUB anatangaza lake pia.

Kazi ya hizi wizara mbadala bungeni ni kuleta maoni na bajeti mbadala. Kushauri, kupinga na kukosoa ni sehemu ya wajibu wa wizara mbadala. Si kosa ndani ya bunge. Bunge sio sehemu ya serikali.

Wabunge wa upinzani, wabunge wa chama kinachoongoza serikali wanao uwezo wa kukosoa, kupinga au kukubali Hoja za serikali ambazo zinawasilishwa ndani ya bunge. Sio lazima, wabunge wakubaliane na kila kitu kinachowasilishwa ndani ya bunge. Bunge sio 'executive Rubber stamp'

Wabunge wa upinzani, kambi rasmi ya upinzani bungeni ipo kwa mujibu wa Kanuni za kudumu za bunge (parliamentary standing orders of the national assembly of the United republic of Tanzania), Kanuni hizi ndio huongoza bunge kwa wakati wote.

Kanuni za kudumu za bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (parliamentary standing orders of the national assembly of Tanzania) Toleo la Januari 2016 limeeleza vyema sana kuhusu Kiongozi wa shughuli za serikali na upinzani bungeni.

Kifungu cha 10. Waziri Mkuu atakuwa ndiye Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni. Kama Waziri Mkuu hataweza kuwepo Bungeni kwa kipindi kinachozidi siku moja, atamteua Waziri mwingine kuwa Kiongozi wa muda wa Shughuli za Serikali Bungeni. Katika kufanya uteuzi huo, Waziri Mkuu atazingatia ukubwa kazini wa Mawaziri waliopo.

Kifungu cha 11(1) Kiongozi wa Upinzani Bungeni atachaguliwa kwa kufuata utaratibu ulioelezwa katika fasili za Kanuni hizi zinazofuata. Kiongozi wa (2) Chama chochote hakitakuwa na haki ya kuchagua Kiongozi
wa Upinzani Bungeni, mpaka kiwe kina idadi ya Wabunge wasiopungua thelathini. Upinzani Bungeni

(3) Endapo kutakuwa na Vyama zaidi ya kimoja ambavyo kila kimoja kina Wabunge thelathini au zaidi, basi Chama chenye idadi kubwa zaidi ya Wabunge kuliko vingine ndicho kitakuwa na haki ya kuchagua Kiongozi

Kifungu cha 12(1) Chama chenye haki ya kumchagua Kiongozi wa Upinzani Bungeni kwa mujibu wa fasili ya (3) ya Kanuni ya 11, chaweza pia Kiongozi kuchagua Naibu Kiongozi wa Upinzani. wa Upinzani

Kifungu hiki (2) kinampa Kiongozi wa Upinzani Bungeni uwezo wa kuteua Mbunge wa Chama chake au wa Kambi yake ambaye atakuwa ndiye Msemaji Wakuu Mkuu kwa kila Wizara iliyopo ya Serikali. Bungeni

Kifungu cha 13(1) kinaeleza; Chama kinachounda Serikali na Chama chenye haki ya kuchagua Kiongozi wa Upinzani Bungeni, vyaweza kuteua Waratibu wa Vyama hivyo Bungeni, ambao watajulikana kwa jina la ''Chief Whip ''wa Serikali na "Chief Whip'' wa Upinzani, Vyama hivyo vyaweza pia kuchagua Waratibu Wasaidizi ambao watajulikana kwa jina la (whips) ''Assistant whips'' Idadi hiyo itaamuliwa na Vyama vyenyewe.

(2) Kazi ya Viongozi hawa, kwa upande wa Serikali ni kuwa kiungo cha mawasiliano baina ya Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni,
na Wabunge wa Upande wa Serikali; na kwa upande wa Upinzani, pia ni kuwa kiungo cha mawasiliano baina ya Kiongozi wa Upinzani
Bungeni, na Wabunge wa Upinzani.

Kwanini Rais Magufuli anawaona watu wenye kupinga na kuikosoa bajeti kuu ya serikali bungeni wanafanya makosa? Ni kosa lipi katika Kanuni linavunjwa mbunge akiikosoa bajeti na hata kusema 'HAPANA' wakati wa kuipitisha?

Rais Magufuli anasema hadharani akiwa Serengeti kwamba amewapa Butiama barabara kwa sababu walichagua mbunge ambaye bungeni amekwenda kuunga mkono kazi za serikali, hivyo Serengeti wanapaswa kujitathmini. Hii sio sawa!

Upinzani bungeni upo kutokana na matakwa ya katiba. Sio matakwa ya Ikulu au ofisi ya Rais. Watanzania wanachagua watu ambao wao wanawahitaji katika chaguzi. Kwani ni kosa mbunge wa CHADEMA kuchaguliwa kuwakilisha maoni na matakwa ya wana Serengeti?

Watu wa Serengeti wanalipa kodi sawa na watu wa Butiama. Watu wa Serengeti Rais wao ni mmoja sawa na watu wa Butiama, watu wa Serengeti walimchagua mbunge atokanae na CHADEMA, lakini kura nyingi walikupa wewe (Magufuli), kwanini usione hii si-sawa? Tusibaguane kwa itikadi zetu za kisiasa.

Mbunge wa Serengeti amefikisha malalamiko yake kwa mkuu wa nchi kuhusu namna mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti anavyotumia fedha za umma isivyotakiwa, amemshtaki kwa mkuu wa nchi, binafsi sikutegemea kusikia jibu la malalamiko yale, ulisema;

"Nadhani huyu Ryoba ana shida. Mkurugenzi Juma nakueleza utakaa hapa hapa. Na wewe unaruhusiwa kuoa wake wawili hadi wanne. Njia ni kumkomesha huyu mbunge kuoa hata dada zake atakuheshimu, ili ujenge amani ndani ya nyumba"

Rais Magufuli, hii sio kauli ya kiongozi, kwa kiongozi mwenzako mbele ya wapiga kura. Hadhira inawasikiliza bahati mbaya inashangilia dhihaka hizi. Sikuona sababu yoyote ya kiongozi mkuu wq nchi kutoa kauli hizi hadharani. Haya ni Matusi, sio tena KEJELI au dhihaka. Tujifunze kuheshimiana, ukipenda kuheshimiwa.

Rais Magufuli, mkurugenzi alisema ameshindwa kufanya kazi katika halmashauri ya Serengeti kwa sababu kuna upinzani, akasema 'amepata na ugonjwa wa BP', ukasema atakaa hapo, kwanini umlazimishe? Mpelekee mtu mwingine ambaye yupo tayari kuwatumikia watu wa Serengeti.

Pia ulimweleza mbunge wa Serengeti, Marwa Ryoba kwamba hauwezi kumteua katika serikali yako, ukatoa na mfano wenye kukera kwamba "hauwezi kuchanganya kunguru katika kundi la ndege", hii sio sahihi pia mheshimiwa Rais. Nilifikiri busara ni kumkanya mkurugenzi kama kakosea au mbunge kama kadanganya.

Mbunge kataja kero kadhaa, barabara ya kuunganisha mkoa wa Mara na Arusha; kutokuwepo kwa manufaa ya hifadhi ya Serengeti; Maji bwawa la Machura hakuna chujio; tatizo la Tembo kuvamia makazi ya wananchi; Ukosefu wa soko la tumbaku; ujenzi uwanja wa ndege; migogoro ya mipaka kati ya hifadhi na wananchi; Maeneo ya malisho kwa wafugaji

Mbunge wa Serengeti pia akaeleza kero nyingine kuhusu Migogoro ya mipaka kati ya wilaya ya Bunda, Serengeti na Butiama, ujenzi wa hospitali ya wilaya, baadae akatoa tuhuma za fedha dhidi ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti.

Mawaziri wako walitumia muda kujibu Hoja za mbunge, Waziri wa maji na umwagiliaji,Waziri wa ujenzi, Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Waziri wa TAMISEMI, naibu waziri wa madini, na watu wa Serengeti walifurahi kuona Hoja za mbunge wao zikijibiwa. Shida ipo kwenye baadhi ya ufafanuzi wa maneno yako mheshimiwa Rais;

Kusema mkurugenzi akaoe wake wengine watatu kutoka kati ya dada Zake na mbunge, ili wafike wake wanne, ni kauli za udhalilishaji. Mheshimiwa Rais unasali, ni mkatiloliki, ndio tunafundishwa hivi? Kwamba tuwadhihaki wengine tunaowazidi mamlaka?

Naamini wewe haupendi kudhalilishwa ndio maana serikali yako hii ilimkamata SUGU na MASONGA na kuwashtaki kwa makosa ya kutoa lugha ya fedheha kwa Rais, Kwanini sasa tuwafedheheshe wengine kama sisi hatupendi kufedheheshwa? Au wengine wanamiliki ngozi za chuma?

Kwanini tutenganishwe na itikadi zetu za kisiasa wakati nchi yetu ni moja tu? Hakuna 'spea' ya Tanzania. Mwingine kuwa CCM na mwingine CHADEMA sio dhambi, sio kosa la jinai, kwani ni lazima wote nchi hii tuimbe nyimbo za kusifu serikali ya awamu ya Tano kwenye kila kitu?

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inatambua uwepo wa vyama vingi vya siasa katika Taifa letu. Inatambua jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama nchi ya kidemokrasia; Tangazo la nchi yenye Mfumo wa vyama vingi Sheria ya 1992 Na.4 ib.5

Ibara ya 3(1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa. (2) Mambo yote yahusuyo uandikishaji na uendeshaji wa vyama vya siasa nchini yatasimamiwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na ya sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo.

Kwanini tusikubali kwamba Katiba yetu imetupa fursa na uhuru wa kuchagua sehemu yoyote kwa wakati wowote kufuata katika siasa za nchi yetu? Kwanini tunafikiri ni kosa mbunge wa upinzani kufikiri tofauti na mbunge wa CCM? hii nchi yetu inaongozwa na taratibu zake, sheria na katiba yetu, sio matakwa ya mtu mmoja.

Ipi sahihi? Wabunge wa upinzani kufika kwenye ziara za Rais? Au wasifike? Wakifika 'mnawananga' na kuwadhihaki. Wasipofika pia mnawasema kwa wananchi kwamba 'wanakimbia' na hawataki kusema kero za wananchi mbele ya mkuu wa nchi. Ipi sawa? Kwanini mnawamyima uhuru hawa wawakilishi kutoka upinzani?

Haitawezekana! Haitoweza kutokea watanzania wote wakapata kuwa wanachama na wafuasi wa CCM. HIVYO sio sawa kuwaona walioikataa CCM katika sanduku la kura sio watanzania na hawastahili hizo huduma za kijamii. Hatulipii kodi vyama vyetu, tunalipa kodi kama watanzania. Kusema 'kwa sababu hamkuichagua CCM' sio kauli ya 'kiuongozi'

Rais Magufuli, unakwenda mbali na kusema kwamba ulimpa mbunge wa Serengeti, Marwa Ryoba nafasi ya pili kuzungumza uone kama atakuwa amebadilisha Mawazo yake na kuhamia CCM. hii 'preemptive' sio sahihi, haikubaliki kamwe. Tusitumie majukwaa ya serikali kufanya siasa.

Mwisho; Nakupongeza kwa dhati kabisa, mbunge wa Serengeti, Mh; Marwa Ryoba Mwita kwa ujasiri wako, hata baada ya dhihaka za hali ya juu kutoka kwa Rais. Ulisimama kidete kusema ambayo yanastahili kusemwa. Historia itakukumbuka. Pole kwa kadhia hiyo, hongera kwa uvumilivu wako. Umekomaa kisiasa UMONA WEITO, UWE NU UMUKURYA INTIINA!

Hampendi kuelezwa ukweli. Kitu pekee ambacho kinaweza kuzuia mimi na wengine kama mimi kusema ni KIFO pekee, lakini watazaliwa wengine kusema, hata Mawe yataongea! Victoria Ascerta!

#MMM, Martin Maranja Masese
 
MTU mwenyewe kapata urais kwa zali la mentali
kujiona Jah people ndo nn????

viongozi badilikeni mnazingua kwa kweli...
magu umeponea chup chup kutoka kwenye kiti.bila Shaka unatambua na kujua.
unazingua kwa kauli zako...
jitahidi kutofautisha
cheo ulichonacho now. na zamani
 
Weka video clip mkuu, utiaji chumvi umekuwa mkubwa sana.
 
Kuna watu nchi hii hata wakipata matatizo wananchi wanayafutahia nakutamani matatizo hayo yawaondoe kabisa duniani.Baadhi ya viongozi wa serikali wajitathmini kwakweli kwani inawapa shida baadhi ya ndugu zao na watu wao wa karibu wanavyoshuhudia hao viongozi wakiombewa mabaya.
 
So we mpinzani Au msema ukweli.
 
Ukisikia ulevi wa madaraka ndio huu. Tatizo viongozi sorry watawala wetu huwa wanaapa kuilinda katiba wasiyoijua. Wakistuka haifai kuilinda maana inaenda kinyume na matakwa yao.
Tuna kazi kubwa sana kufikia utawala wa kisheria.
 
Hahahah Mh Rais alinifurahisha alipo mwambia mkurugenzi Juma amuoe dada wa Rioba ili Rioba ajifunze kuheshimu watu hahaha
 
Makala ndeefu hakuna cha Maana
Sijui ulitaka Rais aseme nini
Matiko nae anaomba maji na barabara wakati baje kaikataa
 
Back
Top Bottom