Rais Magufuli ataleta Mabadiliko makubwa, watanzania tumuunge mkono

Aug 21, 2016
33
504
JPM ATALETA MABADILIKO MAKUBWA TANZANIA WATANZANIA TUMUUNGE MKONO.

Wakati wa uongozi wa awamu ya nne kulikuwa na mijadala mingi, mikubwa na midogo kuhusu mustakabali wa nchi yetu. Kulikuwepo na mazungumzo ya muda mrefu kuhusu mwelekeo wa jumla wa taifa letu, maadili ya taifa letu, uchumi wa nchi yetu nakadhalika. Ungesikiliza mazungumzo ya watu wengi wakati huo na ukisoma magazeti yetu, ilikuwa ni dhahili kuwa nchi yetu ilikuwa imekwama. Nchi yetu ilikabiliwa na changamoto nyingi hususan kuporomoka kwa maadili na tunu za taifa, kuongezeka kwa umaskini na tofauti ya kipato baina ya wachache walionacho na wengi wasionacho. Kuibuka kwa mgawanyiko katika misingi ya makundi ya kisiasa na jamii. Kuibuka na kushamiri kwa utamaduni na siasa chafu, malalamiko kuhusu Muungano wetu na mengineyo.

Mmomonyoko wa maadili ulidhihirishwa na ongezeko kubwa la rushwa na ufisadi, uvunjaji wa haki za binadamu, tabia na hulka ya viongozi kushindana kwa kujilimbikizia mali na kutoheshimiana. Mambo haya yaliondoa uzalendo, uadilifu, ufanisi, matumaini na imani ya wananchi kwa mfumo wa uongozi, viongozi wao na Serikali yao.

Ni dhahiri, Tanzania si nchi maskini isipokuwa inabidi ijipange katika matumizi ya rasilimali zake kama maliasili kwa ajili ya maendeleo ya taifa. Wananchi wengi walionyesha wasiwasi kwamba sehemu kubwa ya rasilimali au maliasili ilikuwa inawanufaisha wawekezaji wa kigeni na washirika wao ambao wana hisa na wachache wenye mamlaka ya kiserikali katika maeneo husika. Ni dhahiri uwekezaji huu ni unyonyaji uliopingwa awali na Azimio la Arusha.

Nchi yetu pia ilikabiliwa na inakabiliwa na changamoto za ukuaji wa uchumi usiogawanyika kwa usawa kunufaisha wananchi wote (equity). Wachache wananufaika na hivyo pengo kati ya maskini na tajiri linaongezeka. Tunashuhudia pia utajiri wa maliasili uliporwa kutokana na kushamiri kwa ufisadi na rushwa, kukosekana kwa uwajibikaji wa kisiasa na kiutawala na kuwepo kwa mkanganyiko katika asasi za utawala. Uwezo wetu wa kujiletea maendeleo tunayotaka ulikuwa ni mdogo. Nchi yetu ilibaki ni tegemezi kwa wahisani na wawekezaji kutoka nje.

Kulikuwepo na wimbi la vijana kuhamia mijini kwa matumaini ya kupata maisha bora, lakini wengi wao waliishia kuwa vibaka na wengine kuwa watumiaji wa dawa za kulevya. Idadi ya wasichana wanaojiuza mitaani iliongezeka. Haki za binadamu na za jamii hazikupewi kipaumbele na uzito wa matukio ya mauaji ya albino na hatua zisizoridhisha zilizochukuliwa na serikali ni mfano ambao ulioonyesha jinsi serikali ambavyo haikuwa makini hata kusababisha wananchi kukata tamaa. Aidha, haki za wageni zililindwa na kuheshimiwa kuliko za wenyeji. Wageni walitetewa kama wavunaji halali wa maliasili, lakini wenyeji wao ni wavuvi haramu, wawindaji haramu, na wavamizi wa maeneo yenye madini.

Changamoto nyingine kubwa ilikuwa ni kuongezeka kwa migongano ya mara kwa mara kati ya Serikali, Bunge na Mahakama. Mfano halisi ni pale ambapo Bunge lilishindwa kuisimamia Serikali kikamilifu kwa wabunge wa chama tawala kushinikizwa wakubaliane nayo au waitetee, hata ambapo ilikuwa na makosa katika utekelezaji wa shughuli zake. Ni dhajiri nchi yetu ilihitji mabadiliko.

Kwa muhtasari, wakati wa Mwalimu Nyerere nchi yetu ilikuwa maskini, lakini yenye upeo, mwelekeo na uwezo wa kisiasa ambao uliwashangaza wengi. Ilichukua msimamo thabiti kujenga ujamaa na kujitegemea, kuunga mkono na kushiriki katika mapambano ya ukombozi kusini mwa Afrika na kupinga siasa za udhalimu popote ulimwenguni. Nchi yetu pia ilijiamini kwa matamko, vitendo na kisiasa. Wakati huo kulikuwa na mwamko mkubwa ndani ya wananchi juu ya kufanya kazi ili kujitegemea na kuinua hali ya maisha yao. Kuanzia zama za rais Mwinyi hadi sasa nchi yetu imeendelea kuwa maskini na imezama kwenye utegemezi badala ya kupambana kwa dhati kuinua hali ya maisha ya wananchi. Ni Tanzania yenye tabaka zinazozidiana mali na kipato. Ni Tanzania iliyogubikwa na rushwa na ufisadi mkubwa. Ni Tanzania ilikuwa na ombwe la uongozi.

Kutokana na changamoto hizi, nchi yetu ilihitaji sana uongozi imara wa chama tawala, unaoweza kutoa mwelekeo wa taifa kwa ujumla.

Watanzania wasomi, wanasiasa, wanaharakati na wengine wengi walilalamikia ombwe (vacuum) la uongozi. Hili ni tatizo kubwa. Katika kitabu cha Uongozi wetu na hatma ya Tanzania, Nyerere alisema hulka huchukia ombwe (nature abhors a vacuum). Hata siasa huchukia ombwe. Kama uongozi ni mbovu, upoupo, au upo kama haupo, au upo kwa maslahi ya fulanifulani tu, watatokea watu waujaze uwazi uliopo. Hauwezi kuachwa hivihivi. Uongozi mbovu ni kama mzoga. Una hali ya kukaribisha fisi na mainzi. Tusidhani kuwa hulka ya siasa yetu ni tofauti na hulka ya siasa za watu wengine. Watu hawatakubali kuvumilia uongozi mbovu kwani wakifanya hivyo, wanajua fika watavuna “matunda ya uongozi mbovu.”

Nchi yetu ilikuwa imefikisha miaka 19 tangu iingie katika mfumo wa vyama vingi. Ni kweli kulikuwepo na vyama vya upinzani vyenye wanachama uzalendo na wenye hamu ya kuona mafanikio kwenye taifa letu, lakini vingi katika hivyo bado mpaka wakati huo havikuweza kuonyesha uwezo wa kushika madaraka na kuwa chama tawala mbadala. Demokrasia na mwenendo wa baadhi ya vyama vya siasa na ndani ya baadhi ya vyama vyenyewe imekatisha tamaa Watanzania.

Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015 ajenda ya kutaka mabadiliko ilikuwa ni moja ya ajenda kuu kwenye vyama vya upinzani na chama tawala. Nyerere aliwaasa watanzania na hasa alikitahadharisha chama tawala kwamba, “Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyaona wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM”. Chama tawala CCM kiliichukulia suala la mabadiliko kwa umakini sana. Katibu Mkuu wa CCM alizunguka nchi nzima akiwaeleza watanzania mabadiliko yaliyohitajika. Kwa kifupi alikifufua Chama cha Mapinduzi na watanzania wakakiamini tena. Lakini pia CCM ilichukua hatua ya kuwaondoa waliotuhumiwa kwa ufisadi na kutoa rushwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM. Harufu ya ufisadi na rushwa ndani ya CCM ikawa imepungua, kwani mtakumbuka wagombea wengi walikuwa wanapita kwenye makanisa na misikiti wakitoa rushwa. CCM ikawaondoa kwenye kugombea urais.

Wakati CCM imechukua hatua hizi, Chadema na UKAWA wakawa na mabadiliko ya kuzungusha mikono lakini ndani ya mioyo yao hawakutaka mabadiliko. UKAWA na Chadema waliokuwa na madai ya muda mrefu kwamba wanao ushahidi wa wale waliotuhumiwa ufisadi wakawakaribisha kwenye chama na kuwapa heshima ya kugombea nafasi za juu, ajenda ya udfisadi ikafa.

Tarehe 25 Oktoba watanzania wakatoa maamuzi, Mabadiliko Bado yatapatikana Ndani ya CCM na siyo Nje ya CCM.

Kutokana na mabadiliko ya uongozi yaliyotokea chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli watanzania wengi wamepata matumaini makubwai. Yale ambayo niliyapigania na kuyapigia kelele kwa wakati huo hadi kuhama CCM, kwa sasa chini ya uongozi wa Rais Magufuli yanatekelezwa. Ndiyo sababu ya msingi ya uwaomba watanzania wamuunge mkono Rais Magufuli na serikali yake.

Kwa muda mfupi wa JPM, serikali imeonyesha kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na changamoto nyingi:

Je ni yapi yatufanye tuandamane kuipinga serikali Wakati kuna mabadiliko makubwa na dhahiri?

Je ni nini kinawaudhi, JPM kuchukua hatua dhidi ya ufisadi bandarini uliokuwa uapoteza mabilioni ya fedha ?

Je ni udikteta kupiga vita uzembe na kutumia madaraka vibaya kwa viongozi mfano kujilipa mishahara 17 mtu mmoja?

Je ni ni kinawaudhi, kuchuku htua dhidi ya watumishi hewa serikalini na kwenye hlmashauri zetu ?

Je tuandamane kupinga kuboreshwa kwa huduma kwenye hospitali zetu ?

Je tuandamane kupinga kuletwa kwa ndege kwenye ATC ?
Je tuandamane kwa ajili ya hatua zilizochukuliwa kwa watoto kupata madawati mashuleni ?

Je tuandamane kwa hatua ya serikali kuchukua hatua ya kuhakikisha wachimbaji wadogo nao wananufaika na madini, kwa kupewa mchanga ?

Chadema na UKAWA wanadai demokrasia inaminywa. Je kuna demokrasia pana ndani ya Chadema ? au CUF ? Mgombea urais wa Chadema alipatikanaje ? Hiyo ni demokrasia pana ?

Je yaliyotokea CUF ni kielelezo cha demokrasia pana?

Nchi yetu ilipitia misukosuko mikubwa na changamoto nyingi, ni mhimu Kwa watanzania na kuzuia upotoshaji na uchochezi unaofanywa na Chadema.
 
Yule yule mchumia tumbo.. Njaa kali jamani hahahaha acha kabsa
 
Hata ukiandika kitabu wewe huaminiki. Huna msimamo. Kwenye dalili ya chakula ndiko unapopapenda. Sintashangaa kesho ukianza kumponda Mheshimiwa pale utakapogundua kuwa mwelekeo wa chakula umebadilika.
 
Ushakatwa mkia, huna effects zozote nje au ndani ya chama ulichopo!
Mh.Rais anasema hapa kazi tu, ujiajiri sahau kuhusu uteuzi!
 
roho Yangu Inaniuma Kuona watu kama nyinyi Pamoja na kisomi Chenu Bado Watumwa kwa wanasiasa

Iv pamoja na elim yako Unashindwa kusema ukweri Wa Nchi Yetu Kuwa imefika mahali Pabaya kweri Jaman

Umeandika Haya ili upate U DC au

Hukuona Changamoto Wapatazo Vijana kuhusu Ajila

Mikopo Kwa Wanafunzi vp

Au Kwakuwa wee watoto wako wapo Nje ya nchi wanasoma au walisoma Huko

Acha njaa wee Mtu Mzima Onaongea vitu Vya Kipuuz kabisa

Ungekuwa Karibu yangu Ningekuchapa Bakola 12 ukamuoneshe MKEO
 
Hoja yako ni muhimu na ni elimu tosha KWA vipofu wa kupambanua mambo! Najua wanachadema watakupinga KWA hoja maana wengi ni vipofu, wakiambiwa jambo na kipofu mwenzao mbiwe wanashangilia hata kama ni jambo la hovyo hovyo wao shangwe.
 
Mh, mpenda zoe, hata useme nini mimi siwezi kukuamini kamwe, unapo zungumzia maendeleo usiangalie hapa mjini lipi alilo lifanya mh limeleta impact moja kw moja watu wahali yachini mwaka sio mdgo, mkuu nenda singida hosptali hazina dawa, we unaongelea ndege? ndege angalia wanao zipanda ni watu wa namna gani mkuu? tuache porojo za kujipendekza hali yamaisha ni ngumu mpka kwa watumishi wa uma, huwez fanya kazi ukaishi kama mfungwa.
 
Mkuu mpendazoe naomba unijibu haya pamoja na kuwa mie sio mwanasiasa.
1. Umezungumzia kushuka kwa maadili katika serikali zilizo pita. Je ni mambo gani ambayo serikali ya jpm inafanya ili kuimarisha madili kwa vijana kama madawa ya kulevya, kujiuza pamoja na wimbi la vijana kuhamia mjini. Mimi ninacho jua kwanza angeimarisha kilimo na viwanda ili watu/ vijana wengi waweze kujiajiri na kuajiri wengine.
2. Muundo wa serikali haufwatwi kwa sasa. Imefika hatu nchi inaendeshwa kwa hisia. Nadhani JPM anahitaji baraza la washauri. Maana kunamuda anafanya maamuzi binafsi ambayo madhara yake kw taifa ni makubwa kuliko tunavyo dhania.
3. Serikali inahitaji planing. Yaani labda saivi kipaumbele ni hiki kama alivyo ainisha mkuu kuwa yeye seriakali yake ni ya viwanda. Lakini napatwa na kigugumizi pale nipoona kiwanda/ viwanda vikijitahidi kusimama vyenyenyewe pasipo msaada wa serikali. Ni kweli tunataka wawekezaji kuwekeza katika nchi yetu. Lakini hatujatengeneza mazingira ya wao kuwekeza. Mfano swala la umeme. Kabla ya kupanga kuwaita watu kuwekeza ilitakiw Tanzania kuzalisha umeme mwingi ambao utatosheleza viwanda vitakavyo jengwa swala ambalo linafanyiwa utekelezaji lakini ni kwa kusua sua.
 
Back
Top Bottom