barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,726
- 32,818
Leo Rais JPM alikuwa Mkoani Shinyanga katika Wilaya ya Kahama,inajulikana kuwa Kahama ni moja ya Wilaya yenye madini pamoja na Geita.Katika hotuba zake,JPM leo ametoa "Go ahead" kwa mamlaka husika wakiwemo NEMC kuhakikisha kuwa wananchi wanagawiwa "Magwangala" yote yanayotoka Mgodini.
Kwa wanaotoka kandokando ya migodi wanafahamu kuwa "Magwangala" ni yale mabaki ya udongo unaotokana na kusafishwa kwa dhahabu,kwa miaka mingi watu wa mwambao mwa migodi wamekuwa wakifa kwa kupigwa risasi au kuumwa na mbwa wa walinzi wa migodi kwa kuvamia na kuchukuwa magwangala.Rais amewaagiza Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa Wilaya na Mamlaka ya mazingira NEMC kuhakikisha kuwa utaratibu unaandaliwa ili watu wapate mgawanyo huo wa "magwangala".
Rais JPM anasema haiwezekani hao wawekezaji waje hapa,wabebe madini yatu na bado waondoke na mabaki ya udongo wa madini yetu,kuanzia sasa ni mwisho kwa wananchi kuzuiwa kuchukuwa magwangala,maana madini ni ya Watanzania na bila hayo madini kuwa Tz hata hao wazungu wasingekuja.Rais anasema hao wazungu walikuja kufuata dhahabu na si "magwangala",kama hawawezi kuyaacha hayo basi wakatafute sehemu nyingine