Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Rais Dk John Pombe Magufuli ameitaka mahakama nchini kuharakisha mchakato wa kuanzisha mahakama ya Mafisadi ili kuwashughulikia mafisadi wote. Amesema kuwa wakati akizindua Bunge, aliahidi kuanzishwa kwa mahakama hiyo hivyo ni wakati sasa wa Mahakama Kuu kutekeleza ahadi hiyo ya Rais.
Ametolea mfano kuwa Mamlaka ya Vitambulisho, NIDA imefanya ufisadi mkubwa huku ikiwa na ufanisi mdogo. Amesema kuwa vitambulisho vilivyotolewa na NIDA havina ubora na wala havina saini ya mmiliki wa kitambulisho tofauti na Vitambulisho vya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambavyo vina saini za mwenye kitambulisho. Aliwaomba Majaji kama kuna mwenye kitambulisho cha Taifa chenye saini yake anyooshe mkono. hakuna Jaji hata mmoja aliyefanya hivyo kwa vile vitambulisho vya NIDA havina saini za wenye kitambulisho. Aidha amesema kuwa NIDA wametumia zaidi ya Bilioni 176 huku wakitoa vitambulisho pungufu ya milioni mbili lakini NEC wametumia bilioni 70 tu na wametoa vitambulisho zaidi ya milioni 22 tena vyenye ubora.
Vile vile amesema kuwa wakati anaingia madarakani, ilikuwa ni vigumu kwa serikali kulipa mishahara ya Watumishi wakati bandarini watu wakitorosha makontena na kuikosesha serikali mapato mengi.
Amesema kuwa anatambua kuwa mafisadi yanayo uwezo wa kuhonga majaji na mahakimu ili yashinde kesi. Hata hivyo amesema kuwa ana imani na Jaji Mkuu na hivyo ni matumaini yake kuwa atasimamia walio chini yake ili haki itendeke.
Kwa kweli kutoka ndani ya moyo wangu, napenda kukiri kuwa Watanzania tumepata Rais. Huyu Magufuli ndiye tuliyekuwa tunamsubiri Watanzania kwa hamu baada ya Sokoine na Nyerere. Shime Watanzania tumuunge mkono ili nchi isonge mbele