Rais Magufuli awataka wenye viwanda kulipa kodi ndogo na wanaoagiza kutoka nje kulipa kodi kubwa

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
775
1,332
fca8ff75-25cc-47e2-b025-f374fd7bbf07.jpg
Rais Magufuli ametoa tuzo za wazalishaji bora viwandani kwa mwaka 2015 huku Kampuni ya Bia Tanzania TBL ikiibuka mshindi wa jumla.

Ambapo amewataka wenye viwanda nchini kulipa kodi ndogo na wale watakao agiza toka nje ya nchi kulipa kodi nyingi ili kukuza viwanda vya ndani.



 


Rais DR.JOHN POMBE MAGUFULI ametoa tuzo za wazalishaji bora viwandani kwa mwaka 2015 huku Kampuni ya Bia Tanzania TBL ikiibuka mshindi wa jumla.

Ambapo amewataka wenye viwanda nchini kulipa kodi ndogo na wale watakao agiza toka nje ya nchi kulipa kodi nyingi ili kukuza viwanda vya ndani.
 
Haya tutaagiza tu ila hata huko tutapouza tutanunua kwa bei ndogo ili hizo kodi zisituathiri
Ila amini viwanda vyenu haviwezi shindana na sisi
Kama chupi tu mmeshindwa mtaweza kipi
 
Leo kaona mbali kidogo. Hakuna sababu ya kuzuia bidhaa za kutoka nje. Linda viwanda vyako kwa kuwapunguzia kodi ili waweze kushindana na bidhaa za nje. Sio kusema hamna kuingiza bidhaa. Sukari imemshtua
 
Aangalie tu na bia isije kuadimika kama sukari, kina Kitwanga hawatamwelewa.
 
Nilitarajia hii ingekuwa fursa ya kutoa policy kwa urefu kuhusu uwekezajj,viwanda na uchumi kwa ujumla,kumbe tumeishia kujipongeza na viwanda vilevile tu!!! Nilitaraji angeweka msimamo kuhusu linkage kati ya Kilimo na viwanda na kutoa hamasa maalum na incentive maalum kwa maeneo Maalum ya nchi kwa Kilimo Maalum, haya maeneo ndio ya kutoa policy statement za miaka mitano zilizochambuliwa kwa kina na wataalam!!! Tanzania ya viwanda ni ndoto!!! Ni ileile oooh ile ile
 
Kwa kiwanda cha pombe hakiwezi kufeli maana ni kitu muhimu cha kupotezea muda, bora kukitoa kwenye listi kinashinda kila mwaka.
 
Maeneo yanayowakutanisha rais na wenye viwanda....ilitakiwa wadau wote wawepo,wadau wa Kilimo wakiongozwa na waziri wao,wadau wa viwanda na waziri wao,wawe na kongamano la siku mbili tatu,waje na suluhisho la kwa mini tuagize mafuta nje wakati tuna uwezo wa kulima mawese kigoma!wakati tuna alizeti singida,wakati tuna Pamba kanda ya ziwa,waulizwe ushiriki wao katika Kuondoa adha ya kuagiza mafuta,adha ya kuagiza sukari,adha ya kuagiza nguo,adha ya mahindi kuoza ghalani ruvuma na rukwa/katavi, ubalozi wa China ungeweza kusaidia kuleta kampuni kubwa zi
 
Sijasikia akizihoji taasisi za serikali kama SIDO na TIRDO zinashiriki vipi kuhakikisha ndoto zake za Tanzania ya viwanda zinatimia
 
Kuna watu mmeshuka maelezo mengi yanayohusu mambo muhimu yaliyokuwa yanapaswa kuzungumzwa na rais, mnayo clip nyingine ya maelezo yote aliyoyatoa rais au nanyi mmesikiliza hicho ki-clip kifupi kutoka itv? Mimi nasubiri kusikia hotuba yote na kama kuna mtu tayari anayo atuwekee ili tuchambue vizuri! Kwa ufupi nimefarijika na maneno hayo mafupi ya rais kulingana na hako ka-clip kutoka itv!
 
Hii hoja inahitaji mjadala mpana ili kweli tuamini tunajengewa Tanzania ya viwanda na sio porojo,kulikuwa na hoja wakati wa kampeni kwamba walionunua viwanda na hawakuviendeleza watanyanganywa....hakuna kauli mpaka sasa,hakuna kauli ya kufufua viwanda iliyotoka,anasema bidhaa kutoka nje ziongezwe kodi,hilo kwenye bajeti halionekani,na hata jinsi ya kufanya haipo ili mwananchi asiumie.....siasaaaaaaa tupu
 
Hii hoja inahitaji mjadala mpana ili kweli tuamini tunajengewa Tanzania ya viwanda na sio porojo,kulikuwa na hoja wakati wa kampeni kwamba walionunua viwanda na hawakuviendeleza watanyanganywa....hakuna kauli mpaka sasa,hakuna kauli ya kufufua viwanda iliyotoka,anasema bidhaa kutoka nje ziongezwe kodi,hilo kwenye bajeti halionekani,na hata jinsi ya kufanya haipo ili mwananchi asiumie.....siasaaaaaaa tupu
Soma tena kutoka kwenye riport iliyotolewa na kaimu mkurugenzi wa Ikulu!
 
Back
Top Bottom