Habari waungwana,
Leo Rais Magufuli anazindua mabweni mapya ya chuo kikuu cha Dar-es-Salaam ambayo aliombwa na kiongozi wa chuo hicho, Jakaya Kikwete.
Fuatana nami kujua kitachojiri UDSM.
=====
Watu kadhaa wameshaongea akiwemo mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda, makamu mkuu wa chuo, Lwekaza Mukandala, Rais wa serikali ya wanafunzi wa UDSM.
Anaeongea kwa sasa ni waziri wa ulinzi, Hussein Mwinyi na anaelezea ushiriki wa jeshi la kujenga taifa katika mabweni hayo ambapo walijenga uzio kwa gharama nafuu pia amezungumzia ushiriki wa jeshi hilo katika miradi mingine ikiwemo shule za Bukoba.
Pia ameongea waziri wa ujenzi, Prof. Makame Mbarawa na ameahidi kuendelea kuisimamia TBA. Kwa sasa anaongea waziri wa elimu, Prof. Joyce Ndalichako.
Ndalichako: Nakupongeza mheshimiwa Rais kwa kutoa kipaumbele kwa sekta ya elimu na majengo ni mazuri yenye mandhari ya kuvutia.
Natamani ningekuwa na maneno mengine ya kuelezea hii furaha, mwenyezi Mungu akupe maisha marefu na serikali yetu chini ya awamu ya tano inawapenda sana vijana.
========
Anaeongea kwa sasa ni Rais John Magufuli na ameomba watu wasimame dakika moja kuwakumbuka askari nane waliouawa Kibiti.
Magufuli: Mimi ha pa ni nyumbani, mimi ni mtoto wa hapa, nikiangalia nawaona walimu waliofanikisha mimi kufika hapa. Tutaendelea kutoa mikopo kwa wanafunzi.
Tufikie mahali, TCU iwe mdhibiti lakini watoto wawe na haki ya kuchagua vyuo wanavyovitaka, kuna vyo vinalazimisha kupata wanafunzi kwa saabu wanapokea mkopo, muwaache wanafunzi wachague vyuo wanavyovita, vyuo visivyochaguliwa vife. Nina uhakika mkiwaacha, chuo cha Dar, UDOM, SUA na vyuo vingine vyenye qualification vitapata wanafunzi wengi.
Najua sitawafurahisha watu wengi na mie siko hapa kuwafurahisha, vyuo vya serikali vijae tu wanafunzi, ishu sio kuwa na vyuo vikuu 100. Unaweza kuwa na vyuo vichache na end product ikawa nzuri.
Nikishafungua Mloganzila, wanafunzi wa medicine wahame hapa. Najua VC unahitaji wanafunzi wengi lakini wanafunzi wa medicine jiandae kuwaachia.
Kulikuwa na mabasi ya chuo, hayo mabasi yako wapi, kama yamepotea, walioanzisha hayo mabasi walikuwa wamekosea? Kweli chuo kikuu hiki kimeshindwa kununua mabasi?
Nitoe ombi kwa uongozi wa chuo kutafuta uwezekano wa kutafuta mabasi hata matano, kikubwa lazima tuangalia maslahi ya wanafunzi hawa.