Mkuu hatukatai hata akitawala miaka 200 sio shida kwani sio wote tunapenda kuwa marais. Ila tunahoji unafuu ni upi katika maisha yetu mpaka tutake atawale zaidi ya miaka 5 na iwapo atafanikiwa basi atawale 5 mingine ya mwisho? Hayo madini mpaka sasa hatujaona mafanikio zaidi ya kulianzisha. Ilibidi tusubiri tuone matokeo chanya ya maisha yetu hapo ndio tufikirie hilo mnalotaka nyie. Nakupa mfano mdogo tu. Kabla ya yeye kuingia madarakani alikuta sukari ni 1,800-2,000@kg. Akalianzisha kama alivyolianzisha sasa kwenye madini, matokea ya vurugu ile sukari sasa imepanda mpaka 3,000@kg na amekaa kimya!! Sasa kama suala hilo dogo tu liko hapo tukimuongezea miaka zaidi ya 10 si ndio tutanunua sukari 50,000@kg. Ile 50m kila kijiji sasa hivi wala haiongelewi tena.
Ni kipi kimekuwa nafuu ambacho tunaweza kweli kutembea kifua mbele kwamba sasa kweli tunajivunia? Ni kweli kuanza kufuatilia hao mafisadi wa mali zetu ni jambo jema. Je hiyo pekee italeta unafuu kwenye maisha yetu au ni yeye atapata sifa binafsi na kwa sasa anataka sifa hiyo pia chama chake kizipate. Ilibidi tusubiri wangalau akiwa amefikisha miaka 8 madarakani hapo tungeweza kuwa kwenye nafasi ya kutaka aongezewe muda.