Rais Magufuli atoa onyo kwa Wakurugenzi

Rais Magufuli atoa onyo kwa Wakurugenzi

mamayoyo1

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
1,011
Reaction score
1,019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaonya Wakurugenzi ambao watanaoesha nia kudai ushuru kufuatia uamuzi wa Serikali, kununua zao la korosho kwa bei elekezi ya shilini 3300, baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya wakulima na wafanyabiashara wa korosho.


Magufuli ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Mtwara wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara kutoka Mtwara kuelekea Newala na Masasi, ambapo amesema serikali haiwezi kuamua kuwasaidia wananchi halafu Halmashauri ijitokeze kutaka ushuru.

"Halmashauri mmeshindwa kusimamia korosho, baada ya kupewa bei nzuri wanapewa 1500, tukasema hapana tukakopa ili tuwalipe, nione Mkurugenzi ananiomba hizo hela, aone kama ataendelea kuwa Mkurugenzi, utaombea kijijini ukiwa unalima".

"Haiwezi Serikali imepanga bei ya korosho 3300, halafu ianze kulipia kodi kwenye Halmashauri ambayo ilishindwa kununua korosho, mkitaka ushuru msimamie vizuri bei ya korosho, siwezi nikakusanya hela mikoa mingine nije niwalipe nyinyi."Amesema Rais Magufuli
 
Amekosekana wa kumsifu!

Wapi dhana ya kulipa kodi!!
 
Njoo na Tanga halmashauri ya jiji inatoza ushuru kwa wavuvi, wachuuzi, wasafirishaji hadi wabebaji! Na hapo unalipa kodi TRA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaona uchungu kulipa kodi, anafikiria sisi tunaolipa kodi na hajali maslahi yetu?
 
Huyu ni kiongozi anayewaza kwa kiwango Cha beseni kuongoza bahari
 
Tuna rais mwenye uzembe wa kufikiria wa kiwango cha juu mno. Halmashauri za mikoa ya kusini miaka yote zimekuwa zikipanga bajeti zao kwa kutegemea ushuru wa mauzo ya korosho.

Yeye kwa kupenda sifa akajitia kuzinunua korosho. Inabidi alipe ushuru.. Hakuna namna nyingine.
 
Back
Top Bottom